Pre GE2025 Hivi ni sababu gani zinafanya tusitumie Vitambulisho vya Mpiga Kura vya kawaida vya INEC kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa?

Pre GE2025 Hivi ni sababu gani zinafanya tusitumie Vitambulisho vya Mpiga Kura vya kawaida vya INEC kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hapana sio hivyo. Ni lazima uandikishwe ndio utapiga kura. Kama unachonkitambulisho na haujaenda kuandikiahwa jua hutaruhusiwa kupiga kura kuchagua mwenyekiti wa mtaa
 
Hilo daftari la INEC halioneshi mtaa/ kitongoji anachotoka mpiga kura. Ni daftari la kata kwa ajili ya uchaguzi wa diwani wa kata, mbunge na rais.

Hili daftari la mtaa ni kwa wakazi wa mtaa/ kitongoji husika pekee kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa mtaa wao. Ni daftari dogo sana la orodha ya wakazi wa mtaa husika ambao idadi yao kwa kawaida huwa haifiki hata watu mia moja ie nyumba 100. Lingeweza pia kutumika kuchagua viongozi wa nyumba kumi.
Sawa..

Lakini hoja hapa ni kupunguza au kuondoa gharama kabisa za kuendesha zoezi Moja mara mbilimbili kwa kuzitumia taasisi mbili tofauti ndani ya nchi moja..

Kwani Kuna ugumu gani INEC ikaandaa daftari kwa mfumo huo...?

Na kwa kadiri ya ufahamu wangu, hata INEC vituo vyao vya kuandikishia wapiga kura huwa ktk kila mtaa au kitongoji na ndivyo hivyohivyo TAMISEMI wanatumia kwenye zoezi lao linaloendelea sasa...

Kwa hiyo ndo kusema kuwa, wapiga kura ktk daftari la INEC wako categorized ktk mitaa na vitongoji vyao tayari...

Kwa hiyo hakuna sababu yoyote ya msingi hili zoezi kufanyika mara ya pili wakati INEC ilishafanya kazi yake..

Therefore, kwa kinachofanywa na TAMISEMI it's a total wastage of time and national money🤑🤑
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Unaofanyika ni uboreshaji kuna watu wamehama makazi, wapo pia waliopoteza vitambulisho vyao na wapo waliofika umri sahihi wa kupiga kura yaani miaka 18.
Ila kama hujahama makazi na kitambulisho unacho utatumia hicho hicho unacho takiwa ni kwenda kuhakiki kwamba utakuwepo tu.
Hujaelewa hoja yangu...

Yote haya unayosema wewe yalishanywa na TUME HURU YA UCHAGUZI wiki chache zilizopita...

Swali langu ni kwanini TAMISEMI inafanya zoezi hilohilo tena la kuandikisha wapiga kura upya wakati INEC ilishafanya kazi hiyo tayari...?

Na kumbuka kuwa, hawa TAMISEMI hawaboreshi daftari bali kila mtu ni lazima, ajiandikishe upya ili ashiriki uchaguzi wa November, 2024....

Baada ya uchaguzi huu kupita bila shaka na daftari lao linakuwa limesha expire na uchaguzi wa serikali za mitaa ujao wa mwaka 2029 kama mfumo huu utaendelea kutumika, basi ina maana tutajiandikisha tena upya....!!

Unaona utaratibu huu ulivyo wa hovyo na kugharimu fedha nyingi bila sababu za msingi pesa ambayo ingetumika kuhudumia mahitaji mengine ya wananchi...?
 
Sawa, sasa nakusaidia ufahamu kuwa kuna tofauti ya kushinda, na kutangazwa kushinda.
Hayo ni mazungumzo baada ya habari, kila mmoja anaweza kusema lake, lakini ukweli wa mambo habari imekwisha
 
Mtoa mada si kweli zoezi la tume huru ya uchaguzi limefanyika Tz nzima, zoezi hilo linaenda kwa mikoa nadhani mwezi uliopita lilifanyika mkoa wa sindida.
Niungane na wewe kwenye hoja ya kuwa na kitambulisho kimoja kitakacho tumika kwenye chaguzi zote mbili
 
Unaofanyika ni uboreshaji kuna watu wamehama makazi, wapo pia waliopoteza vitambulisho vyao na wapo waliofika umri sahihi wa kupiga kura yaani miaka 18.
Ila kama hujahama makazi na kitambulisho unacho utatumia hicho hicho unacho takiwa ni kwenda kuhakiki kwamba utakuwepo tu.
Nina shaka na ukweli kwenye maelezo haya
 
Kwa vyovyote vile naona kuna inconvenience kubwa na gharama zisizo za lazima kwenye mchakato huu... hii huenda ni kukosekana matumizi ya teknolojia kwenye mchakato huu
 
Ni mbinu ya CCM kuchomeka hadi wanafunzi wawapigie kura
 
Hii ya daftari la Kudumu la wapiga kura la INEC ilikua muhimu sana..imefanyikia lini mkuu
Hiyo INEC ni lini iliwahi kuwa na mawasiliano na sisi wapiga kura! Vitambulisho vyetu ni vya NEC ambavyo havijaidhinishwa na INEC amnayo ni NEC iliyosilimu bila idhini ya wazazi.
NEC ni ileile na wanaccm walewale na uongo na ulaghai wao ni uleule.
 
Back
Top Bottom