Hivi ni mwanasiasa Gani alikuwa na Kingereza kizuri Kama B. Mkapa

Hivi ni mwanasiasa Gani alikuwa na Kingereza kizuri Kama B. Mkapa

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania kipindi Cha nyuma aliwahi kusifiwa Kwa umahiri wake wa kuongea lugha ya Kingereza na Waandishi wa Habari wa CNN wakati wakimhoji na Ile ni kutokana na umahiri wake mkubwa wa kutema Yani, kutema ung'eng'e, lugha ambayo ilikuja Tanzania Kwa Njia ya Meli, lugha pia ambayo inawasumbua watanzania wengi wakiwemo wanasiasa na wasanii wa bongo movie Kwa ujumla.

Rais nyerere pia alikuwa ni mtaalamu kweli kweli wa lugha, Tena bila kuandikiwa , alikuwa anaweza kubishana Kwa kingereza Kwa masaa hata matatu bila kuchoka kama alivyokuwa Mkapa , lakini Mkapa alikuwa vizuri katika lugha zaidi ya Nyerere.

Rais Mkapa licha ya kutema yai lililonyooka na grammer iliyosahihi alisomea masomo ya juu ya Kingereza na pia alikuwa mwandishi wa habari. Zamani waandishi wa habari nao walikuwa ni wajuzi zaidi katika kingereza mtu kama hamza kasongo, this week in perspective(jina nimesahau), jenerali ulimwengu walikuwa miamba wa kingereza tofauti na waandishi wa habari wa Sasa kina Mwijaku, baba levo, masanja mkandamizajji, masoud kipanya kingereza hawajui kabisa.

Hivyo nadiriki Kusema Rais Mkapa alikuwa ni mwanasiasa mwenye kingereza Bora wa Tanzania wa Muda wote yaani GOAT/MBUZI i.e the greatest of all time. Najua Kuna wale machawa watasema yule wa kuupiga mwingi ndo anajua sana kingereza ,
 
Ili muwe na taifa huru mnapaswa kuwa na utamaduni wenu na lugha yenu. Kuona lugha za wageni ni za maana huo ni utumwa wa fikra. Kujifunza kiingereza na lugha zingine za kigeni ni vyema lakini kumudu kuongea lugha za kigeni sio ujanja na kushindwa kumudu kuongea lugha za wageni sio ushamba
 
Labda niweke hivi lugha mpya mara nyingi ni tatizo kwa wengi tu!, Hata wazungu hiyohiyo English inawamaliza kinyama tena wenzetu akiwa haijui anakuambia kabisa kuwa haipandi hivyo mtazungumza machache mno!.
ila kuna waingereza na wamarekani kudadeki hawa usipodindisha sikio hamtaelewana!.
Mfano black American wanaongea haraka haraka japo sio wote na namna wanavyo pronounce maneno mnaweza kuchengana!.

Nilishawahi kukutana na black america wawili ktk hao wawili mmoja ni anaongea fasta fasta inabidi umsikilize vizuri!, mpk yule mwenzake akaanza kuniambia kama unaweza kumsikiliza huyu basi we English unaijua!.
lkn nilikuja kukutana na lizungu kudadeki ile English sijui ya wapi..🤣

Lugha ngeni huwa sipendi sana kumsema mtu na pia vichwa tunatofautiana kwenye kushika lugha!, wapo watz wanaongea English wazungu wenyewe wakasome!.
ila tu lugha mama kila mtu anatakiwa kuijua vyema!, ukishindwa kuijua lugha yako mama mi nakusema ila English we charanga kosea ilimradi tunaelewana sio shida zangu!..

Ni hitimishe tu hivi "ujuzi wa lugha nao ni kipaji".
 
Utumwa wa kifikra. Hata hivyo wote Nyerere, Mkapa etc ni wababaishaji wa Ze,ze,ze. Ni ngumu kuwa nguli wa lugha kama siyo lugha yako ya kila siku.
 
Kiingereza hakina faida yoyote katika ustawi wa Taifa letu.. Mfano china mwaka 1960 /1961 alifanya kitu kinainatwa mabadiliko ya kiutamaduni na kuchoma vitabu vyote vilivyokuwa kwenye lugha ya kiingereza wanakipa kiingereza kipaumbele...ona Leo wapo mbali sana ...mm nikiwa kiongozi nitaanza na mfumo wa elimu .. kiingereza kitafundishwa kama somo tu...mambo mengine yote kuanzia elimu ya awali mpaka bio vikuu Kiswahili ndo kitachotumika
 
Halafu baada ya kujua kingereza akiba kiasi gani Cha pesa na ardhi??
 
Benjamin William Mkapa ,Rais wa Tanzania kipindi Cha nyuma aliwahi kusifiwa Kwa umahiri wake wa kuongea lugha ya Kingereza na Waandishi wa Habari wa CNN wakati wakimhoji na Ile ni kutokana na umahiri wake mkubwa wa kutema Yani, kutema ung'eng'e , lugha ambayo ilikuja Tanzania Kwa Njia ya Meli, lugha pia ambayo inawasumbua watanzania wengi wakiwemo wanasiasa na wasanii wa bongo movie Kwa ujumla.

Rais nyerere pia alikuwa ni mtaalamu kweli kweli wa lugha, Tena bila kuandikiwa , alikuwa anaweza kubishana Kwa kingereza Kwa masaa hata matatu bila kuchoka kama alivyokuwa Mkapa , lakini Mkapa alikuwa vizuri katika lugha zaidi ya nyerere.
Rais Mkapa licha ya kutema yai lililonyooka na grammer iliyosahihi alisomea masomo ya juu ya Kingereza na pia alikuwa mwandishi wa habari. Zamani waandishi wa habari nao walikuwa ni wajuzi zaidi katika kingereza mtu kama hamza kasongo, this week in perspective(jina nimesahau), jenerali ulimwengu walikuwa miamba wa kingereza tofauti na waandishi wa habari wa Sasa kina Mwijaku, baba levo, masanja mkandamizajji, masoud kipanya kingereza hawajui kabisa.

Hivyo nadiriki Kusema Rais Mkapa alikuwa ni mwanasiasa mwenye kingereza Bora wa Tanzania wa Muda wote yaani GOAT/MBUZI i.e the greatest of all time. Najua Kuna wale machawa watasema yule wa kuupiga mwingi ndo anajua sana kingereza ,
Kwahiyo ndugu mtanzania mwenzangu.. unataka kusema kwamba, kuongea kingereza ndo usomi?
 
Kuna Oscar Kambona pia alikuwa anakijua, wanasema hata January Makamba naye yuko vizuri, lakini watanzania wengi wanaokijua vizuri ni wale waliosoma au walioishi kwenye hizo nchi
 
Kati ya Marais tuiowahi kuwa nao mwalimu ndiye alikuwa mzungumzaji mzuri wa lugha ya kiingereza.

Alikuwa mzungumzaji mzuri sio wa kiingereza tu hata kuongea mbele za watu. Nadhani kusoma vitabu vingi na uandiahi wa vitabu achilia mbali alivyovitafsiri vilimsaidia kuwa mzungumzaji mzuri. Alikuwa hatumii nguvu kufikisha ujumbe.
 
Back
Top Bottom