Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Tanzania ina wasanii wengi mno lakini cha kusikitisha ubinafsi umewapiga kiasi cha kuua kabisa ubunifu wao. Wazee wenzangu tunakumbuka tamthiliya ya tausi ilivyokuwa na mashiko wakati ule.
Hivi inaingi akilini nchi ya uchumi wa kati tunaangalia tamthiliya za wenzetu zilizofasiriwa kwa Kiswahili cha kubumbabumba badala ya Kiswahili sanifu cha Kitanzania?.
BASATA na BAKITA, Sijui kama wanaona Kiswahili kinavyooza kutokana na tawi la sanaa kuachwa katika ombwe. Hali ni mbaya kwenye sanaa ya ndani licha ya wasanii wengi kuwa na ndoto kubwa ya kutoka nje.
Fuatilieni picha za Kinaijeria " Nigerian movies" utaona namna maarifa ya asili " indigenous knowledge inavyopewa kipaumbele" siyo huku tunajifanya Wazungu na kuharibu usemi Mama.." mother tongue" pamoja na utamaduni zetu.
Isidingo the need na Gangaa zimeisha sasa tunasubiria toleo jingine halafu tunakuwa kuambiana sanaa ya bongo kwenye maigizo imekua.