Hivi ni kweli kuna maisha baada ya kifo?

Sasa utakua upande upi endapo dini itakinzana na sayansi, kwa mfano ishu ya flat earth na jua kuzunguka dunia
Mimi sio Astronaute. Mambo ya flat earth ama jua kulizunguka jua huwa sifuatilii kabisa. Hapa nimefuatilia kwa sababu mimi ni mwanasayansi ya mwili wa mwanadamu. Tukiwa chumba cha upasuaji tukiwabadilishia watu figo,Ini na after unaona mgonjwa karecover. Unasema Asante sayansi. Ukiwa na mgonjwa wa Covid ambae alikuwa tubed. Siku mnaondoa tube na mgonjwa anaweza kupumua mwenyewe mnasema Yes. Kuna wakati mwingine mnafail mgonjwa anafariki dunia. Lakini mnakuwa mmejaribu kila njia kuokoa maisha.
 
Nikwasababu kuna neno "vimejitosheleza" lililotangulia kabla ya hilo neno nililoandika mimi

Nikuulize wewe, neno "vimejitosheleza" unalifafanua vipi?
Jibu maswali niliyo kuuliza.
 
Wasomi kama nyie mnaoamini miujiza ndio mnaifanya afrika igande.. mungu unayemtaja anayejua yote ndio huyu alikua anahamasisha utumwa na biashara ya utumwa?
 
mimi naamini in law of physics, evolution and natural selection
 
Madr kama nyinyi hakawii kushawishi watu waende kwa mganga[emoji2357][emoji2357][emoji2357][emoji2357] we unajua mwili wa binadamu unavyofanya kazi halafu unatupia neno msaada wa mungu
 
Umeandika kwamba wanasayansi "Kuna wakati mwingine mnafail mgonjwa anafariki dunia. Lakini mnakuwa mmejaribu kila njia kuokoa maisha".
Sasa je, hayo maisha mlioshindwa kuokoa baada ya mgonjwa kufariki dunia yalitoka wapi na yanaenda wapi?
 
Unashindwa kwenda kutubu kwani padre msimamia kitubio ndio mliegombania demu jana yake.
 
Ukifa hujui Kama unekufa una-transform na kuingia katika ulimwengu mwingine.

Uhakika ni kuwa Maisha baada ya kifo yapo Ila yapoje hakuna ajuaye.

Ni ishu ya ku-transformation
Total contradiction! yapo lakini hakuna ajuaye yapoje! Taarifa ya uwepo unao uthibitisho zaidi ya simulizi za bible? Unaweza thibitisha kisayansi?
 
Umeandika kwamba wanasayansi "Kuna wakati mwingine mnafail mgonjwa anafariki dunia. Lakini mnakuwa mmejaribu kila njia kuokoa maisha".
Sasa je, hayo maisha mlioshindwa kuokoa baada ya mgonjwa kufariki dunia yalitoka wapi na yanaenda wapi?
Hiyo ndiyo inaonyesha kuwa uwezo kwa mwanadamu una limit. Ila tena jiulize Yes tumekubali kuna limit. Na ndiyo maisha ya mwanadamu ya mwisho na mwisho ni kufa. Mtu akifa ndo kafa baada ya hapo ni decomposition.
 
Nilifanya surgery miezi miwili iliyopita, niliwekewa general anesthesia (ganzi ya kulala kabisa).

Niseme tu, mimi sikuwa na Imani na mambo ya nafsi, roho, dimensions zingine n.k ingawa nilikuwa open to proof and understanding, Lakini toka nimeamka kutoka kwenye ile surgery, ni kama nimeamka hivi, ni kama nimezinduka, nahisi Kuna ukweli fulani ambao siujui/hatuujui juu ya haya maisha, a certain reality beyond what we see. Probably waliotuletea hizi dini walikuwa wamejaribu Kwa uwezo wao kuelezea ukweli huo.

Ilikuwa kidogo nianzishe thread niulizie experiences za watu waliowahi kuwekewa ganzi na kulala kabisa. Nikasema sitaki negativity, nitatafuta ukweli taratibu.

Nimejaribu ku google experiences za watu, sijaona yeyote aliyeandika ku experience nilicho experience. Apparently wote walilala tu na hawana kumbukumbu yeyote.

