Habari Wakuu! Kwa muda mrefu sasa, nime-observe hii trend ambapo sikukuu za hawa wenzetu mara nyingi(kama sio karibu mara zote) zimekuwa zikiangukia siku ya pili ya matarajio.
Swali ni je, hii trend imekuwa ni hivi hivi hata kwa siku za nyuma au ni siku hizi tu?
Je, BAKWATA huwa wako sahihi na wale wanaotangulia kusherehekea siku moja kabla ndio huwa hawako sahihi?
Ukitaka kujiridhisha, chunguza kuanzia mwakani.
Au kuna sababu za kisayansi /kijiografia zinazopelekea mwezi mara nyingi kuandama katika maeneo mengine (uarabuni, n.k) kabla ya huku kwetu?
Binafsi siku hizi huwa sipati shida kujua sikukuu za hawa wenzetu zitaangukia lini kwani siku zote hupiga mahesabu ya siku ya pili ya matarajio ndio itakuwa sikukuu na karibu siku zote imekuwa hivyo.
Mapokeo ni kuandama kwa mwezi ambao haundami siku moja dunia nzima
Pia Kuna kuhitlafiana katika tafsiri ya aya Kama ilivyo kwa dini zote, mfano WaHindu billion moja wanatofautiana mara laki tatu japo kwao wote Krishna Ni Supreme Deity
Acha porojo kwa hiyo umeamini yeye ndo anaficha mwezi na ku uonyesha? Tambua kwamba mwezi ni wa Mungu masiku ya shaka angalia mwenyewe mwezi hujaona uliza walio kuzungukaNakumbuka funga ya ramadhani ya mwaka huu,mufti akiwa anatangaza utasikia anasema tumewasiliana na wenzetu wa ukanda huu wanasema mwezi haukuonekana kwaiyo tutaendelea kumalizia siku 30,sasa katika izo nchi anazozitajaga utasikia Kenya,uganda mpaka comoro tumeongea nao wanasema hawakuuona,ila ramadhani ya mwaka huu 2022 mufti alisema tumewasiliana na wenzetu wa Zanzibar wao wanasema hawajauona ila nchi jirani zetu kama kenya na uganda hakuzitaja aliitaja tu Zanzibar,na mwaka huu Kenya na Uganda wamekula eid kabla yetu sasa sijajua kwanini mwaka huu kawakataa ilihali miaka ya nyuma lazima azitaje nchi jirani,
Ila nilichogundua hapa kuna kama kiushindani kwa sie waislamu kila kundi linajiona bora,nakumbuka ramadhani ya mwaka huu shekhe wa mkoa wa Dsm alialikwa kwenye hafla fulani hapa katika maelezo yake alisema kwa kuwauliza wahudhuriaji mnataka ama mnapenda eid tuisheherekee lini wakajibu basi shekhe wa mkoa akasema ilo limepita akajinasibu si mnajua mie ndio katibu wa mwandano kwa bakwata basi ilo limeisha nitafanya ivyo.....Nilishangaa sana yaani mtu anaamua yeye tu kwa maamuzi na cheo chake kutuamrisha nataka iwe siku fulani ambayo anamaslahi nayo na sio kufuata kama maamuzi ya dini yanavyotaka
Mkuu skukuu ya leo sio ya kuangalia mweziHata Mimi najiulizaga.
Leo asubuhi mwezi nimeiuona, kwanini waislamu huu hawautaki wanataka mpaka Saudia waseme wameuona ndio na Hawa wa confirm?
Mwaka huu ilikuwa hivi: Siku mwezi unaandama ili funga ianze Bakwata walitoa excuse kuwa wamewasiliana na jirani zetu Kenya wakaambiwa bado.Mkuu acha mawazo hayo kuna siku mwezi ushaonekana wazii halafu bakwata wakaukataa ?
Na selikali inamaslahi gani kupangia waislam kufunga na zina pishana siku 1 tu
Mimi sioni tatizo katika hili mana mwezi ni wa Mungu na mbingu ni yake na hua unaonekana pande zote tatizo ni subra tu
Hao bakwata hawana uwezo wakuficha mwezi kuoneka mbaya zaidi hawawi pekee yao kuna nchi zina fwatana pia au na hizo nchi zipo chini ya Selikali yetu?
Sasa kama anga ipo VERY CLEAR na mwezi huonekani, kumbe unamuuliza jirani ili iweje?! Hiyo si ndo ile inaitwa "kuandamisha mwezi?Mwaka huu ilikuwa hivi: Siku mwezi unaandama ili funga ianze Bakwata walitoa excuse kuwa wamewasiliana na jirani zetu Kenya wakaambiwa bado.
Siku ya kufungua Kenya wakatangaza mwezi umeandama ila huku Bakwata wakasema bado hujaandama na wakaelekeza siku inayofuata ndio itakuwa Eid.
