Yawezekana,Polisi,Mahakama hazina vitendea kazi kalamu,karatasi n.k.Pesa zote wanagawana posho za vikao na marupurupu mengine,pole sana mkuu ndio TZHabari wanajamvi, siku mbili zilizopita nilienda katika hospitali ya wilaya Tandahimba. Nina tatizo ambalo linahitaji upasuaji mdogo lakini nilipofika nikaambiwa sitaweza kufanyiwa kwani hospitali haina GAUZE, daktari akaongeza kuwa hili ni tatizo la nchi nzima kwani hata huko MSD zimeisha.Hivi ni kweli tumefikia hapa? naomba mnifahamishe wanajamvi kama maeneo mengine kuna tatizo kama hili.
Hata Muhimbili hakuna gauze wala iodine, twafa mwakahuu, wao(viongozi wakiongozwa na kikwete) mafua tu Ulaya.
Habari wanajamvi, siku mbili zilizopita nilienda katika hospitali ya wilaya Tandahimba. Nina tatizo ambalo linahitaji upasuaji mdogo lakini nilipofika nikaambiwa sitaweza kufanyiwa kwani hospitali haina GAUZE, daktari akaongeza kuwa hili ni tatizo la nchi nzima kwani hata huko MSD zimeisha.Hivi ni kweli tumefikia hapa? naomba mnifahamishe wanajamvi kama maeneo mengine kuna tatizo kama hili.
Gauze na madawa mengine yakinunuliwa yanahamishiwa kwenye pharmacy zao. Ukifika hospitali wanakuambia hapa hazipo lakini nenda kwenye pharmacy ileee utapata. Katika hili jamii ndo tulaumiwe kwa kulea hali hii katika nchi hii. Kila mtu anajiona hahusiki na kuwa shape hawa watumishi wetu waliojigeuza kuwa ma master wetu. Na ni jamii hii hii tunawa encourage hawa jamaa waibe. Mtu akiajiriwa kama civil servant na maisha yake yawe chini tunamcheka na kumuona kafulia na hatumii akili yake kula kwa urefu wa kamba yake. Akila kwa kamba yake mpaka mpaka majani yanaisha tunalalamika. Kabla ya kulaumu hali hii tujiulize ni nini tumefanya japo kuwastua hawa 'wezi'? Kama tukiona kiburi hawaelewi kwa nini tanzania isiwe misri leo? Hii kulalamika na kwenda kulala majumbani kwetu haitusaidii kitu, tuchukue hatua sasa! Mifano tunayo, INAWEZEKANA!
[font="]issue ya huduma za hospitali tanzania ni scandal. Nashangaa watu hawajaishtukia kiukweli. Ukiugua siku hizi ni very risky kwa sababu hakuna uhakika wa kupata tiba sahihi hata kama una hela za kuhonga watoa huduma. Watoa huduma ni wachache na wengi wao ujuzi wao unatia mashaka na utendaji wao ni wa ubabaishaji. Kukosa gauze msd hakuna anayekosa usingizi from the minister down. Lakini sishangai sana kwani hapo ndipo nchi imefikishwa. Ukikuta kuna uozo katika ngazi ya ukuu wa nchi then what do you expect katika lower levels....!! Hakuna tena rolemodels wa utandaji uliotukuka . Hata hivyo ziko spot ambazo bado zinashine katika hospitali zetu ingawa sio institutional bali ni individuals . Hofu yangu zisije nazo zikaambukizwa halafu ikawa kaput.[/font]
propaganda......