Nikawaza labda nilikuwa naota nikawa nakumbuka ndoto. Lakini ndoto ni tofauti, ukiamka unajua kabisa ulikuwa unaota. Nomatter how real the dream felt you'll still know that it was just a dream!

What I experienced was different! I was somewhere else! Very aware! The real me was there, not an imaginary me! Na kwanza sijawahi kuota chochote Cha namna ile. Nikawa nawaza kabisa nikiwa kule Is this real life? Yani hata ile wakati naanza kuzinduka na kurudi kulala, ilikuwa ni kama I'm jumping into this world then jumping right back into the other. And I was very aware of both. Like yes niko hapa nimelala nafanyiwa surgery, lakini huku kwingine ni wapi!! Mbona mauzauza!

Tangu nimeamka all I could think of was that experience. Where was I?? Nikawa na shauku kweli nije nimwambie daktari, sema alinitoa confidence maana nilimuanzia mbali, nilimwambia Kuna scenario fulani ikitokea kwenye theater akakataa haikutokea wakati yeye mwenyewe hakuwepo wakati inatokea.

Nikaona nikimwambia na hayo mengine ataniabia nilikuwa naota, and sitaki kabisa mtu adismiss nilicho experience kirejareja...

Yani mpaka nikawa na hamu nifanyiwe surgery nyingine niwekewe ile anaesthesia nione kama nitarudi kule. Nikawaza au ile ganzi ilinilevya kama madawa ya kulevya? Labda wanaovuta madawa ndo huwa Wana experience nilicho experience!! Manake niliwahi kusikia wanaovuta wanakuwa wanaona mauzauza.

Sema huwa sipati muda kukaa mwenyewe most of the times, lakini siku nilikaa kimya peke yangu nikawa nimekodolea macho mmea fulani and honestly zile pattern za majani ni kama pattern za kule nilikokuwa, the awkward patterns and the motions were coming back to me.

Coz where I was was just a world of awkward patterns and very very fast motions and awkward distant shadowy figures and awkward sounds (I could describe the sounds as the sounds you hear ukiwa ndani ya maji). Jumlisha na feeling of helplessness like I want to move but I can't, but I'm just sliding!!!

Inshort, nimeanza kuamini there's more to the human consciousness than just "ukifa haupo tena!" Manake kama wanategemea ukiwekewa ganzi uwe "umekufa Kwa muda", me nilikuwa sijafa bwana I was very aware.

* Bila kusahau surgery yenyewe ilimchukua kama lisaa hivi, lakini ile nimedumbukia kwenye ulimwengu huo Hadi nimeanza kuzinduka ilikuwa kama sekunde chache tu!! Like 30 seconds!!

Someone tag a doctor for me.
 
Hiyo ndiyo inaonyesha kuwa uwezo kwa mwanadamu una limit. Ila tena jiulize Yes tumekubali kuna limit. Na ndiyo maisha ya mwanadamu ya mwisho na mwisho ni kufa. Mtu akifa ndo kafa baada ya hapo ni decomposition.
Kaka neno Mungu ni nadharia pana sana unajua watu wengi wanaamini Mungu kama mtu flani hivi mwenye macho n.k as(as the bible refers) lakini si lazima Mungu awe mfano wa binadamu ila yaweza kuwa Mungu ni jambo jingine kabisa. Wapo wanaoamini Mungu ni Sub Atomic particles etc etc.
Turejee kwenye mada, ushahidi si lazima uwe wa physical bali hata nathari na athari ya mazingira unaweza kuwa ushahidi tosha. Kukosekana kwa ushahidi physical haifanyi kuwa jambo flani ati kuwa ni batili au halipo. Katika kutathmini hii dhana ya maisha baada ya kifo inaweza kujadiliwa katika misingi mikuu miwili Ili kubashiri maisha baada ya kifo yaani probability. Misingi hii ni uwepo wa maisha kabla ya kiumbe kutokea (hapa tutamzungumzia zaidi binadamu), na maisha baada ya kiumbe kutokea.
Unajua kabla ya kuwepo kwa binadamu zipo processes flani zilitokea na kusababisha uwepo wa hii Dunia ambayo ni favourable kwa kutokea kwa uhai (refer to the Big Bang theory).
Jambo hili la kuzuka kwa Dunia mpya si jambo la muhali wala ukiwa yani kwamba limetokea tu kwa bahati mbaya bali ni hatua kadha wa kadha zimefanyika ili kuyaumba maisha. Dunia ndio sehemu rasmi iliyochaguliwa kwa viumbe kuishi na wala sio Mars wala Jupiter (japo elimu yetu inaweza kutufanya tukaishi huko)
Hii ni ishara ya mwanzo kabisa. Msingi wa pili ni ule wa nadharia ya Darwin aka Darwinism theory ya kuwa binadamu hajatokea from nowhere rather ni stages mbalimbali ambazo viumbe vimezipitia mpaka kuwepo kwa hivi viumbe vya leo.
Natamani kuandika kwa urefu zaidi ila nimalizie tu kwa Conclusion ya kuwa hizi ni nadharia na kama ni hivyo suala la kuwepo au kutokuwepo kwa maisha baada ya kifo ni bahati nasibu. Sote twaweza kuwa sahihi na ndio maana tukaita Imani. Yani kuipa uhakika na uyakini wa jambo flani lipo hata kama hulioni kwa macho. Tunaweza kubishana sana na kupingana ila niamini kila mtu yupo sahihi, ila nikushauri tu mkuu usikubali kuamini au kukataa jambo ati kwa kuwa hulioni au hujalithibitisha kwa macho. Yapo mambo flani flani ambayo tunakubali kuwa yapo bila ya ushahidi wowote ule wa kisayansi kwa kuwa Bado Bado elimu yetu haijafanikiwa kuyajadili au kuyatolea hoja.
 
