Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Nimemuona Sisty Nyahozya kwenye Mkutano Mkuu wa CHADEMA, lakini pia nimemuona kwenye Mkutano Mkuu wa ACT WAZALENDO , huku nimemuona akipewa na Airtime ya kuongea na Wajumbe .
Kiukweli nimekwazika sana na uwepo wa mtu huyu kwenye mikutano ya vyama hivi , na wala sina kumbukumbu kama amewahi kuhudhuria mikutano ya CCM na kupewa heshima kama alivyofanyiwa na vyama hivi , bila kumung'unya maneno mimi binafsi sijawahi kuipenda ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.
Hii ni kwa sababu ofisi hii imekuwa mara zote ikifanya kazi ya kutumwa na CCM ili kukandamiza wapinzani , huku watendaji wake akiwemo huyu Sisty na boss wake Mutungi wakitajwa kama wanachama watiifu wa CCM, hatuna haja ya kurudia kutaja uchafu wao, lakini mgogoro ule wa CUF ulionyesha dhahiri upande wa ofisi ya Msajili, ambapo ofisi hii ilisimamia kikamilifu wizi wa hela za CUF kupitia akaunti binafsi kinyume kabisa cha Katiba ya nchi ili kumfaidisha mtu wao Lipumba .
Sioni sababu yoyote ile iwe ya kijinga au ya maana ya kumkaribisha adui kwenye mikutano ya vyama vya siasa , ile methali ya kizamani inayosema "MCHAWI MPE MWANAO AKULELEE" imepitwa na wakati vibaya sana ! ifike wakati maadui wa Demokrasia watengwe hata kama wana mamlaka, na wananchi waelezwe adui yao ni yupi .
Hatuwezi kukubali kufuga majini chumbani, yatamaliza watoto.