Hivi ni kweli kabla ya hii mipaka ya kisiasa, Moshi ilikuwa Kenya na Mombasa ilikuwa Tanzania?

Kabla ya ukoloni nchi iliyokuwepo ni Zanzibar pekee, na Mombasa ilikuwa sehemu ya Zanzibar, so ni kweli Mombasa ilikuwa sehemu ya Tanzania kwa sababu Zanzibar ni Tanzania kwa sasa
Ukiwauliza kabla ya waarabu kuja zanzibar
Hapi kulikuwa na watu gani?hawana majibu

Historia inauotakiwa kufundishwa ni ile kabla ya ukoloni/biashara ya utumwa

Ova
 
Huu ndo uungwana. Mwandishi. Tuliosoma hiki kitu chuoni,tunakuelewa
 
Mrangi,
Unauliza huku shingo umetoa.kuwa kabla ya Waarabu kuja Zanzibar na hapa nadhani unawakusudia Waomani Zanzibar ilikuwa inakaliwa na watu gani?

Hili si swali la kumshinda mtu yeyote kulijibu.

Visiwa hivi vya Zanzibar na Pemba wakiishi watu weusi.

Kuna kitabu, ''Omani Sultans in Zanzibar,'' (1988) kimeandikwa na Ahmed Hamoud Al-Maamiry.

Katika kitabu hiki anaeleza kuwa Waarabu walifika Pwani ya Afrika Mashariki miaka mingi sana kabla ya Wazungu na Wareno walipowasili 1498 waliwakuta Waarabu ni wenyeji sehemu hizo pamoja na hii Zanzibar.

Wareno waliikalia Oman kutokea India mwaka wa 1508 na mwaka wa 1650 Waomani walifanikiwa kuwatoa nchini kwao.

Wazanzibari wakaomba msaada Oman iwasaidie kuwaondoa Wareno nchini kwao na hili lilifanyika bila ya masharti yoyote.

Waomani waliizingira ngome ya Wareno Fort Jesus kwa siku 33 na mwisho Wareno walisalimu amri na kuondoka Pwani ya Afrika ya Mashariki 1698.

Hivi ndivyo walivyopatikana masultani 12 waliotawala Zanzibar.

Lakini muhimu ni lazima utambue kuwa kufikia hapo Waarabu na Waafrika walishachanganya damu na hivi leo ndiyo unawaona Wazanzibari hawa ambao watu kutoka Tanganyika wanapenda kuwaona kuwa ni wageni Waarabu.

Kwa bahati mbaya wapo wasiopenda udugu huu na hili na wanatamani sana kizazi hiki kinachokwenda nyuma karne na karne kionekane kuwa Zanzibar si kwao, visiwa hivi vya hawa Waafrika tena wametokea Tanganyika haizidi hata miaka 100 kiasi ukimuuliza wapi kaburi la babu yake hana pa kuonyesha.

Ndiyo hawa leo wanauliza hapa kabla ya kuja Waarabu Zanzibar walikuwa wanaishi watu gani?

Jibu nimelitoa kuwa katika visiwa hivi wakiishi watu weusi.

Hawa watu weusi wakachanganya damu na Waarabu na ndiyo hawa Wazanzibari waliopo Zanzibar hivi sasa karibia karne saba.

Ukweli huu hawautaki.

Wanajifanya hawajui kuwa kuna Mzanzibari Riyami ana damu ya Kimanyema.

Mzanzibari Barwani ana damu ya Kimakonde.

Baadhi ya hawa mimi ni ndugu zangu na mimi sina chembe ya damu ya Kiarabu.

Wapo wasiopenda Zanzibar hii na ipo sababu lakini hawana ujasiri wa kusema.

 
Nyoosha vizuri hapa. Waarabu wa Oman walifikia Pemba miaka hiyo uliyoitaja na kule Unguja kulikuwa na wenyeji ambao ni Waafrika chini ya Sultani wao Mwinyimkuu. Then Wareno walitishia kutaka kuikalia Unguja ndipo Sultani Mwinyimkuu akaomba msaada kwa Sultan wa Waoman waliopo Pemba. Sultan wa Oman kweli akaweza kutetea kisiwa cha Unguja kisikaliwe na Wareno.

Baada ya ushindi Sultan wa Pemba akamuuliza Sultan Mwinyimkuu wa Unguja kuwa atamlipa nini baada ya yeye kuwapiga Wareno? Mwinyimkuu akamuambia nitakupa watu wangu wakulimie bure. Sultan wa Pemba hakufurahishwa na jibu hilo ndipo akamuua Mwinyimkuu kwa gobole.

Kama nimekosea naomba radhi maana nilisikia tu hiyo sehemu kutoka kwa wana Historia wakongwe
 
Stux...
Nifahamishe ninyooshe nini kabla sijajibu hayo mengine.
 
Imekuwepo migration ya watu pale kwa muda mrefu. Julius Nyerere,kwa mfano,babu yake( grandfather) ni mjaluo.
Mama Maria Nyerere,kwa mfano,babu yake ni mjaluo.
Lakini Watanzania tukiitaka Mombasa,labda Wakenya watakuwa very happy kutupatia. Jomo Kenyatta alikuwa ana complain sana kuhusu Mombasa.
 
Kabla ya ukoloni nchi iliyokuwepo ni Zanzibar pekee, na Mombasa ilikuwa sehemu ya Zanzibar, so ni kweli Mombasa ilikuwa sehemu ya Tanzania kwa sababu Zanzibar ni Tanzania kwa sasa
Hata kilomita kumi za ukanda mzima wa pwani ya Tanganyika ni mali ya Zanzibar, arafu Zanzibar sio Tanzania, ila Tanzania ni Zanzibar na Tanganyika,mnawapotosha wajukuu.
 
Aisee🤣🤣🤣
Babu yake Nyerere ni Mjaluo?

Mama Maria Nyerere Babu yake Jaluo.

Uzanaki na Ujaluo wali na wali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…