Sir robby
JF-Expert Member
- Jun 22, 2022
- 2,396
- 4,080
Wadau najua hakuna kinachoshindikana kwa serikali ikitaka kujua jambo au mambo yote yanayotokea kwenye hiyo nchi, labda tu iwe haitaki. Kuna haya matukio ambayo mpaka sasa serikali haijayapatia ufumbuzi;
1. Kutekwa kwa mfanyabiashara Mo mpaka sasa wahusika hawajakamatwa.
2. Kupigwa risasi kwa mwanasiasa Tundu Lissu mpaka sasa serikali ipo kimya licha ya tukio lenyewe kutokea eneo la makazi ya mawaziri lenye ulinzi na kamera.
3. Kutekwa na kupotea kwa Ben Saanane, Azori Gwanda na wengine mpaka sasa familia zinalia na kuwatafuta ndugu zao bila mafanikio na serikali ipo kimya.
4. Kuvamiwa na Clouds TV na Paul Makonda tukio ambalo ni la kijambazi lakini mpaka sasa serikali haijawakamata wahusika licha ya kufahamika.
Ukweli, wakati umefika kwa matukio hayo ambayo ni mazito na hayajapata utatuzi serikali iyafanyie uchunguzi kwa kushirikisha vyombo vya nje kwani vyombo vyetu ukweli inaonekana vimeshindwa.