Uchaguzi 2020 Hivi ni kweli kuwa CCM inakubalika kama ambavyo watawala wetu wanavyotuaminisha?

Kama ni wembe ule ule wa kufunga ofisi ni kweli mtashinda kwa hizo asilimia
 
CCM wana matumizi mabaya sana ya fedha za wananchi, leo Katibu Mkuu wao yupo Mtwara basi imekuwa neema kwa madereva bodaboda wamekula posho kila mmoja elfu 10 kwenda kumpokea Airport.

Na kulikuwa na bodaboda zaidi ya 200 hivi ambao wamekula hela ingawa wengine hawakutokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM inakubalika sana vijijini na kwenye vitongoji ambapo asilimia kubwa ya umma wa watanzania wenye elimu ya msingi na kati wako kwa wingi na wanashiriki kupiga kura. Kwa upande mwingine vyama mbadala vinakubalika mijini tena kwa msimu na watu wa tabaka la kati ambao ni waongeaji wazuri na elimu nzuri na ya wastani lakini wengi wao hawaoni maana ya kushiriki kupiga kura pamoja na kujua umuhimu wake.

Kwa tabia hizo mbili kinzani ambazo haziwezi kubadilika ndani ya miezi minane ijayo ni turufu kwa CCM kushinda uchaguzi ujao labda swali likiwa ni kwa asilimia ngapi.
 
Nafikiri itolewe haki ya kufanya mikutano kwa vyama vyote isiwe ccm ndiyo wanazunguka nchi nzima na wengine wakitaka kufanya mikutano wanaambiwa kuna taalifa za kiintelejensia,Na leo hii mnaiona ccm inakubalika kwa sababu wapinzani wake wamefungwa mikono nawashangaa mnaosema na kujidai kuwa ccm inakubalika wakati siyo kabisa!!
 
Bora wapate kabisa kipande cha boss'but is it cost benefit consious'
 
Siku hizi ninakuwa mno "Lethargic" kusoma articles zako humu kwani naona kama ziko very sarcastical, sycophantic, ambiguous or even hypocritical.
 
mtuambie akina Azory na Saanane wako wapi au kuwadhulumu uhai pia ni maendeleo kwenu.
 
Kumbe wewe Mayala ni hopelesd sana
 
Wajinga wanyonge kwa wingi wao ndio uamua nani awe kiongozi
 
Kumbe wewe Mayala ni hopelesd sana
Wewe unataka akale wapi yeye na watoto wake???Mtukufu Rais alilijua mapema sana ndipo akasema Jina MAYALA kwa kisukuma maana yake Njaa!!!!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…