Hiyo ndiyo inaonyesha kuwa uwezo kwa mwanadamu una limit. Ila tena jiulize Yes tumekubali kuna limit. Na ndiyo maisha ya mwanadamu ya mwisho na mwisho ni kufa. Mtu akifa ndo kafa baada ya hapo ni decomposition.
Nakubaliana na wewe kwamba mwanadamu ana ukomo (limit) wake wa kufahamu mambo fulani. Hata hivyo, ukomo wetu usihalalishe kuwa hakuna maisha baada ya kifo.

Mimi naamini kuna maisha baada ya kifo kwa sabababu hatujashudia yakioza (decompose) kabirini kama uozavyo mwili wa mfu.

Kumbuka; mtu akifa tunasema amepoteza maisha yake. Maisha yake yamepotea, yameutoroka mwili wa marehemu.
Kitu kinapotea haimabishi hakiwezi kupatikana sehemu nyingine.
 
Mwili unaoza bwana. Kwanza maiti ikikaa muda mrefu bila treatement inaoza na kunuka mpaka funza wanatoka. Watu waliozikwa makaburi yakifukiliwa itakutwa mifupa tu na baadae mifupa huoza na kujimix kwenye udongo.
 
Maisha baada ya kifo yapona yataendelea kuwepo. Ndiyo, ukifa utazaliwa chura au nyoka au kiumbe chochote na hata mmea. Napo utakufa na kuzaliwa kiumbe mingine tena ndio maana wakasema maisha ni mzunguko!
 
Maisha baada ya kifo yapona yataendelea kuwepo. Ndiyo, ukifa utazaliwa chura au nyoka au kiumbe chochote na hata mmea. Napo utakufa na kuzaliwa kiumbe mingine tena ndio maana wakasema maisha ni mzunguko!
[emoji848][emoji848]
 
Mkuu komenti yako nimei-secreenshoot, ili nijikumbushe pale ninaposahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwili unaoza bwana. Kwanza maiti ikikaa muda mrefu bila treatement inaoza na kunuka mpaka funza wanatoka. Watu waliozikwa makaburi yakifukiliwa itakutwa mifupa tu na baadae mifupa huoza na kujimix kwenye udongo.
Hujanielewa. Sijaandika kwamba mwili hauozi, la hasha.

Nimeandika kuwa mwili uliopoteza maisha ndiyo huzikwa na huoza kaburini. Maisha yaliyopotea hayazikwi kaburini. Yamkini yapo mahali fulani pasipojulikana.

Maisha na mwili ni vitu viwili tofauti. Maisha yakitoweka, mwili huoza. Maisha hupokewa kabla ya mwili kuoza.

Kwa hiyo maisha yapo baada ya kifo.
 
[emoji848][emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…