Hivi ni mimi tu haya maisha yanataka kunikataa?

asante mkuu ubarikiwe
 
Dah !
Uchumi wa kati huo mamaeeee[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Huwa naamini ukiweza kuishi nchi ngumu kama Tanzania ,unaweza survive popote
Kenya je
 
Msoto wa Tanzania ni nuksi , sasa imagine wewe upo kwenye ajira na cha moto unakiona na kutoa yowe hivyo ,
Je sisi majobless huku mitaani tusio na ajira , wala biashara au kipato cha kueleweka tunaishije ?

Huo ugumu wa maisha unaoexperience hapo kwenye ajira haifiki hata nusu ya ugumu wa life la kitaa
 
Pole Sana .

Ila ungeanza kujikita katika vipaumbele kwanza .

Mfano Una familia ya watu watano wanakutegemea.

Na unaona mshahara hautoshi , hapo jibu linakuja kuwa unabidi kuanza kujijenga kwanza wewe ili usimame then ndo uwasimamishe ndugu zako.


Mshahara wa ualimu ni Mdogo Sana hivyo ungeweza kufikiwa kwa kuweka vipaumbele kwanza.


naweza kusema mkuu kuna mambo hayapo sawa katika mpangalio wako wa mambo ktk uchumi .

Kukopa ni vizuri ikiwa Unaenda kuizalisha hiyo hela
Ila Kutokukopa ni vizuri zaidi ikiwa hauna jambo la msingi unaenda kufanya.

Hivyo usiache kazi Ila punguza matumizi ili yaendane na kipato chako .
 
Maisha bhana muda mwengine hayataki unyooke sanaaaa!

Sijajua kwa kazi za walimu zipoje! Ila kwenye kazi hiyo hiyo kama kuna mianya ya namna fulani ya kupiga wewe jiseti halafu piga.

Muhimu usidhulumu mtu.
 
Regardless of the situation, never give up!

njoo nikukopeshe tena weka kiwanja bondi
ushauri: Ndugu yangu kama unapata mshahara kama 350,000 after tax, chukua 150,000 mapema sana weka Mpesa yani usiiguse hii hela jikaushe kabisa, itakusaidia kuanza maisha mengine baada ya miezi kadhaa..

Any way mimi ni mpambanaji mwenzio.. nilianza biashara ya kausha damu kwa mtaji 40,000 tu sasa hivi nina 2,000,000 na nishanunua kiwanja. nakula navaa nalipa kodi na nasaidia wazazi pia.

Najikausha kama vile sizioni starehe
 
Maisha bhana muda mwengine hayataki unyooke sanaaaa!

Sijajua kwa kazi za walimu zipoje! Ila kwenye kazi hiyo hiyo kama kuna mianya ya namna fulani ya kupiga wewe jiseti halafu piga.

Muhimu usidhulumu mtu.
labda uuze boksi la chaki
 
labda uuze boksi la chaki
Kama hali ndiyo hiyo kitu muhimu hapo jijenge wewe mwenyewe kwanza.

Ukishaweza kufika level fulani itakuwa ni rahisi kwako kuweza kuwanyanyua wengine mmoja baada ya mmoja.

Ila kwa sasa hiyo nguvu hauna! Kuwa mbinafsi. Jijenge mwenyewe kwanza.
 
Kama hali ndiyo hiyo kitu muhimu hapo jijenge wewe mwenyewe kwanza.

Ukishaweza kufika level fulani itakuwa ni rahisi kwako kuweza kuwanyanyua wengine mmoja baada ya mmoja.

Ila kwa sasa hiyo nguvu hauna! Kuwa mbinafsi. Jijenge mwenyewe kwanza.
asante kwa ushauri mkuu
 
Huwa nawashangaa sana watu ambao wako kwenye ajira halafu wanawaza kuacha kazi. Wakati kuna watu wanaenda mpaka Kwa waganga ili wapate hiyo ajira. Tatizo linaanzia pale unapojitwika majukumu ambayo yako juu ya uwezo wako mpaka unaingia madeni. Nakushauri usifikirie kuacha kazi. Nitumie ajira uliyonayo kufanikiwa kimaisha. Kama uko mjini omba uhamisho ukae kijijini, Lima mazao kama mpunga, ufuta, alizeti, au Katanga nk. Ukivuna toa shukrani Kwa Mungu.
 
Samahani kama sitakufurahisha Kwa ushauri wangu ,
Hizi ajira zinapaswa kuangaliwa Kwa mapana yake la sivyo unaweza ukaishi maisha magumu isivyo kawaida. Hakuna sababu ya kuendelea kufikiria ajira
Angalia nje ya box mbona watu wamejiajiri na wanafanya maisha safi yanaenda

IF YOU DON'T LIKE SOMETHING CHANGE IT , IF YOU CAN'T CHANGE IT CHANGE YOUR ATTITUDE

THINK BIG ACHA KUOGOPA HAKUNA MTU MUOGA ALIYEWAHI KUFANIKIWA MAISHA NI VITA HALISI PIGANA ILI UISHI AU ZUBAA YAKUUE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…