Uchaguzi 2020 Hivi ni kweli kuwa CCM inakubalika kama ambavyo watawala wetu wanavyotuaminisha?

Upo serious Ndugu? Vijijini wanaishi watu wasio na elimu?Nani kawakosesha elimu?Mnapenda kutukana Wananchi wa vijijini huku mkiwasifia watawapa kura za kishindo?Mnautumia uelewa wao mdogo kwa faida yenu na mnahakikisha hawaambiwi ukweli na yeyote?Mnapanga kuiba kura zao kwa kuwa hawafahamu haki zao kwa njia ile ile mliyoitumia katika uchaguzi wa serikali za mitaa?
Mnawadhalilisha Watanzania wenzenu katika nchi yao huku ninyi mkiishi kama wafalme kwa kodi zao,viyoyozi full ac ofisini na kwenye magari,mishahara yenu na posho nono,halafu mnawadhihaki waajiri wenu?
Inaumiza akili,mwili na roho za wengi,only CCM's are enjoying endlessly.
 
Hoja dhaifu Sana hizi labda kama hujamaanisha. Ikiwa umemaanisha inamana hujui makandokando yaliopo ktk hoja zako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukifikiria matatizo yaliyoetwa na ccm utagundua ni mengi kuliko mazuri...mm sion kukubalika kwa ccm
 
Hii fasihi yataka akili kubwa kuelewa.
 
TWAWEZA walishatoa majibu ya utafiti wao kuwa fisiemu inapendwa na watu wa namna gani, utafiti uwa unapingwa kwa utafiti fisiemu hawajafanya utafiti wao wanajiaminisha kwa uchaguzi wa serikali za mitaa uliogubikwa na hila mbalimbali yani mgombea wa upinzani akienda kwa mtendaji kuomba fomu anapewa fomu nusu ila akija wa fisiemu anapewa fomu zote na ata wakikosea kujaza fomu walikuwa wanafutiwa na kurekebishiwa kwenye makosa, wagombea waupinzani wananyimwa fomu arafu usema kuwa uchagu huo ulikuwa uhuru na haki
 
Uzuri wangu sio mwanachama wa chama chochote maana naona wote wanachumia tumbo, kumbuka Wema, Lowasa, Sumaye na wengine walipohamia upinzani, wapinzani wakafurahia na kuanza kuwa-amplify kana kwamba ni watu sahihi chamani.

Mtu unajiuliza hivi hakuna watu wanaofaa humo upinzani! Yaani wako na mambo ya u-CCM, yaani mtu wa upinzani akihamia CCM kila chombo cha habari ndio habari.

Ki ukweli upinzani wa dhati Tanzania bado sana maana hakuna mwenye msimamo ndani ya chama chake bali ni wachache sana sana kuwapata.

Huwa naangalia watu wanajinadi ooh tuko na rais anayejali watu wanyonge halafu huyo anayepigiwa debe akisimama anawatusi pasi kujali hali na shida za watusiwa.

Pia ndugu, kwa sasa though haiapply elimu wanasema ni bure, zamani walikuwa wanachangia 20,000 + michango ya maji, chaki, mlinzi na mengine kama yapo.

Siwezi tukana wa wanakijiji maana nami ni mwanakijiji nayaona yanayoendelea kijijini kwetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aaaaaaa wapi.
 
Hakika, twawea walishamalia kazi, katika utafiti wao, kwa kukuibia ibia kidogo walichosema ni hiki;

Kuwa CCM inakubalika zaidi vijijini, tena kwenye kada za watu ambao hawajaenda shule.....

Vipengele vingine waliivyoelezea twawwza malizia mwenyewe........
 
Account yako imekuwa Hacked? ..au umepatwa na mafua ya Corona? But if you are talking Ironically, basi nimekuelewa Mayala!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa upande wa Rais uungwaji mkono umeserereka kutoka 96% mwaka 2016, ambavyo vilikuwa ni viwango vya juu kuwahi kutokea nchini, mpaka 55% mwaka 2018, viwango vya chini kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya nchi
 
Nabarikiwa sana na aina ya uandishi wako, ingawa ili kukuelewa huwa nayaelekezea maandishi kwenye kioo ndio niyasome, yaani kama selfie vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa upande wa Rais uungwaji mkono umeserereka kutoka 96% mwaka 2016, ambavyo vilikuwa ni viwango vya juu kuwahi kutokea nchini, mpaka 55% mwaka 2018, viwango vya chini kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya nchi
Hiyo ni kwa mujibu wa Rais au Twaweza?

Ninejaribu kukuuliza tu Mkuu The coolest jw ili nipate kujua..........

Kwa vile nakuwa kama nimechanganyikiwa vile, kusikia kwa mujibu wa Rais aeleze kishuka kwake kuaminiwa na watanzania, utakuwa ni ajabu na kweli!
 
Kwa upande wa Rais uungwaji mkono umeserereka kutoka 96% mwaka 2016, ambavyo vilikuwa ni viwango vya juu kuwahi kutokea nchini, mpaka 55% mwaka 2018, viwango vya chini kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya nchi
Huo ndiyo ukweli mtupu, ambao wale watu wa Lumumba hawataki kabisa kuusikia........

Ndiyo sababu kubwa inayowafanya tegemeo lao kubwa kwa ushindi wa aina yoyote hapa nchin ubaki kwa Jeshi la Polisi nchini
 
Lakini wewe mzee hizi teuzi kweli? Ila nakutabiria 2020/2025 lazima Ukuu wa mkoa au Ubunge wa Kuteuliwa kazi yako tumeiona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bi Mkubwa aliniambia nimpeleke kuhakiki taarifa zake kwenye daftari la wapiga kura,
Hali niliyojionea ni makundi makubwa ya vijana walihamasika kuja kujiandikisha,Mazungumzo yao yalikuwa waziwazi wengi wakiulizana ushapata " Kichinjio", hakika inaonekana wazi kabisa jinsi watu walivyoichoka CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…