Wanashiriki CAF vilabu kwa sababu kwa sababu , kisheria Znz haitambuliki FIFA ,hivyo ikapelekea Tanzania tukawa na nafasi 2 tu za vilabu toka Tanzania katika mashindano ya CAF kwa maana ya Champions League na Shirikisho
Turudi nyuma miaka ya 90 Tanzania ikiwa ina nafasi mbili tu za ushiriki ,ilitumia mtindo wa LIGI YA MUUNGANO kupata wawakilishi wawili ,tunakumbuka ligi hii ilishirikisha timu 3 toka Bara na 3 toka Tanzania visiwani ( enzi za TFF na ZFF )
CAF na FIFA wakaleta mabadiliko ambapo bingwa ligi ya nchi mwanachama atacheza CCL na mshindi wa kombe la FA ( chama cha soka cha nchi itashiriki shirikisho )
Hapa ki kanuni znz ikawa nje ,ila CAF kwa busara na kutaka kula wakaipa 'favor' ZFA kushiriki vilabu vya znz michuano ya CAF ya vilabu tu hivyo katika vilabu CAF imeipa znz heshima hy
Tanzania bara tukabaki na TPL ambayo bingwa anacheza CCL na mshindi wa Azam cup FA anacheza shirikisho
Kwa utaratibu huu Tanzania bara na Zanzibar tulikuwa na timu 6 ktk michuano ya CAF mwaka huu 2019/2020
Nimejaribu vile najua ,naruhusu kusahihishwa
MTC | 101| [emoji769]