Sasa kwanini walishindwa kuwasiliana na jirani zetu tena kama mwanzo?
Ebu tung'amue hili kwanza tunaweza kupata chochote juu ya Bakwata
Unaona hapo, hata kufunga siku 30 condition yake ni kwa sababu umeshindwa kuuona mwezi kutokana na mawingu, na kwahiyo huna uhakika kama umeonekana au hapana!Allah’s Messenger (peace_be_upon_him) said: Whenever you sight the new moon (of the month of Ramadan) observe fast, and when you sight it (the new moon of Shawwal) break it, and if the sky is cloudy for you, then observe fast for thirty days.
Kwani idi ya kuchinja inaenda na muandamo wa mwezi sheikh!???? 🤔Hili jambo ingawaje linakuzwa sana lakini kwa anayefahamu ni jambo dogo sana... huwa lina-trend kwa sababu tu linahusisha holidays.
IPO HIVI...
Kuna HADITHI inasema Mtume alinukuliwa akisema (sio nukuu rasmi)."Fungeni na fungueni kwa kuuona mwezi, vinginevyo iwe kwa kutimia siku 30"
Tafsiri yake ni nini!
Msianze kufunga au kula Idd hadi mhakikishe mwezi umeonekana. Lakini kama zimetimia siku 30 na mwezi hamjauona, basi siku inayofuata fungeni tu au ufungueni tu kwa sababu mweandamo hauwezi ku-exceed siku 30.
Wakati hadithi hiyo inatolewa ilizingatia pia mazingira ya Kijiografia, na kama sikosei, ilitaja umbali... kwamba, hata kama Dar hujaonekana, lakini Tabora umeonekana na mazingira yetu ya kijiografia yanafanana, basi watu wa Dar watafuata habari za Tabora...
NOW...
BAKWATA wao wanashikilia ile conservative definition of the hadith... kwamba, fungeni na fungueni kwa kuona mwezi au kama zimetimia siku 30. Na pia usipoonekana kwenye mazingira yao watafuta habari za maeneo ya jirani...
WENGINE...
Hawa wengine hoja yao ni kwamba, hadith ilitoka zama ambazo hapakuwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia, na ndo maana umbali uliokuwa defined ulikuwa mfupi. Kwahiyo, hivi sasa mwezi unaweza kuonekana Uturuki, na kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, hata watu wa Mpindimbi watapata habari za kuonekana mwezi kwa sababu DUNIA INA MWEZI MMOJA TU!
Aidha, wanadai, kwa location ya Middle East na East Africa, HAIWEZEKANI mwezi uonekane Saudia halafu East Africa usionekane... from geographic point of views coz' hata masaa tunafanana!
REMEMBER... hiyo ni hadith na sio QURAN.
Kwa maana hiyo, Muumini anaweza kutumia "Mwezi wa BAKWATA" au "Mwezi wa Saudi Arabia" kwa sababu almost karibu wote wapo sawa!!
BUT... I repeat, BUT...
Kuna jambo MAJORITY HAWAFAHAMU....
Saudi Arabia HAWATEGEMEI mwandamo wa mwezi perse bali wanatumia the so-called ASTRONOMICAL CALUCULATIONS.
BAKWATA wanaotegemea mwandamo wa mwezi kwa 100%, ukiwauliza tarehe 29/07/2028 ya kizungu itakuwa tarehe ngapi kwa mwezi wa Kiislamu, hawawezi kukupa jibu lakini wanaotumia astronomical calculations watakupa jibu!
Kwa maana nyingine, hata leo hii ukiwauliza Saudi Arabia mwakani Eid itakuwa tarehe ngapi kwa kizungu, WATAKUAMBIA!!
So, unless patokee na kutofautiana kwa wazi kabisa kati ya mwandamo na astronomical calculations lakini Saudi Arabia wanafahamu tarehe ya Eid hata kabla hawajaanza kufunga!!!
Kwa mfano, hii Eid iliyosaliwa leo na BAKWATA, wanaotumia Astronomical Calculations wanakuambia mwaka 2025 itakuwa June 9 and 10
View attachment 2286068
Vipi idi hii nayo ni mwezi pia?? 🤔Sasa kama anga ipo VERY CLEAR na mwezi huonekani, kumbe unamuuliza jirani ili iweje?! Hiyo si ndo ile inaitwa "kuandamisha mwezi?
Tunaweza tusiwapende BAKWATA especially kutokana na tabia yao ya kujiingiza kwenye siasa za CCM lakini kwa hili, BAKWATA wanaweza kuwa sahihi zaidi kuliko wanaodhani ndo wapo sahihi!!
Hadithi zote zinazungumzia suala la KUUONA MWEZI, na hakuna popote inaposema ili mradi Saudi Arabia umeonekana, basi dunia nzima inapaswa kufunga ama kufungua kama wafanyavyo Saudi Arabia!
