Hivi ni kweli Mungu hana upendeleo?

Hivi ni kweli Mungu hana upendeleo?

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!
Huwa namtafakari sana Mungu,je ni kweli hana upendeleo kwa wale wanao amini kama kuna Mungu naombeni jibu.

Binafsi naona kama kuna watu wamependelewa sana wao na familia zao zimependelewa naona mpaka uzao wao pia unazidi kupendelewa.

Au kuna Miungu tofauti tofauti kila mtu anaabudu wake??
 
Warumi 2:11 kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.

Matendo ya Mitume 10:34 Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;

Waefeso 6:9 Nanyi, akina bwana, watendeeni wao yayo hayo, mkiacha kuwaogofya, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo.

MUNGU HANA UPENDELEO WALA HATAKUJA KUWA NA UPENDO NENO LAKE NI KWELI NA HAKI

Naongelea Mungu aliyenibadilisha na kabadilisha maisha ya watu wengi walio mtii
 
Sio kama nakufuru

Lakini jibu ni ndio .
Kuna watu toka.kuiona dunia mpka Leo hawajawahi kuona kitu kinachoitwa shida
Majibu haya hutokea kutokana na hisia za maumivu ya shida ambayo mtu anapitia lakini ukweli ni kwamba MUNGU hana upendeleo kabisa ,tupo sawa kwa MUNGU

Ndio maana hakuna mtu aliyebora kuliko mtu mwingine kwa MUNGU bali kila mtu nibora kwenye nafasi yake

Miongoni mwa kauli zinazo UA kuajiamini na kuweza kufanya vitu vikubwa ni kuamini mtu mwingine ni Bora/anapendelewa kuliko wewe
 
Uumbaji wa Mungu ni wa mipango. Mungu anaiangalia dunia kama super structure na kila mmoja amempa nafasi yake. Ukikubali nafasi aliyokupa kama mdau ktk dunia na kuitimiza kwa upendo huta jiuliza kwa nini mwingine ni Raisi, Doctor, pastor, mfanyakazi wa ndani, muosha maiti. etc. Fulfil God purpose by staying in your lane.
 
Naposikia watu wamebakwa, kuteswa, watoto na wa mama wanauliwa vitani. Naposhuhudia kila siku maskini barabarani, ninapoona umaskini uliopo vijijini. Ninapoteza ndugu zangu kisa hospitali hazina madaktari, dawa na vifaa tiba. Kiukweli nahisi kuna upendeleo unaendelea kwenye hii dunia lakini cha ajabu watu wanaamini peponi kutakuwa pazuri. Je una uhakika gani utafika kama hapa dunia tu panakushindwa?
 
Jiulize ni kwanini.dini sisi tumeletewa uku atukuwa na mtume muafrica ndo utapata jibu..kwaiyo babu zetu wenye walikufa dini azijafika na walikula nguruwe.bila kujua ni alamu.watachomwa.moto
Babu zetu watahukumiwa kwa matendo yao maana sheria tayari zilikuwa zimeandikwa katika mioyo yao kabla ya ujio wa dini.
Mfano, walipotaka kufanya matendo mabaya (wizi, uzinzi, uuaji...), walishtakiwa na dhamira zao. Ikiwa waliamua kutenda mabaya hapo hamna excuse!

Umeandika kuwa walikula nguruwe bila kujua na kisha watachomwa moto!
Je umefikiria kwanza ulichoandika hapa?
 
Habari wadau!
Huwa namtafakari sana Mungu,je ni kweli hana upendeleo kwa wale wanao amini kama kuna Mungu naombeni jibu.

Binafsi naona kama kuna watu wamependelewa sana wao na familia zao zimependelewa naona mpaka uzao wao pia unazidi kupendelewa.

Au kuna Miungu tofauti tofauti kila mtu anaabudu wake??
Ikiwa wazazi wamepambana kweli kweli na kuweka mazingira mazuri ya watoto wao, utasemaje kuwa Mungu kawapendelea?
 
Habari wadau!
Huwa namtafakari sana Mungu,je ni kweli hana upendeleo kwa wale wanao amini kama kuna Mungu naombeni jibu.

Binafsi naona kama kuna watu wamependelewa sana wao na familia zao zimependelewa naona mpaka uzao wao pia unazidi kupendelewa.

Au kuna Miungu tofauti tofauti kila mtu anaabudu wake??

Wewe umekosa nini hadi umlalamikie Mungu na unataka akupe kitu gani ili utosheke na kuridhika??!!
 
Muda mwingine shida tunazopitia hufanya kuona kama Mungu ametuacha lakini kama tungepewa macho yakuona matendo ya Mungu atendayo kwetu na hata mabalaa anayotuepusha nayo ,asee yatupasa kumshukuru Mungu kwa kuwa bado yu hai na mzima wa afya tele
 
Je wale wanaopata mabalaa si ni binadamu kama sisi tu? Au unadhani wanastahili matatizo?
 
Back
Top Bottom