Hivi ni kweli wasanii wengi wa Tanzania baba zao waliwatelekeza?

Hapa kuna ukweli, wababa tunajisahaulisha na michepuko badae unakuta watoto wametoboa na wewe huna chochote unabaki kulaani tu watoto kwamba wamekutelekeza wakati wewe ndio ulisababisha yote hayo.

Kuna cha kujifunza hapa.
Yaani hapa hawakumbuki wala kulisema, wengi akili yote huishia kwa michepuko, siku yanamshinda huko ndiyo anamkumbukà mkewe anakuta tayari.watoto walishakuwa na kujitafutia, laana zinanza, unajiuliza mbona yeye alipomkimbia mkewe na watoto hawakumlaani kapiga mbizi huko mpaka kachoka?
 
Wanahesabu umri wakiona miaka sasa zaidi ya 20 wataanza kijileta kwa watoto
 
Kama baba yako kakulea vizuri usiongee kwa kauli jumuishi. Kuna wazee ni hatari halafu mbaya zaidi huwa wakifika uzeeni wanatoswa na vimada vyao anabakia kulaumu watoto wamemtelekeza.
Kuna Kaka aliondoka na kumwambia mkewe naenda kuoa huko, kamuacha mkewe na mtoto dada kapambana mwanaye kamaliza STD 7 kafaulu Baba anapita mule na bodaboda, form one Mzee kagoma kutoa pesa , ikabidi huyo dada aongee Kaka zake kumsaidia baada ya miaka 2 anamwambia mwanaye shule ya nini halafu unamsikiliza sana mama yako, kazi zakufanya zipo nyingi, mtoto kampuuza akamaliza shule kwa hisani ya wajomba, Baba anabadilisha michepuko huko! Subili mtoto aje kupata kazi ndiyo wale wababa walaamishi !
 
Ukiona mwanaume anatelekeza mtoto wake basi ujue kuna jambo ambalo sio la kawaida.
Achilia mbali kulelewa vizuri, mimi pia ni mzazi najua nacho kiandika mkuu.
Sio kweli acha kutetea maovu kama una ndugu zako wa kike wewe andaa pesa zakusomeshea wajomba zako
 
Domo alipokuwa na wema alikuwa karibu sana na babaake ...alipo achana na wema akamletea babaake chuki
 
Huyo hakutelekezwa na baba ya yake, mama ndiye aliyekimbia na watoto kwenda kuolewa kwingine baada ya hali ya uchumi ya mumewe kuwa ngumu
Aaaaiiiseee! Kwa hiyo Hemed alikuwa anajaribu kumu cover up mama yake? Huo uchotara wa Hemed unatokana na mama yake au baba yake? Mimi nilimsikia tu anamponda baba yake E tv alikuwa anafanyiwa mahojiano na Jonijo. Nazani siku hiyo alikuwa amevuta bangi pia maana alikuwa anajisifia yeye ni mzuri( good looking),pia anapenda sex( kufanya ngono), pia yuko vzr kitandani( good in bed),na kwamba anaweza kumiliki hata wanawake mia 9 wote wakawa daraja moja( main chicks).
 
Kwenye No.1 umemaliza kila kitu mkuu.
 
Ipo haha ya kuwaandalia semina ma-star wetu jinsi ya kuongea na Media
 
Tatizo hili kwa kiasi kikubwa linachangiwa na watu kuzaa nje ya ndoa...laiti watu wangefuata misingi ya dini na kuoana kihalili kabisa basi hizi kesi za watoto kutelekezwa na baba zao zingekuwa chache mnoooo...
Kabisa mkuu pia ukiangalia wasanii wengi ambao wametelekezwa baba alimuacha mama ake akaenda kuoa mke mwingine na hisi hapa ndo shida ilipoanzia hakuna mawasilianao
 
Baba yake ni mwarabu alikuwa pale tanga mjini stand ya ngamiani akiuza change na baadaye alishindwa hiyo kazi sababu kubwia unga akala hizo change akafungwa gereza la maweni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…