Hivi ni kweli Tanzania kulikuwa na msanii mmoja tu wa maigizo?

Hivi ni kweli Tanzania kulikuwa na msanii mmoja tu wa maigizo?

Kanumba angekuwa hai nadhani ndio angekuwa celebrity mwenye mtonyo mrefu zaidi hapa bongo!
 
!
!
Ngojea nipite tu. Mi Bongo movie waaalah afadhali hata bongo flavor kwa maana ya muziki ila hawa wanawake waobesha mapaja na wanaume wapaka kalikiti walaaaa sinaga mazoea nao
 
Jamaa alikuwa mbunifu na mwenye kujituma sana..RIP Kanumba
 
Mgombea furani wa uraisi alisema akiwa Rais kipaumbele chake ni elimu, elimu, elimu

Unafikilia kwanini kanumba aliweza tusua vidato sita akivyopitia haikuwa magumashi ilimjenga kielimu kweli

Hakuwa muoga wa kuthubutu Hakuwa muoga wa hadhira wala kukosolewa hiyo ndio sifa moja wapo ya mtu aliyepitia darasani na elimu ikamkomboa

Sasa kwa unachouliza nazani jibu umepata wasanii wa sasa waoga kujaribu waoga kukosea waoga kukosolewa

Mfano unamuona shilole na broken English yake wenzake wanaojifanya wanajua kingereza na kumcheka mwisho wa Siku watasema shikamo shilole sababu shilole atakuwa mzuri katika lugha na atakuwa anajiamini sababu anachofanya shilole sasa ndio sifa moja wapo ya mtu anayejifunza lugha ya Pili kuwa ongea kosolewa usisite ongea mwisho wa Siku atatambua makosa nakuwa mzuri katika lugha zaidi ya kina wema sepetu
Aaah huyo anafanya kuchekesha watu tu
 
Huyu ndugu, nakumbuka interview yake moja aliyoifanya baada ya kutoka kutembelea jumba la Big Brother south africa, alilalamika sana namna watanzania walivyokua wakimkejeli kutokana na kukosea kwake kuongea lugha ya kingereza. Jamaa alilalamika kwamba watanzania badala ya kumpa support kwa kazi nzuri aliyokua akiifanya ya kukuza sanaa na jina la nchi, ndio kwanza wanamkatisha tamaa kwa kuendekeza tamaa, akamalizia kwa kusema kwamba " Kama watu hawaoni jitihada anazozifanya, ipo siku miti na mawe vitazungumzia kazi alizokua akizifanya" Ni kweli alijitahidi sana.
Mkuu watanzania ni mabingwa wa kukosoa, yaani unaweza kufanya kitu kizuri wenyewe watafuta sehemu ya kukosoa tuu. Ndio maana kuna watu wanasema usipokata tamaa TZ hakuna mahali duniani unaweza kukata tamaa.
 
mungu alitupa kitu kimoja kimoja kwenye bongo movie alitupa kanumba ndo hivyo kashamchukua kwenye music yupo yule mmanyema wa tandale na kwenye soka yupo mndengereko wa mbagala mkina pazi
 
Sanaa Tanzania ni danguro na genge la wahuni ukitaka dada yako kila siku akatwe mruhusu tu kuigiza
Na ushahidi mzuri tu yule babu Jengua anawakata watoto wadogo tu.
Babu Jengua, kumbe anawakata eeeh!
 
Kanumba alikuwa na uthubutu. Kanumba alikuwa ana jituma sana... Kanumba alikuwa serious sana...

Hawa tulio nao wamebaki kufanya sherehe tuu...

Nyie si ndio mnawafanyisha hizo sherehe?
ImageUploadedByJamiiForums1472887378.313985.jpg

Kiasi sasa wasanii wa Tanzania ndio wanaongoza East Africa kwa kuonekana mabwege.
 
Kanumba alikuwa akiwapa changamoto wasanii wengine, hivyo sasa amekufa hakuna wakuwapa changamoto wengine hivyo ndio maana wengine wanaamua kuwa waimbaji taarabu na bongo …f
 
Ye mwenyewe kwenye uigizaji alikuwa wakawaida tu,alichojitahidi ni on the business side
 
Back
Top Bottom