Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Ukimtafuta mzazi "uliyeambiwa" alikutelekeza fanya yafuatayo:Ni sahihi kabisa kumtafuta mzazi wako aliyekutelekeza utotoni, ingawa uamuzi huu ni unaweza kuchukuliwa kama ubnafsi na unategemea mambo mengi.
Watu wengi huchagua kuwatafuta wazazi walio watelekeza kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutaka kufaham historia yao ya kifamilia, kupata majibu kuhusu kwa nini waliachwa, na mambo mengine ambayo yanasibu famila
Vipi wewe Mwanabodi una mtizamo gani kuhusiana na jambo hilo
Siku nikipata tetesi kua mshua ana kibunda ndo nitamtafuta.Cha ajabu inatokeaga mzazi akipatikana kachokaaa yani kajichokea hadi mtoto anaishiwa nguvu.
Hoja sio kujua tatizo la mama, hoja ni baba kumtelekeza mtoto.Kutelekeza kuna mambo mengi usione ulitelekezwa sababu hasa ni wamama kuwatibua wanaume ,matusi dharau hivo kumutafuta baba au mama ndio unapata ukweli nini tatizo sio ww unasikiliza upande mmoja na kutoa hukumu ni ujinga usio mfano baba atakueleza tatizo la mamako lilivyo kuwa hivo usihukumu
English people say No research no right to say
Ni excuses za kipuuzi za kina baba wazembe tu.Hoja sio kujua tatizo la mama, hoja ni baba kumtelekeza mtoto.
Huu upumbavu wa baba kupotea alafu mtoto akikua akawa Ommy Dimpoz, baba anatoka kuendesha bajaj uko anakuja na kisingizio cha "huwezi jua mama yako alinifanyia nini" ni ushenzi.
Mtoto akikua akawa Diamond ndio baba anatupa mitumba huko anakuja mbiombio kutia huruma na kudai ni damu yake, ila mtoto huyohuyo akiwa muuza makopo huwezi sikia baba anamlilia akimlaumu mama mtoto kwa mabaya aliyomfanyia mpaka akakimbia mtoto.
Ukikosana na mama mtoto si ulikimbia ukamuacha mtoto wako na hujawahi lipa ada, kujua anakula nini, analala wapi na anasomaje, sasa imekuaje akiwa maarufu ghafla unajua anaishi wapi, anamiliki nini na anafanya nini?
Kama ambavyo hujaambiwa na mtu na hakuna namna ungewezwa fichwa hizo taarifa, vilevile na alipokuwa mdogo hukutakiwa kuambiwa na mtu wala kufichwa taarifa.
Mzazi aliyetelekeza mtoto haumii ukiwa kapuku, au mlevi usiye na lolote.Yani moyo hauwezi kutulia mpaka umfahamu mzazi wako. Vilevile mzazi nae Kuna jambo linakuwa linamfukuta moyoni japo hawezi kusema. Hii ni Sheria ya asili ya mwanadamu. Kutaka kujua alitokea wapi
Hapa bongo kati ya watu maarufu waliotelekezwa na wazazi wao, taja mmoja ambaye alifichwa na mama yake.Wewe kuna problem nyie hamuna maturity hakuna kina mama wanaficha watoto na kuwaambia baba yenu ni mbaya? Ujue yako mazingira ya namuna hiyo
Pia mkeo anaweza kukuambia ukileta mtoto atakufa sasa mazingira hayo utamuonyesha ?iko he kima pia ya kuficha jambo
Nakazia na mzazi atabaki kuwa mzazi tu.Ukimtafuta mzazi "uliyeambiwa" alikutelekeza fanya yafuatayo:
1. Usimuulize kwani "alikutelekeza"
2. Usitake umjue kwa undani kwa siku moja
3. Usimuombe hela isipokuwa ushauri tu
4. Usimwangalie kwa jicho la kumchunguza na usionyeshe kumshangaa kwa hali utakayomkuta nayo
5. Usimweleze uliyopitia alivyokuwa mbali
6. Usimweleze madhaifu ya mzazi uliyekuwa nae
7. Mwambie unashukuru kumfahamu na kama una chochote mwachie na endelea kuwa na mawasiliano nae
NB
Unahitaji kuwa mvumilivu ipo siku utajua nini kilitokea hadi akaingia mitini. Kuwa tayari kusamehe kwa pande zote mbili ili maisha yaendelee salama kwa faida yako