Hivi ni lazima Mawaziri wanapoongea kumtaja taja Rais kila baada ya sentensi mbili?

Walamba miguu hao. Wanafanya hivyo ili waonekane ni loyal kwa aliyewateua. Mtaani kugumu huyo akiwekwa benchi ataanza kulia njaa.
 
Hii tabia ilianza kwa Jiwe.. huko awamu nyingine haikuwepo... na ndio inaendelea
 
Sisiemu hakuna timamu
Col 2:3
 
Ni maelekezo vinginevyo ataondolewa kwenye kitengo
 
Shida ni kwamba viongozi wengi bado wameshindwa kutofautisha interest za Rais Samia na Interest za Mwendazake! Kwa Mwendazake hiyo ilikuwa sawa kabisa na walitaja kila wakati hadi awamu ya serikali! Lakin kwa mama naona wanajichanganya tu labda pengine sababu PM pia ana utamaduni huo!
Inashangaza waziri wa serikali badala ya kusema ....Serikali inataka kuona wananchi waki.......Yeye lazima amtaje Rais, hapa sidhani kama hata Mhe. Rais mwenyewe anavutiwa na utamaduni huu!
 
C in C hakwepeki mzee.
Yote yanafanywa na yeye
Haya yameanza awamu ya 5 jee hizo awamu zingine hazikuwa na ma commander in chief?
Ni ushamba mtupu ulioanzia Chato na kwa vile huyu mama ni uzao wa awamu ya 5 basi mambo ni yakeyale
 
Rais ni kama maji hawezi kumkwepa kumtaja maana kila anachoongelea anafanya Rais utekelezaji wote anafanya Rais
 
Rais ni kama maji hawezi kumkwepa kumtaja maana kila anachoongelea anafanya Rais utekelezaji wote anafanya Rais
Hata pumzi yako ni kutoka kwa Rais sio ee? Mimba ya mamako ilitokana na juhudi za Rais?
 
Kiukweli ni Njaa zunawaginga vichwa wanadhani wasipoweka sifa basi hawaonekaniki kufanya kazi! Na wakiachwa hawajui waende wapi?!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…