Sijui nitumie lugha gani rahisi ili tuelewane maana hapa ni pure pharmacology. Lakini ina nut shell si kwamba kila dawa ukinywa na pombe utakuwa ila kwa hizo nitro imidazole kama metronidazole, tinidazole secnidazole na nyingine it's obvious utapata disulfiram like effect ambayo ni worse ni inaweza kuwa life threatening.
Kwa kifupi dawa ukinywa huwa zina hatua nne kwenye mwili wa mwandamu ambapo ni 1. Absorption (unyonywaji)
2. Distribution (usambazaji)
3. Metabolism(kuichakata dawa )
4. Excretion( utolewaji)
Kuna enzymes ambazo huwa zipo kwenye ini zinahusika kufanya kazi ya metabolism ili kiasi fulani cha dawa kitu mike mwilini na Mabaki ya toke kwa njia ya jasho, mkojo, haja kubwa n.k
Moja ya enzymes hizo kuna kitu kunaitwa Cytochrome P 450 ambayo hutumika kwenye metabolism ya dawa nyingi pamoja na chakula. Na kwa kuwa enzyme huwa zinafanya kazi katika mfumo wa kama kufuri na funguo mara nyingi unakuta kuna kuwa na competition kati ya enzymes na substrate.
Hapa substrates kwetu n dawa husika pamoja na pombe. Zote zinakuwa zinataka kutumia hiyo CYP P450 ili kuwa metabolised. Sasa kunachotokea mara nyingi pombe inakuwa mshindi na kuacha dawa bila kuwa metabolised hivyo kufanya kuwa toxic mwilini .Hivyo basi toxicity inasabishwa na hiyo bio - accumulation. Nimejaribu tu kugusa gusa maana kwa undani wake ni somo refu.
Lakini kwa kifupi ni kwamba USIUMIE POMBE wakati umekunywa dawa. Sio lazima ufe ila unaweza ku impair metabolism ya sawa. Ahsante sijui kama kidogo nimeeleweka
kuna kitabu kinaitwa ifahamu pombe sema nimekwama kwenye distribution . hizi baadhi ya dawa zenye muingiliano na pombe.
[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD] NO[/TD]
[TD="width: 204"] JINA/ KUNDI LA DAWA[/TD]
[TD="width: 144"] MATUMIZI[/TD]
[TD="width: 223"] MADHARA IKITUMIKA NA POMBE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 44"]
1.[/TD]
[TD="width: 204"]
Isoniazid[/TD]
[TD="width: 144"] dawa hii hutumika kutibu kifua kikuu. Mara nyingi hupatikana kwenye mchanganyiko wa dawa nne uuitwao RHZE.[/TD]
[TD="width: 223"] Dawa hii inaongeza uwezekano wa kupata matatizo ya ini. Pia ikitumika na divai kuna uwezekano wa kupanda kwa shinikizo la damu (BP)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 44"]
2.[/TD]
[TD="width: 204"]
Metronidazole/fragyl[/TD]
[TD="width: 144"] dawa hii mara nyingi hutumika kutibu matatizo ya tumbo.[/TD]
[TD="width: 223"] Kuharisha,kichefuchefu, kutapika, maumivu makali ya kichwa, kizunguzungu[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD] 3.[/TD]
[TD="width: 204"]
asprin[/TD]
[TD="width: 144"] Dawa ya maumivu na kushusha homa[/TD]
[TD="width: 223"] Inaongeza uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 44"] 4.[/TD]
[TD="width: 204"]
Chlorpropramide tolbutamide tolazamide[/TD]
[TD="width: 144"] Dawa za kisukari[/TD]
[TD="width: 223"] Kuharisha,kichefuchefu, kutapika, maumivu makali ya kichwa, kizunguzungu[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 44"] 5.[/TD]
[TD="width: 204"]
metoclopramide[/TD]
[TD="width: 144"] Dawa ya kichaa na kuzuia kutapika[/TD]
[TD="width: 223"] Inasababisha kulewa zaidi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 44"] 6.[/TD]
[TD="width: 204"]
ketaconazole[/TD]
[TD="width: 144"] Dawa ya kutibu fangasi[/TD]
[TD="width: 223"] Kubabuka ngozi,kutapika na kizunguzungu[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 44"] 7.[/TD]
[TD="width: 204"]
Cimetidine ranitidine nizatidine[/TD]
[TD="width: 144"] Dawa za vidonda vya tumbo[/TD]
[TD="width: 223"] Ranitidine na nizatidine Zinaongeza kiasi cha pombe kwenye damu, madhara ya cimetidine kwenye ubongo huongezeka.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 44"] 8.[/TD]
[TD="width: 204"]
doxycycline[/TD]
[TD="width: 144"] Dawa ya kutibu maambukizi .
[/TD]
[TD="width: 223"] Unywaji wa pombe kupita kiasi hupunguza nguvu ya dawa hii. Sio lazima unywaji huu uwe pamoja na dawa.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 44"] 9.[/TD]
[TD="width: 204"]
verapamil[/TD]
[TD="width: 144"] Dawa ya kutibu shinikizo kubwa la damu (BP) na maumivu ya moyo.[/TD]
[TD="width: 223"] Dawa hii huongeza kiasi cha pombe kwenye damu na kuzidisha madhara yake. Pia kuna hatari ya madhara kwenye moyo[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD] 11.[/TD]
[TD="width: 204"]
Valium (diazepam)[/TD]
[TD="width: 144"] Dawa ya usingizi na kutuliza[/TD]
[TD="width: 223"] Dawa hii huongeza madhara yasababishwayo na pombe.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 44"] 12.[/TD]
[TD="width: 204"]
Ascorbic acid (vitamin C)[/TD]
[TD="width: 144"] Dawa ya kuongeza vitamin C mwilini[/TD]
[TD="width: 223"] Inaongeza utokaji wa pombe mwilini , kusaidia kuona na kuongeza balansi baada ya kutumia pombe.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Hizo ni baadhi ya dawa tu lakini haishauriwi kwa mtu anayetumia dawa yeyote kutumia pombe. Hata kama hautapata madhara lakini pombe inaweza kusababisha dawa itoke haraka mwilini na hivyo isiue wadudu au kufanya kazi yake ipasavyo. pia kwa kuandika baadhi ya madhara yanaweza kuonekana ni ya kawaida lakini yanaweza kuwa hatari na kuhatarisha uhai wa mtu. Je ni muda gani mtu anatakiwa asubiri kabla ya kunywa pombe?. ukichukulia dawa ya metronidazole (fragyl), tafiti nyingi zinashauri kusubiri saa 24 (siku moja) au zaidi na wengine wanashauri kutumia pombe baada ya saa 72 yaani siku tatu baada ya kutumia dawa hii. Kwa mtu mwenye afya ya kawaida saa 24 zinatosha kabisa lakini kwa wazee au watu wenye magonjwa mengineyo inashauriwa kusubiri zaidi ya saa 24. Ni vizuri pia ukawasiliana na mtaalamu wa dawa kabla haujatumia pombe iwapo utakuwa umetumia dawa. Yeye anaweza kukupangia muda mzuri wa kusubiri kulingana na hali yako.