Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,222
- 2,912
Imekuwa kawaida sana kwa wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi ya serikali inayokatwa kupitia VAT ambayo ili iende serikalini inabidi wahusika watoe risiti kwa wanunuzi
Maduka mengi hasa ya vifaa vya ujenzi ukienda kununua bidhaa wanakuonyesha bei mbili uchague unayotaka. Wanakwambia bei hii ni pamoja na risiti (ambayo huwa juu) na bei hii ni ya bila risiti (ambayo huwa chini).
Kwa utaratibu huu unadhani ni mteja yupi ata opt kununua kwa bei ya risiti? Kwa mfano unanunua vifaa vya milioni tano, halafu unaambiwa bila risiti unalipa milioni tano net lakini ukitaka na risiti una lipa milioni tano na laki tatu. Unadhani ni wateja wangapi wako tayari kununua risiti?
Nachojiuliza ni kwanini gharama za kodi ziletwe kwa mlaji wa mwisho? Pia, ni kweli huu utaratibi TRA hawaufahamu? Usalama wa Taifa hawajui? Kwanini wameruhusu nchi kuibiwa hivi?
Ni pesa kiasi gani serikali inapoteza kwa mfumo huu?
Watumishi wa umma na wafanyakazi wengine wanakatwa kodi moja kwa moja kwenye mshahara kupitia PAYE, lakini mtaani watakutana na tozo za taka, bili ya maji, bili za umeme n.k lakini huku wafanyabiashara wanaopata faida kubwa wana enjoy supernormal profit. Huu si unyanyasaji?
Kwanini serikali imewaachia hawa wafanyabiashara kufanya wanavyotaka halafu imewabana wafanyakazi?