Hivi ni kweli nchi yetu inakosa vifaa vya kutabiri matetemeko ya ardhi na volkano kutoka milimani?

Hivi ni kweli nchi yetu inakosa vifaa vya kutabiri matetemeko ya ardhi na volkano kutoka milimani?

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Aisee, ni uzembe wa hali ya juu sana. Mamlaka ya hali ya hewa ndiyo taasisi pekee iliyotakiwa kuongezwa nguvu na kuwezeshwa kipesa kwa kuwa ndiyo ambayo hushikilia uhai wa watu na wanyama kwa ujumla.

Inasikitisha sana. Mpaka inafikia hatua Mlima Hanang unaleta madhara makubwa kwa watu na mifugo kiasi hiki, uongozi umetulia tu, na hakuna jitihada zozote zinazofanyika ili kuboresha huduma za utabiri wa hali ya hewa, badala yake unaegeshea nguvu nyingi kuwatafuta Geologists ili wafanye tafiti dhidi ya mawe yaliyotoka Mlimani Hanang kama yanaweza kuwa madini. Inauma sana.

Tuseme kwenye volkano na matetemeko ya ardhi tumeshindwa, kwenye mvua je? Au tutaendelea kudanganyana juu ya ujio wa mvua za El Ninho mpaka lini? Ni heri kinga kuliko tiba. Serikali, egesheeni nguvu kwenye mamlaka za hali ya hewa, boresheni huko. Kama huduma hizo zingelikuwa bora, mngetoa taarifa watu waanze kujikataa mapema kutoka kwenye maeneo hayo hayarishi. Mbona nchi za wenzetu tena ndogondogo kama Rwanda zimeweza? Kwani wao waweze wana nini, na sisi tushindwe tuna nini?

Inauma sana.
 
Taarifa: Mamlaka ya hali ya hewa (TMA) inahusika na hali ya hewa, Wajiolojia (Geologists) pamoja na Taasisi ya Jiolojia wanahusika na tafiti za miamba iliyopo juu na chini ya uso wa ardhi ikiwemo pia chanzo au uwezekano wa kutokea matetemeko ya ardhi hivyo kupelekwa wataalam wa miamba Hanang siyo kosa na siyo kwamba wameenda kutafiti madini.

Kwa mujibu wa taarifa ya wataalamu wa Wizara ya Madini pamoja na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa madini (Geological Survey of Tanzania-GST), hakukuwa na tetemeko la ardhi wala mlipuko wa volkano katika mlima Hanang. Chanzo cha maafa haya ni kumeguka kwa sehemu ya mlima Hanang yenye miamba dhoofu iliyonyonya maji ya mvua na kuporomoka (landslide) na hivyo kutengeneza tope (mudflow).

Sehemu hiyo iliyonyonya maji ilizua mgandamizo na sehemu ya mlima ikashindwa kuhimili mgandamizo na hivyo kumegeka na kutengeneza tope ambalo ndilo liliporomoka kufuata mkondo wa mto Jorodom huku likizoa mawe na miti na kuvamia makazi binadamu pembezoni mwa mto na chini ya mlima Hanang. Taarifa ya wataalamu hao imefafanua zaidi kuwa mlima Hanang umeundwa na miamba laini ya chembechembe za mchanga utokanao na volkano (volcanic sediments).
 
Back
Top Bottom