Hivi ni sahihi kumutafuta mzazi wako aliyekutelekeza utotoni?

Hivi ni sahihi kumutafuta mzazi wako aliyekutelekeza utotoni?

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Ni sahihi kabisa kumtafuta mzazi wako aliyekutelekeza utotoni, ingawa uamuzi huu ni unaweza kuchukuliwa kama ubnafsi na unategemea mambo mengi.

Watu wengi huchagua kuwatafuta wazazi walio watelekeza kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutaka kufaham historia yao ya kifamilia, kupata majibu kuhusu kwa nini waliachwa, na mambo mengine ambayo yanasibu famila

Vipi wewe Mwanabodi una mtizamo gani kuhusiana na jambo hilo
 
Ukimtafuta mzazi "uliyeambiwa" alikutelekeza fanya yafuatayo:
1. Usimuulize kwani "alikutelekeza"
2. Usitake umjue kwa undani kwa siku moja
3. Usimuombe hela isipokuwa ushauri tu
4. Usimwangalie kwa jicho la kumchunguza na usionyeshe kumshangaa kwa hali utakayomkuta nayo
5. Usimweleze uliyopitia alivyokuwa mbali
6. Usimweleze madhaifu ya mzazi uliyekuwa nae
7. Mwambie unashukuru kumfahamu na kama una chochote mwachie na endelea kuwa na mawasiliano nae
NB
Unahitaji kuwa mvumilivu ipo siku utajua nini kilitokea hadi akaingia mitini. Kuwa tayari kusamehe kwa pande zote mbili ili maisha yaendelee salama kwa faida yako
 
Mzazi ni Mzazi tu mkuu, hata kama una kinyongo naye hakikisha mama ako halali njaa mpaka mwisho wa uhai wake.

Angekuwa na nia mbaya na wewe angekuua Mapema sana ukiwa bado upo tumboni 🙏🙏🙏🙏
 
Kutelekeza kuna mambo mengi usione ulitelekezwa sababu hasa ni wamama kuwatibua wanaume ,matusi dharau hivo kumutafuta baba au mama ndio unapata ukweli nini tatizo sio ww unasikiliza upande mmoja na kutoa hukumu ni ujinga usio mfano baba atakueleza tatizo la mamako lilivyo kuwa hivo usihukumu
English people say No research no right to say
 
Cha ajabu inatokeaga mzazi akipatikana kachokaaa yani kajichokea hadi mtoto anaishiwa nguvu.
Siku nikipata tetesi kua mshua ana kibunda ndo nitamtafuta.

Haya mambo ya kumtafuta halafu ukute ni apeche zaidi yako, una wadogo zako kibao nao apeche.
Gafla bin vuu unageuka tegemezi 😂😂
 
Yani moyo hauwezi kutulia mpaka umfahamu mzazi wako. Vilevile mzazi nae Kuna jambo linakuwa linamfukuta moyoni japo hawezi kusema. Hii ni Sheria ya asili ya mwanadamu. Kutaka kujua alitokea wapi
 
Watu mnajustify upuuzi sana
Hakuna sababu ya mzazi kumtelekeza mtoto,kwa mazingira yoyote mzazi alitakiwa aweke effort kuwepo kwa mwanae kwa namna moja au nyingine.
Hakuna haja ya mtoto kumtafuta mzazi ni jukumu la mzazi kumtafuta mtoto wake
 
Kutelekeza kuna mambo mengi usione ulitelekezwa sababu hasa ni wamama kuwatibua wanaume ,matusi dharau hivo kumutafuta baba au mama ndio unapata ukweli nini tatizo sio ww unasikiliza upande mmoja na kutoa hukumu ni ujinga usio mfano baba atakueleza tatizo la mamako lilivyo kuwa hivo usihukumu
English people say No research no right to say
Hoja sio kujua tatizo la mama, hoja ni baba kumtelekeza mtoto.

Huu upumbavu wa baba kupotea alafu mtoto akikua akawa Ommy Dimpoz, baba anatoka kuendesha bajaj uko anakuja na kisingizio cha "huwezi jua mama yako alinifanyia nini" ni ushenzi.

Mtoto akikua akawa Diamond ndio baba anatupa mitumba huko anakuja mbiombio kutia huruma na kudai ni damu yake, ila mtoto huyohuyo akiwa muuza makopo huwezi sikia baba anamlilia akimlaumu mama mtoto kwa mabaya aliyomfanyia mpaka akakimbia mtoto.

Ukikosana na mama mtoto si ulikimbia ukamuacha mtoto wako na hujawahi lipa ada, kujua anakula nini, analala wapi na anasomaje, sasa imekuaje akiwa maarufu ghafla unajua anaishi wapi, anamiliki nini na anafanya nini?

Kama ambavyo hujaambiwa na mtu na hakuna namna ungewezwa fichwa hizo taarifa, vilevile na alipokuwa mdogo hukutakiwa kuambiwa na mtu wala kufichwa taarifa.
 
Ni excuses za kipuuzi za kina baba wazembe tu.

