Hivi ni kweli wasanii wengi wa Tanzania baba zao waliwatelekeza?

Umeongea kweri tupu
 
Mkuu mama akiwa bint anaweza kumpenda kijana furani wakaanzisha mahusiano.....
Binti akapata mimba,Ila kwakua mama yake na baba yake(babu na Bibi yako) hawajampenda kwa namna moja au nyingine wanamkataa
Bint huyo akaolewa na mwanaume mwingine ........
Wewe mtoto utapewa sumu Kari juu ya baba yako tangu mdogo,utaishi ukimchukia miaka yotee,.

Siku moja mtafute baba yako ongea nae,from there utagundua kama Ni kweri au Ni sumu ulipewa
 
Ni upuuzi wa mwanamke (mama) kuhamisha chuki za ugomvi wao kwa mtoto.
Hakuna mzazi asiyependa kuishi na mwanaye wa kumzaa mwenyewe, narudia tena huyo baba hayupo na hatokuwepo kwa mazingira ya kawaida.
 
Nashukuru wazazi wangu wote wawili wako pa1. Pia wako karibu na mie.
 
Hapa kuna ukweli, wababa tunajisahaulisha na michepuko badae unakuta watoto wametoboa na wewe huna chochote unabaki kulaani tu watoto kwamba wamekutelekeza wakati wewe ndio ulisababisha yote hayo.

Kuna cha kujifunza hapa.
 
Ni upuuzi wa mwanamke (mama) kuhamisha chuki za ugomvi wao kwa mtoto.
Hakuna mzazi asiyependa kuishi na mwanaye wa kumzaa mwenyewe, narudia tena huyo baba hayupo na hatokuwepo kwa mazingira ya kawaida.

Mkuu labda unatolea mfano huko kwenu Oystersbay, lakini kwetu uswahilini kuna watoto kibao wanataabika baba zao hawajulikani walipo. Utakuta kwenye kibanda umiza wamejazana wanalala kama wapo Big Brother. Kwa hali ile nani anaweza kukataa msaada wa baba?
 
Kama baba yako kakulea vizuri usiongee kwa kauli jumuishi. Kuna wazee ni hatari halafu mbaya zaidi huwa wakifika uzeeni wanatoswa na vimada vyao anabakia kulaumu watoto wamemtelekeza.
Ni upuuzi wa mwanamke (mama) kuhamisha chuki za ugomvi wao kwa mtoto.
Hakuna mzazi asiyependa kuishi na mwanaye wa kumzaa mwenyewe, narudia tena huyo baba hayupo na hatokuwepo kwa mazingira ya kawaida.
 
Kama baba yako kakulea vizuri usiongee kwa kauli jumuishi. Kuna wazee ni hatari halafu mbaya zaidi huwa wakifika uzeeni wanatoswa na vimada vyao anabakia kulaumu watoto wamemtelekeza.
Ukiona mwanaume anatelekeza mtoto wake basi ujue kuna jambo ambalo sio la kawaida.
Achilia mbali kulelewa vizuri, mimi pia ni mzazi najua nacho kiandika mkuu.
 
Ni upuuzi wa mwanamke (mama) kuhamisha chuki za ugomvi wao kwa mtoto.
Hakuna mzazi asiyependa kuishi na mwanaye wa kumzaa mwenyewe, narudia tena huyo baba hayupo na hatokuwepo kwa mazingira ya kawaida.
Kweli asee
 
Ukifuatilia visa vya hao watoto utagundua nachosema kina mashiko.
Halafu huko Ostersbay ndo wapi mkuu....karibu kwetu Ndono - Uyui ujionee ukarimu wetu.
 
Ukifuatilia visa vya hao watoto utagundua nachosema kina mashiko.
Halafu huko Ostersbay ndo wapi mkuu....karibu kwetu Ndono - Uyui ujionee ukarimu wetu.

Mkuu watoto waliotelekezwa huko uswahilini ni wengi sana, hivyo visa unavyosema sijui kama vinatosha kuwa excuses.
 
Kumbe upo ndono.
Ukifuatilia visa vya hao watoto utagundua nachosema kina mashiko.
Halafu huko Ostersbay ndo wapi mkuu....karibu kwetu Ndono - Uyui ujionee ukarimu wetu.
 
Hii sio kweli, sema kwa vile ni kesi chache ni rahisi kwako kuhitimisha hivyo... ni sawa na ile kuamini kuwa wenye mashoto (left handed) wengi wao ni mashuhuri.

Hii inakuwa wengi wao kati ya wangapi.?
 
Baba yako kakulea wee kuanzia chekechea mpaka chuo, kwanini akutelekeze wakati tayari anakaribia kula matunda? Lazima kuna sababu sio bure,kuna rafiki jirani yetu amegoma kabisa kumpeleka mtoto chuo,sio kwamba hana uwezo la hasha ,Kijana kaanza kibri anaingilia ugomvi wa wazazi wake halafu anakuwa upande wa mama yake ,unatarajia nini hapo?
Mfano unamwambia baba yako,baba wacha dharau hizo, unamdharau sana mama yangu,yaani unamwonyesha umwamba baba yako,halafu umesikiliza malalamiko ya upande mmoja tu wa Mama yako,je wewe ukiwa baba utaendelea kumthamini huyo mtoto?
 
Sio wakiachana tu hata baba akioa mke wa pili tu inakuwa shida,Bibi mkubwa anaanza kuwanywesha sumu watoto mwisho wa siku watoto wanamuona baba si lolote wala si chochote,na baba naye akiona hivyo lazima aonyeshe ubaba wake anakata laini,na anaweza akawatamkia kuanzia leo mama yenu ndio baba yenu,tusijuane
 
Tatizo hili kwa kiasi kikubwa linachangiwa na watu kuzaa nje ya ndoa...laiti watu wangefuata misingi ya dini na kuoana kihalili kabisa basi hizi kesi za watoto kutelekezwa na baba zao zingekuwa chache mnoooo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…