Kwani ni nini maana ya shikamoo? Unanikumbusha mtu anayesema anaona shida sana kumpa shikamoo mtu ambaye wamepitiana.Mwingine akadai kwamba mtu amwombaye "chadema" yaani V hana adabu na anaona anadharauliwa kuombwa.
Sasa mimi sielewi, kama aliyekuzidi umri anastahili kumpa heshima, lakini mumeo aliyekuzidi miaka 40 hauko tayari kumwamkia, au yule anayeombwa cadema anaamini amedharauliwa, hivi heshima ya mwanamke iko kwenye chadema? Mbona wanawake mnajidhalilisha? Kwani ni kibaya kipi kutembeleana, mie nilidhani mungezidisha kuheshimiana kwa kuwa hata vilivyofichika - nyeti mmepeana na kwa hiyo mnajuana kwa kina zaidi? Si ni wasiri ninyi? Jamani, sasa utampaje mtu chadema yako asipokuomba? Mbona msipoombwa muda mrefu mnaenda Bagamoyo na Ujiji kusafisha nyota?
Ni utovu wa nidhamu kumnyima haki ya kuamkiwa mtu yeyote ati tu sababu unakula mhogo wake. Heshima ya mwanamke iko moyoni mwake na sio hapo ambapo Terry alishasema hakijai hata kenye kiganja cha mkono. Amkeni na mjijue position ya heshima zenu wanawake! Mumeo atajisikia vizuri sana ukimwamkia kwa sababu ni dalili mojawapo ya submission kwake.