Pole mkuu kwa changamoto unayopitia.
Kama mdau alivyosema huenda mikopo ndio inakutesa zaidi kwa maana umekopea mshahara na hela ya mkopo imeisha lakini majukumu yako pale pale na imefikia wakati mshahara hauwezi kukidhi mahitaji.
Usikate tamaa, punguza matumizi yasiyo lazima, punguza kusaidia ndugu pasipo ulazima (kuwa bahiri na ukubali kusemwa na hao utakaowanyima hela). Shida za familia zetu huwa haziishi hasa kwenye extended families, shida zingine ignore sema huna hela hata kama ipo. Kubali nao wapitie kipindi kigumu cha mpito hawatakufa, hii itakupa ahueni ya mzigo kwenye matumizi kwa kiasi kidogo cha pesa unachopata.
Kubali kuwa umekosea mahali fulani jipe mda urekebishe kosa hilo (mpaka utakapomaliza kulipa mkopo).
Jitahidi kulipa madeni uliyokopa, usijaribu kudhulumu uliowakopa bora ulipe kidogo kidogo kuliko kudhulumu.
Punguza matumizi then ufocus kwenye kulipa madeni hasa hasa ya watu binafsi maana kama ni ya benki unakatwa automatically.
Kingine jitahidi kufanya saving hata kama ni ndogo kiasi gani iweke tu at least 10% ya unachopata kama utaweza.
Kwa sasa usifikirie kuacha kazi endelea na kazi ila acha kuwaza kwamba watu wengine watakuonaje kwa hali yako ya sasa. Hayawahusu, ishi maisha yako usiishi watu wanavyotaka uishi, ishi utakavyo kulingana na hali yako.
Nakutia moyo kuwa hayo unayopitia, kwenye maisha hutokea kwa wengine pia. Mwiko kukata tamaa maadamu una afya njema mengine unaweza kuyafix na ukabadilisha kabisa hali uliyo nayo kwa sasa na ikawa historia. Jipe mda!