Hebu tafuta online The Book of Fasting... yaani ni sehemu ya Hadith. Au Google "Sahih Muslim 1087 + The Book Fasting". Moja ya hadith inamzungumzia Umm Fadl. Huyu katoka zake Medina kaenda Syria, kule akakuta mwezi umeandama Ijumaa, na kwahiyo Jmosi pale Syria wakaanza kufunga!
Baada ya mwezi kupita, akarudi zake Medina, kwa hesabu zake alitarajia kule akute Ramadhan imeisha na kwahiyo siku inayofuata iwe Eid. Hata hivyo akakuta siku inayofuata watu wa Medina wanaendelea kufunga. Ndipo akasema kule alikotoka, Mwezi wa Ramadhan uliandama Ijumaa!
Akaulizwa na Abdullah bin Abbas ikiwa aliuona huo mwezi yeye mwenyewe kwa macho yake, akajibu YES, na watu kibao waliuona, na ndo maana Jmosi wakaanza kufunga!
Abdullah bin Abbas akasema "sisi, yaani watu wa Medina hatukuona mwezi Ijumaa bali Jmosi, na kwahiyo kesho tunaendelea hadi tutimize siku 30 au tuone mwandamo!"
Dogo akamuuliza Abdullah bin 'Abbas, ikiwa mwandamo wa kule Syria pale Medina hautambuliki?! Abdullah bin 'Abbas akasema, kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume, HAPANA! Hapana kwa sababu, according to Sahihi Muslim, Hadith No 2378, AbuHurayrah alimnukuu Mtume Muhammad akisema :-
Unaona hapo, hata kufunga siku 30 condition yake ni kwa sababu umeshindwa kuuona mwezi kutokana na mawingu, na kwahiyo huna uhakika kama umeonekana au hapana!
Lakini anga lipo clear, sababu pekee ya kutouona mwezi ni kwavile HUJAONEKANA!! Lakini kwa kuwa hivi sasa tumejiongeza na kuwauliza majirani, basi waulize ikiwa anga lina mawingu lakini kama halina mawingu, unauliza ili iweje?!
That being said, BAKWATA wahukumiwe kwa kutotaka kutumia teknolojia lakini kwa mujibu wa Hadith, BAKWATA wapo sahihi unless kama imewahi kuthibitika Bongo watu wameuona mwezi, na wakatoa ushuhuda kama inavyotakikana na bado BAKWATA wakafinya hizo taarifa... sijui kwa manufaa ya nani au ili iweje.. I DON'T KNOW!!
Bakwata janja janja nyingiNakumbuka funga ya ramadhani ya mwaka huu,mufti akiwa anatangaza utasikia anasema tumewasiliana na wenzetu wa ukanda huu wanasema mwezi haukuonekana kwaiyo tutaendelea kumalizia siku 30,sasa katika izo nchi anazozitajaga utasikia Kenya,uganda mpaka comoro tumeongea nao wanasema hawakuuona,ila ramadhani ya mwaka huu 2022 mufti alisema tumewasiliana na wenzetu wa Zanzibar wao wanasema hawajauona ila nchi jirani zetu kama kenya na uganda hakuzitaja aliitaja tu Zanzibar,na mwaka huu Kenya na Uganda wamekula eid kabla yetu sasa sijajua kwanini mwaka huu kawakataa ilihali miaka ya nyuma lazima azitaje nchi jirani,
Ila nilichogundua hapa kuna kama kiushindani kwa sie waislamu kila kundi linajiona bora,nakumbuka ramadhani ya mwaka huu shekhe wa mkoa wa Dsm alialikwa kwenye hafla fulani hapa katika maelezo yake alisema kwa kuwauliza wahudhuriaji mnataka ama mnapenda eid tuisheherekee lini wakajibu basi shekhe wa mkoa akasema ilo limepita akajinasibu si mnajua mie ndio katibu wa mwandano kwa bakwata basi ilo limeisha nitafanya ivyo.....Nilishangaa sana yaani mtu anaamua yeye tu kwa maamuzi na cheo chake kutuamrisha nataka iwe siku fulani ambayo anamaslahi nayo na sio kufuata kama maamuzi ya dini yanavyotaka
Eid na matukio karibu yote yanatokana na mwandamo wa mwezi. Eid hii huwezi kusikia sana habari za mwandamo kwa sababu, mosi haihusishi funga ya lazima ambayo inakusanya watu wengi na pili, Eid hii husherehekewa siku kadhaa baada ya mwezi kuwa umeshaonekana.Vipi idi hii nayo ni mwezi pia?? 🤔
Kwa mengine lakini sio kwenye hili. Wanachonikera sana BAKWATA ni kujiegemeza zaidi serikalini, na matokeo yake kuwa influenced na siasa za nchi.Bakwata janja janja nyingi