Hivi ni kweli kuwa kila Mwana JamiiForums ana degree?

inategemea na degree ya nini na kutoka chuo gani aisee. maana kuna vingine vya mtaani, na kuna degree mpaka za puchi.
 
Minaona hiyo inatokana na kejeri kama wewe ukisema ni form 6 ,diploma au form4. wenye elimu zao humu wengine wanakejeri na kuwazarau wanaosoma chuo au ambao hawajafika chuo
 
Yani, haiitaji mtu kudeclare kiwango chake cha elimu, mawazo yake tu utajua huyu mtu kabukua kiasi gani...
 
si kweli kuwa wote tuna degree.Mimi nimeishia darasa la saba.

Watu wengine wana masters degree hivyo jaribu kuomba ushauri kwao pia kuna wenye phd....sasa amua wewe kuomba ushauri kwa nani
 
Elimu ya darasani na namna inavyombadilisha mhusika hi vitu viwili tofauti. Ni kweli kuwa elimu husaidia kwa asilimia kubwa sana kumfanya mtu awe na mabadiliko chanya na hasi kwa uchache.
Hoja ambayo sana inatawala ni mtu kuwa na elimu halafu anakuwa sawa na asiye na elimu kama hiyo ktk MAWAZO, MATENDO, MAFANIKIO, BUSARA, UPEMBUZI, UJUZI n.k na hata kufikia sisi kusema AMESOMA ILA ELIMU YAKE HAIJAMSAIDIA.
MFANO:
1. kijana aliyemaliza chuo kikuu kuandika C.V ama barua ya kuomha ajira ni kazi
2. Form six ama hata chuo kikuu kuongea lugha ya kikoloni kwa tabu (zama za wazee wetu lugha ilikuwa kigezo na sense of pride)
3. Kijana wa chuo kikuu atokaye familia maskini na apataye mkopo, huyu hasaidii nyumbani kwao ni kuishia Club, wanawake, mashugadadi, pombe na kununua vifaa vya ki elekroniki vya gharama ( smartphones, flat screens, sub woofers etc) wakati wazee wetu enzi wanasoma ilikuwa kukumbuka nyumbani ni first priority
4. Kijana aliyemaliza degree yake (uchumi, sheria, umakanika, umeme, udaktari,) pale apatapo kazi hajui chochote ktk kazi husika ama anajua kwa sehem ndogo sana ukilinganisha na walio chini yake kielimu, anaanza kuelekezwa na CERTIFICATE HOLDER ama DIPLOMA HOLDER..... ilhali huyu alokuja ana elimu kuwazidi waliopo.

Hiyo ni baadhi ya mifano inayoleta kubezwa kwa wenzetu WASOMI
 
Humu kuna wasio hata na astashahada yoyote ila wana busara, hekima na maarifa, pia kuna wenye astashahada, stashahada, shahada ya kwanza, shahada ya uzamili, shahada ya uzamivu lakini hawana hekima, busara wala maarifa. Lakini kinyume chake pia ni sahihi.
 
Elimu ya darasani na namna inavyombadilisha mhusika hi vitu viwili tofauti. Ni kweli kuwa elimu husaidia kwa asilimia kubwa sana kumfanya mtu awe na mabadiliko chanya na hasi kwa uchache.
Hoja ambayo sana inatawala ni mtu kuwa na elimu halafu anakuwa sawa na asiye na elimu kama hiyo ktk MAWAZO, MATENDO, MAFANIKIO, BUSARA, UPEMBUZI, UJUZI n.k na hata kufikia sisi kusema AMESOMA ILA ELIMU YAKE HAIJAMSAIDIA.
MFANO:
1. kijana aliyemaliza chuo kikuu kuandika C.V ama barua ya kuomha ajira ni kazi
2. Form six ama hata chuo kikuu kuongea lugha ya kikoloni kwa tabu (zama za wazee wetu lugha ilikuwa kigezo na sense of pride)
3. Kijana wa chuo kikuu atokaye familia maskini na apataye mkopo, huyu hasaidii nyumbani kwao ni kuishia Club, wanawake, mashugadadi, pombe na kununua vifaa vya ki elekroniki vya gharama ( smartphones, flat screens, sub woofers etc) wakati wazee wetu enzi wanasoma ilikuwa kukumbuka nyumbani ni first priority
4. Kijana aliyemaliza degree yake (uchumi, sheria, umakanika, umeme, udaktari,) pale apatapo kazi hajui chochote ktk kazi husika ama anajua kwa sehem ndogo sana ukilinganisha na walio chini yake kielimu, anaanza kuelekezwa na CERTIFICATE HOLDER ama DIPLOMA HOLDER..... ilhali huyu alokuja ana elimu kuwazidi waliopo.

Hiyo ni baadhi ya mifano inayoleta kubezwa kwa wenzetu WASOMI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…