Hivi ni kweli Mungu hana upendeleo?

Hivi ni kweli Mungu hana upendeleo?

Habari wadau!
Huwa namtafakari sana Mungu,je ni kweli hana upendeleo kwa wale wanao amini kama kuna Mungu naombeni jibu.

Binafsi naona kama kuna watu wamependelewa sana wao na familia zao zimependelewa naona mpaka uzao wao pia unazidi kupendelewa.

Au kuna Miungu tofauti tofauti kila mtu anaabudu wake??
Jiuluze ni kwa nini KWA ASILIMIA KUBWA WATU MAFUKARA SANA NI WALE WALIOWEKA SANA DINI MBELE.
 
Romans 9:11
[11](kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),

[12] aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo.

[13]Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.

[14]Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!

[15]Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye.

[16]Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.

Tafakari hapa mkuu
 
Ziheshimuni mamlaka kwan mamlaka zote zimetoka kwa Mungu.
Swali.Kama mamlaka zote zimetoka kwa Mungu why wengine wamependelewa kupata viongozi bora na wengine kupata watawala mabogus mfano afrika
 
Anaeijua Sana dini hawezi kuwa fukara labda ataishia kwenye umasikini na sio ufukara
Ok. Umaskini. Huwa hawawi matajiri wa mali na fedha kabisa. Muda mwingi badala ya kupambana kujijenga kiuchumi, unawakuta kanisani. Badala ya kupambana mchana na usiku, unawakuta mlimani siku 40 wanaomba Mungu awafanyie muujiza. Sababu ni kwamba Mungu anataka watu wachape kazi sana. Ila hawa wakereketwa wa dini wao wanaamini zaidi miujiza ya maombi na sio juhudi za kazi. Kwao juhudi za maombi ni kila kitu.
 
Babu zetu watahukumiwa kwa matendo yao maana sheria tayari zilikuwa zimeandikwa katika mioyo yao kabla ya ujio wa dini.
Mfano, walipotaka kufanya matendo mabaya (wizi, uzinzi, uuaji...), walishtakiwa na dhamira zao. Ikiwa waliamua kutenda mabaya hapo hamna excuse!

Umeandika kuwa walikula nguruwe bila kujua na kisha watachomwa moto!
Je umefikiria kwanza ulichoandika hapa?
Mungu kakataza nguruwe na wenyewe wamezila sana yani wakati mungu anasema ni alamu

Sent from my TECNO K8 using JamiiForums mobile app
 
Ok. Umaskini. Huwa hawawi matajiri wa mali na fedha kabisa. Muda mwingi badala ya kupambana kujijenga kiuchumi, unawakuta kanisani. Badala ya kupambana mchana na usiku, unawakuta mlimani siku 40 wanaomba Mungu awafanyie muujiza. Sababu ni kwamba Mungu anataka watu wachape kazi sana. Ila hawa wakereketwa wa dini wao wanaamini zaidi miujiza ya maombi na sio juhudi za kazi. Kwao juhudi za maombi ni kila kitu.
Hao awasali awamjui Mungu,Mungu ni Kazi na sala
 
Hapa kuna theolojia ambayo tunahitaji ufafanuzi wa mtaalam.

Roho Mtakatifu akatuongoze katika hili.
 
Habari wadau!
Huwa namtafakari sana Mungu,je ni kweli hana upendeleo kwa wale wanao amini kama kuna Mungu naombeni jibu.

Binafsi naona kama kuna watu wamependelewa sana wao na familia zao zimependelewa naona mpaka uzao wao pia unazidi kupendelewa.

Au kuna Miungu tofauti tofauti kila mtu anaabudu wake??
kwakwel
 
Warumi 2:11 kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.

Matendo ya Mitume 10:34 Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;

Waefeso 6:9 Nanyi, akina bwana, watendeeni wao yayo hayo, mkiacha kuwaogofya, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo.

MUNGU HANA UPENDELEO WALA HATAKUJA KUWA NA UPENDO NENO LAKE NI KWELI NA HAKI

Naongelea Mungu aliyenibadilisha na kabadilisha maisha ya watu wengi walio mtii
Warumi 9:13. Kama ilivyoandikwa,
Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.
Kwa bahati nzuri haya nzima haijaonyesha ubaya wa Esau.
Mungu hupendelea. Yapo maandiko mengi tu yanayothibitisha hili.
Hivi mtu anaokoka kwa akili na utashi wake?
If no.
Basi utajua kuwa Mungu huchagua(hupendelea).
 
Back
Top Bottom