Nawaza kati ya haya:
1. Wametoka kwa single mothers - ni kawaida kwa dunia ya sasa kumpa mimba binti na kusepa. Wadada wengi wanajali raha ya muda wasiwaze matokeo ya starehe hizi.
2. Mimba zenye utata - zamani hizo hakukuwa na DNA test, hivyo mwanamke akiwa mwingi wa habari alikataliwa na wote pale alipopeleka ujauzito. Hii inatokana na tabia mbovu ya mwanamke mwenyewe.
3. Kuzaa na mwanamume ambaye hakuwa tayari zaidi ya kutaka starehe tu. Baadhi ya wanawake hudanganywa kuwa wakibeba mimba ya mwanamume wataweza 'kupendwa na hivyo kujihakikishia ndoa.
4. Kuzaa na mume wa mtu. Hapa wanaume wengine hukataa katakata ili kunusuru ndoa zao halali. Wengi hutaka starehe za muda tukutokana na tamaa.
5. Mabinti wadogo kuangukia mikono mwa matapeli wa mapenzi, baadaye kuwakataa ama kuwakimbia.
6. Ndoa kuvunjika na mama kukimbia na mtoto, ama ndoa kuvunjika na mume kususa mke na mtoto. Pia mazingira ya hivyo ya siku hizi, mke kutumia mtoto kama njia ya kiuchumi dhidi ya baba wa mtoto pale wanapotengana.
Ukitaka kujua mazingira ya huu upupu tafakari ule mwito wa Ret.RC wa Dar kwa wajane na waliotoswa. Asilimia kubwa waliokwenda pale walikuwa na malalamiko ya kuzalishwa kisha kutoswa. Tazama aina ya wanawake waliokusanyika pale, wengi ni "watema shombo wakubwa." Mfano ni yule madame aliyemwanika mumewe mitandaoni kuwa hatunzi watoto wake, kisha akaibukia kwa RC.