Hivi ni kweli kuna maisha baada ya kifo?

Hivi ni kweli kuna maisha baada ya kifo?

Ulosa sahihi kabisa mimi huwa nahitimisha kwa kusema hivi Watu huwa hawafikirii na hii imetokana na kujazwa ujinga wa Sayansi yaani mtu anakuja kabisa anasema ukifa umekufa,yaani hata akili tu ya kawaida inakataa,yaani niishi nife halafu iwe basi tu ? Akili inakataa kabisa.
kwa nini akili ikatae kwa mfano kama ndiyo uhalisia itakuwaje hapo
 
una udhibitisho wa hili
Kwa mambo aliyonitendea/aliyotenda Mungu naamini yupo.Kuhusu kuthibitisha hili inategemea Imani yako ipo wapi ?Unaamini Mungu alikuumba na pia aliuumba ulimwengu au unaamini duniani ilikuwepo tu hamna aliyeiumba na pia binadamu alikuwepo tu
 
Akili iliyo salama haijawahi kupingana na uhalisia,ukiona hivyo huo si uhalisia.
Kuna wakati akili hukataa uhalisia wewe haijawahi kukutokea mfano unatangaziwa kifo lakini unakataa kabisa na akili haikubali uhalisia na ukweli wa tukio hilo
 
kuna wakati binadamu inatubidi tukubaliane na hali ilivyo kwa sababu ya HOFU
 
Najaribu kuwaza according to bible

Baada ya ufufuo yesu atarud duniani na kuitawala dunia kama mfalme(wakati huo shetan atakua amefungwa)

Baadae shetani ataachiliwa huru na atadanganya wengi sana.

Kwa nadharia kama za mtoa mada sasa ndio naamini shetan ataweza kudanganya wengi sana baada ya ufufuo
Sasa kwanini mungu atuletee shetani ili atudanganye halafu tukishadanganyika mungu ambaye kamleta huyo shetani akatuchome sisi moto, kwa mfano wewe unamkataza binti yako mwanafunzi asiwe na mchumba na unamuonya kwamba akiwa na mchumba utamuadhibu kisha wewe mwenyewe baadae unamtafuta mwanaume unamwambia aende akamtongoze huyo binti halafu baadae ukija ukimuona binti yako na huyo mwanaume ni wachumba unamuadhibu binti yako , ni kwann haya mambo yamekaa hivi kiupandeupande?
 
na jee hiki tunachoamini leo ndicho walichokuwa wana amini wazee wetu mababu zetu asili yetu kabla ya kuja wakoloni barani Africa??
 
Sasa kwanini mungu atuletee shetani ili atudanganye halafu tukishadanganyika mungu ambaye kamleta huyo shetani akatuchome sisi moto, kwa mfano wewe unamkataza binti yako mwanafunzi asiwe na mchumba na unamuonya kwamba akiwa na mchumba utamuadhibu kisha wewe mwenyewe baadae unamtafuta mwanaume unamwambia aende akamtongoze huyo binti halafu baadae ukija ukimuona binti yako na huyo mwanaume ni wachumba unamuadhibu binti yako , ni kwann haya mambo yamekaa hivi kiupandeupande?

Sasa kwanini mungu atuletee shetani ili atudanganye halafu tukishadanganyika mungu ambaye kamleta huyo shetani akatuchome sisi moto, kwa mfano wewe unamkataza binti yako mwanafunzi asiwe na mchumba na unamuonya kwamba akiwa na mchumba utamuadhibu kisha wewe mwenyewe baadae unamtafuta mwanaume unamwambia aende akamtongoze huyo binti halafu baadae ukija ukimuona binti yako na huyo mwanaume ni wachumba unamuadhibu binti yako , ni kwann haya mambo yamekaa hivi kiupandeupande?
Nyakati za mwisho maarifa yataongezeka sana (wewe ni zao la kuongezeka kwa maarifa)

Mm naamini hakuna kitu ambacho kimejileta chenyewe hapa duniani, lazima kuna nguvu somewhere imefanya mm na ww kuwepo hapo tulipo

Nguvu hyo yawezekana ikawa kubwa sana zaidi ya tunavyofikiria au inaweza ikawa tumeipa nguvu isizostahili.

Hiyo nguvu iliyotuweka hapa duniani naweza kusema ndio mungu.

Jibu lako lipo hapo tunapofikiria kwamba ni mkubwa au hana nguvu sana.
 
Umejuaje hili ?

Lakini ukiangalia na kutafakari kauli yako haingii akilini. Yaani tuishi tu duniani kisha tukifa iwe basi ? Sasa nini lengo la sisi kuishi duniani ?
Lengo ni kuja kupambana na mazingira
 
Kuna wakati akili hukataa uhalisia wewe haijawahi kukutokea mfano unatangaziwa kifo lakini unakataa kabisa na akili haikubali uhalisia na ukweli wa tukio hilo
Hiyo siyo akili,hivi unaijua akili ilivyo ?

Hivi unajua ya kabisa kila mwanadamu ameumbwa na silika ya kuweza au kujua ya kuwa Mola yupo au ulimwengu umeumbwa ? Sasa ndivyo ilivyo na akili,kwamba haipingani na uhalisia zaidi ya kuukataa kwa makusudi basi hakuna kinyume chake.
 
Lengo ni kuja kupambana na mazingira
Umejuaje kama lengo ni hilo na mwisho wa siku iweje ? Yaani ukishapambana na mazingira ?

Naomba unitajie sifa za mshindani au ili shindano liitwe shindano washindani wanatakiwa wawe na vigezo gani vya msingi ?
 
Jibu kwanza maswali niliyo kuuliza usikimbie maswali.
Umeona sasa tatizo lako lilipo?

Nilichokijibu kwenye hoja ya mdau kimetokana na madai yake mwenyewe kua amri kumi "zimejitosheleza", sasa wewe kuniuliza uhalali wa jambo halafu ukaacha msingi wa hoja unakua unanifanya nitilie mashaka uelewa wako
 
Ulosa sahihi kabisa mimi huwa nahitimisha kwa kusema hivi Watu huwa hawafikirii na hii imetokana na kujazwa ujinga wa Sayansi yaani mtu anakuja kabisa anasema ukifa umekufa,yaani hata akili tu ya kawaida inakataa,yaani niishi nife halafu iwe basi tu ? Akili inakataa kabisa.
Kwahiyo kwasababu akili yako ya kwaida inakataa ndio unajiridhisha kwa kusema watu wengine hawafikirii vizuri?
Wewe kama nani?
 
Huku kufufuliwa sasa walienzi tunaenzi na tunaendelea kuenzi mwisho wa kuenzi ni lini hasa
Kuna wenzio huko nyumanao walihoji kama wewe hv na walijibiwa hivi:

Soma hapa

QURAN 17:49-52

"Na walisema: Je! Tutapo kuwa mifupa na mapande yaliyo vurugika, (Kaburini) ndio tutafufuliwa kwa umbo jipya? Sema: Kuweni hata mawe na chuma. Au umbo lolote mnalo liona kubwa katika vifua vyenu. Watasema: Nani atakaye turudisha tena? Sema: Yule yule aliye kuumbeni mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: Huwenda yakawa karibu! Siku atakapo kuiteni, na nyinyi mkamuitikia kwa kumshukuru, na mkadhani kuwa hamkukaa ila muda mdogo tu.'
 
Back
Top Bottom