Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 22,502
- 48,479
Asipoelewa hapa basi tena.Sababu hiyo ni kodi ambayo ipo kwenye bidhaa na huduma na ni indirect tax ambayo kila hatua ya mzunguko kutoka kwa mzalishaji mpaka kwa mtumiaji wa mwisho kuna 18% inachajiwa.
Kwahiyo kwenye manunuzi inakuwa INPUT TAX na kwenye mauzo inakuwa OUTPUT TAX
Kwa mfano ukinunua kitu 1,200, humo kuna 183.050 (Input Tax)
Ukakiuza kwa 1,800 humo kuna 274.576 (Output Tax)
Vat Payable =Output Tax-Input Tax
Mfanyabiashara anawasilisha tofauti ya (274.576- 183.050)=91.526 mamlaka ya Mapato.
Hapo kama hatoi risiti hiyo ni offence na bado atabanwa kwenye hesabu za mwisho wa mwaka. Ila akinunua mzigo bila risiti na akauza bila risiti anakuwa amefanya Tax Evasion ambayo akibainika adhabu yake ni kubwa. Mfanyabiashara yeye ni wakala wa kuikusanya VAT, ila inalipwa na mlaji wa mwisho.
Inshort ukitaka VAT ilipwe kimamilifu hakikisha manunuzi makubwa yote kutoka viwandani na import yamefanyika kwa risiti. Hii itasaidia kujua nani ana mzigo wa kiasi gani na aliyenunua akiuza bila risiti atakuwa na input kubwa sana italeta alert. Control input then you won't have to worry about output.