Hata mkiwa na mtafaruku na mkeo, so rahisi kwa baba bora kutojua mwane yuko wapi na anafanya nini huko, sio baada ya miaka 30 ndo anajitokeza yeye akiwa apeche akitegemea mtoto aliemtelekez amsaidie.
 
Wewe kuna problem nyie hamuna maturity hakuna kina mama wanaficha watoto na kuwaambia baba yenu ni mbaya? Ujue yako mazingira ya namuna hiyo
Pia mkeo anaweza kukuambia ukileta mtoto atakufa sasa mazingira hayo utamuonyesha ?iko he kima pia ya kuficha jambo
 
Yani moyo hauwezi kutulia mpaka umfahamu mzazi wako. Vilevile mzazi nae Kuna jambo linakuwa linamfukuta moyoni japo hawezi kusema. Hii ni Sheria ya asili ya mwanadamu. Kutaka kujua alitokea wapi
Mzazi aliyetelekeza mtoto haumii ukiwa kapuku, au mlevi usiye na lolote.
Mzazi yeye kwenye hesabu zake haupo, anakuwa anategemea sababu alikuacha kwenye shida you will be nobody.

Baadae ukifanikiwa anakuwa chawa wako, wala hawezi kukupenda unajidanganya tu. Haiwezekani mzazi akupende ukiwa na miaka 35 wakati tangu ukiwa hujui kuongea hajawahi kukupenda. Mzazi huwa anapenda mtoto mdogo kuliko mkubwa, ndio maana last borns wanapendwa zaidi ya kaka na dada zao.

Msanii Kanumba ninajuana na upande wa mama yake. Kanumba alipokuwa maarufu baba yake uko sijui Shinyanga akaanza kusumbua anataka apewe gari mara apewe hela nyingi kama anavyopewa mama yake (aasumptions).
Wakati kiuhalisia Kanumba hakuwa na hela kivile, ila mzee kwa sababu hana ukaribu nae sana wa kuweza kufunguka in and out anamuona kwenye TV basi akajua anachoona kwa TV, kusoma skendo magazetini na ile lifestyle ya msanii kwenye udaku ndio maisha halisi hivyo akawa analeta chuki kwa mama Kanumba kuwa anamzuia mtoto, mara amemlisha sumu.

Mama Kanumba mwenyewe alidhani mwanae ana hela, ila alipofariki ndio akaambiwa uhalisia. Sasa imagine mama maisha yake yote alikuwa anadhani mwanae ana hela ila haweki demands kubwa. Ila baba yuko uko anadai tu. Tulijua kabisa baba mtu hampendi mwanae na kuna muda alitoa kauli mbaya na hata kwenye kifo hakusikitika habari zake ziliishia hapo.
 
  • Thanks
Reactions: x x
Mama yako aliekulisha sumu usimuamini sana mtafute Baba yako akwambie ukweli.
 
Wewe kuna problem nyie hamuna maturity hakuna kina mama wanaficha watoto na kuwaambia baba yenu ni mbaya? Ujue yako mazingira ya namuna hiyo
Pia mkeo anaweza kukuambia ukileta mtoto atakufa sasa mazingira hayo utamuonyesha ?iko he kima pia ya kuficha jambo
Hapa bongo kati ya watu maarufu waliotelekezwa na wazazi wao, taja mmoja ambaye alifichwa na mama yake.

Ni Mwana FA?
Diamond?
Ommy Dimpoz?

Mzee Nyembo nasikia alizalisha wanawake kama tisa hivi, mwanzoni kabla mwanae hajasisitiza kwa mkazo kuwa hataki mazoea alikuwa anajitambulisha kama "babake Omny Dimpoz" alitelekeza na jina kabisa. Kwanini asiende kulilia wanae wengine ambao lets say ni bodaboda au wakata kuni?

Mzee Abdul kwanini aliacha mitumba uko na mademu zake, akaja kuimba dudu la yuyu na kumlilia Diamond.

Aliyekukataa mkatae, jamii itakuwa ya kipumbavu sana tukilea ujinga. Ninayo majamaa zangu kama mashoga unasikia eti "nilizalisha mtoto analelewa na mama yake". Haya mang'ombe baadae najua yatasema "huwezi jua mama yako alinifanya nini".
 
Ukimtafuta mzazi "uliyeambiwa" alikutelekeza fanya yafuatayo:
1. Usimuulize kwani "alikutelekeza"
2. Usitake umjue kwa undani kwa siku moja
3. Usimuombe hela isipokuwa ushauri tu
4. Usimwangalie kwa jicho la kumchunguza na usionyeshe kumshangaa kwa hali utakayomkuta nayo
5. Usimweleze uliyopitia alivyokuwa mbali
6. Usimweleze madhaifu ya mzazi uliyekuwa nae
7. Mwambie unashukuru kumfahamu na kama una chochote mwachie na endelea kuwa na mawasiliano nae
NB
Unahitaji kuwa mvumilivu ipo siku utajua nini kilitokea hadi akaingia mitini. Kuwa tayari kusamehe kwa pande zote mbili ili maisha yaendelee salama kwa faida yako
Nakazia na mzazi atabaki kuwa mzazi tu.
 
Back
Top Bottom