Hivi ni kweli kuwa kila Mwana JamiiForums ana degree?

Hivi ni kweli kuwa kila Mwana JamiiForums ana degree?

nasikia Mpigamsuli laana ya jf imemuandama hadi elimu ya.huko muccobs haiendi poa ni mtu wa.kuchomoa sup na kukwepa kidisco

Teeh, ailikua anadance na akili za watu jf mwisho wa siku wamemgeuza.... I wish to see him back with....! Hivi jamaa kamaliza chuo au kamba ilikatikia palipoozea?
 
Last edited by a moderator:
mbona mimi nilishajitambulisha kitambo tuu...nimeishia darasa la tano pale shule ya msingi madenge
 
Usisahau
Dr. Mengi.
Dr. Mrema.
Dr. Geo Davie Mkuu wa Manabii.
Dr. Manyaunyau.
Dr. Presdent.
Dr. Mama mchungaji Rwa....
Dr. Nape Nauye.
Dr. Ndodi.
Dr. Mchunguzi Huru [phd]
Dr....

Nilipata kusikia namba 7 alitumia kofia yake kutaka kupakua alama (marks) kutoka kwa Lecturer mmoja alipokuwa anachukua Masters somewhere akazinguliwa, kumbe kapekecha mpaka kuingia kwenye u-Dr
 
Shalom wakuu!
Swali hili limekuwa likinitatiza sana tangu miaka 2 iliyopita tangu nilipojiunga na JF,

Imekuwa ni kama fashion kwa wanaJF wengi kudeclare elimu zao katika post zao nyingi, ajabu kila mtu anasema sijui alipokuwa chuo mwaka wa pili, mwingine ooh nimejiajiri lakini nina degree yangu, hivi ni kweli wote tumesoma mpaka level hizo?

Hakuna hata mwenye diploma au Form4 kabisa?

Mbaya zaidi hadi vijana wa BRN wa humu JF naona wameanza taratibu kurithi haka karoho ka kipepo kanakotokana na kutojikubali.

Tubadilike jamani.

Shardcole, humu ndani kuna watu wenye elimu tofauti tofauti. Kuna waalimu wenye diploma, waalimu wale wa zamani Upe, Kuna maproffessor, kuna wakulima, Kuna bodaboda, kuna wasukuma toroli, kuna polisi, mawaziri, madaktari, fundi ujenzi, wafanyabiashara, wabunge, housegirls, wanafunzi (primary, secondary, forms 5/6, chuo kikuu) , kuna mahakimu, majaji n.k. Kwa hiyo watu ni wa kila aina wako humu vile vile kama unavyoona facebook, WhatsApp, Viber, twitter, instagram n.k. Kuna kuna wanvyuo kama chuo kikuu, chuo cha ufundi kama seremala, welding, driving n.k. Wenye degree zao nao wapo wakiwa na degree mbalimbali. Kwa hiyo hapa tuko mchanganyiko.
 
Last edited by a moderator:
mbona mm sijui kusoma na kuandika lakini nipo hapa
 
Teeh, ailikua anadance na akili za watu jf mwisho wa siku wamemgeuza.... I wish to see him back with....! Hivi jamaa kamaliza chuo au kamba ilikatikia palipoozea?
hahahaaa...haya bana..lakin mshaambiwa thermomter ina degree lkn inafanya kaz kwapani!
 
Ndugu yangu yaani ya humu ndani ukiyafuatilia, utachoka. Yaani;
-Hakuna mwenye vitz, wote wana v8
-Humu JF wote wanapiga bao 5 na kuendelea, sasa haya mabango ya kuongeza nguvu za kiume ni ya akina nani? Labda wana JF hawahusiki!
-Humu wote wapo dsm, wa Mkiu hayumo humu.
-Humu Jf kila mtu amewahi kupanda ndege au amepanda ndege muda huu.
-Mwenye KIBAMIA humu hayumo, humu kila mtu ana Tangopori tu. Chezea JF weyee!
-Humu watu tunajua kila kitu, mpaka dawa ya ebola imo humu.

-halafu kinginee, hakuna mla mihogo hata mmoja humu wakati kila siku tunapanga foleni kwa mama Cha Upepo.
JF iache kama ilivyo.

Mkuu CM ukifuatilia majibu mengi yaliyotolewa kwenye uzi huu unaweza kujua elimu na IQ zao wala huhitaji kuviona vyeti vyao
 
Last edited by a moderator:
Shardcole, humu ndani kuna watu wenye elimu tofauti tofauti. Kuna waalimu wenye diploma, waalimu wale wa zamani Upe, Kuna maproffessor, kuna wakulima, Kuna bodaboda, kuna wasukuma toroli, kuna polisi, mawaziri, madaktari, fundi ujenzi, wafanyabiashara, wabunge, housegirls, wanafunzi (primary, secondary, forms 5/6, chuo kikuu) , kuna mahakimu, majaji n.k. Kwa hiyo watu ni wa kila aina wako humu vile vile kama unavyoona facebook, WhatsApp, Viber, twitter, instagram n.k. Kuna kuna wanvyuo kama chuo kikuu, chuo cha ufundi kama seremala, welding, driving n.k. Wenye degree zao nao wapo wakiwa na degree mbalimbali. Kwa hiyo hapa tuko mchanganyiko.

Mbona umetusahau makorokoroni? Mimi sifichagi ujuzi wangu mimi ni korokoroni na nina cheti changu cha mgambo nilichofaulu vizuri tuu hizo degree zenu ni mbwembwe tu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom