KERO Hivi ni sahihi Wanafunzi wa shule ya msingi kwenda shule saa 12 asubuhi mpaka 12 jioni?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Kuna tabia inakomaa ya wanafunzi hasa kwa Dar kwenda shule saa 12 asubuhi na kutoka 12 jioni, awali tabia hii ilikuwa kwa shule za kulipia za watu binafsi ikawa inapigiwa kelele ila sasa naona hata za Serikali zinafanya hivyo.

Wengi wanaweka sababu kuwa wanawaandaa watoto kwa mitihani ya Taifa, swali langi ni je, Wizara ya elimu imeruhusu muda huo au ni matakwa ya shule fulani fulani tu?

Katika mazingira hayo hayo kwa shule za Serikali wapo wazazi wasioweza kulipia chakula kila siku kwa ajili ya watoto kwenye huo mpango wa wazazi kuchangia watoto wale shule hivyo inamlazimu mtoto kushinda njaa siku nzima mpaka 12 jioni na kama anakaa mbali kidogo hadi afike nyumbani ni saa moja!

Ina maana elimu ya msingi imekuwa ngumu kiasi hicho mpaka watoto washinde shule kutwa nzima na hata siku ya Jumamosi wanalazimishwa kwenda kwa masaa hayo hayo.

Kwa upande wangu naona kuna tatizo ambalo inabidi Wizara iliangalie ili watoto waone kusoma siyo adhabu ukizingatia wanarudi usiku na mzigo mzigo wa begi la madaftari mengi sana mpaka wanafika wanaomba kunyooshwa mabega kwa maumivu ya kubeba kaunta zaidi ya 12 kila siku na kushindwa shule kutwa nzima mpaka usiku.

1772549442457.png

​
 
Nimemaliza la saba mwaka 2005.

Madarasa ya mitihani kama la 4 na 7 walikuwa wanaanza kusoma saa 12 asbh, siyo kufika! Hapana! Yani saa 12 kamili mwalimu yuko darasani.

Na kwa wale vichwa walimu wakatufanyia mpango tukawa tunajisomea mpaka usiku.

Sasa mkuu wewe kinachokushangaza ni nini? Tuwaache walimu wafanye kazi zao kwa uhuru!

Wewe kama hautaki, basi nenda shule kajicommit kimaandishi ili mwanao awe anaenda shule muda unaotaka wewe.
 
Hata mm pia hili liliwah kunisikitisha, nilipopata stor moja, kuna mzazi alishindwa kumudu gharama za chakula, ikabid mtoto awe anakomaa asubh had jioni, inasikitisha sana. Na hiyo c Dar tu ni mashule mengi hata mikoan pia.
 
Nimemaliza la saba mwaka 2005.

Madarasa ya mitihani kama la 4 na 7 walikuwa wanaanza kusoma saa 12 asbh, siyo kufika! Hapana! Yani saa 12 kamili mwalimu yuko darasani.

Na kwa wale vichwa walimu wakatufanyia mpango tukawa tunajisomea mpaka usiku.

Sasa mkuu wewe kinachokushangaza ni nini? Tuwaache walimu wafanye kazi zao kwa uhuru!

Wewe kama hautaki, basi nenda shule kajicommit kimaandishi ili mwanao awe anaenda shule muda unaotaka wewe.
Kua kwanza ndio uchangie mada
 
Samahani wewe mleta thread umetumwa na MUNGU kuniletea hii thread hujui tu.

If GOD wishes nitarudi December kukupa confirmation ya hiki nachosema.
 
I believe nimesoma one of the best schools in Dar es Salaam. Masomo always kuanzia saa 2, Sikumbuki kukaa shule past saa 9! Naongelea form 4.

Sanasana kilichoongezeka ni Muda mwingine walimu wa Maths na Physicis wanatuita tuje jumamosi, mwisho saa 6.

Nashangaa watoto wa primary wanatoka shule saa 11! Jumamosi wanatoka saa 9! Au ndo mtaala mpya! ! !

Kwanini mtoto wa Primary aende shule jumamosi??
 
Sisi tuliosoma zamani tena shule za kidumu na fagio, ilikuwa tunaanza masomo saa 1:30 asubuhi hadi 9:30 mchana

Baada ya hapo, ni kurudi nyumbani kwaajili ya chakula cha mchana

Miaka hii shule nyingi wana utaratibu wa kula shuleni

Kwahiyo watoto wanapata muda mzuri kujifunza pamoja na mazoezi

Upande wa DSM, nafikiri wangeona uwezekano wa kuwa na hiyo ratiba ya kutoka saa 9:30 jioni

Unapomtoa mtoto saa 12 jioni, kwa changamoto ya usafiri iliyopo hapo mjini, mtoto atajikuta anafika nyumbani saa 4 usiku

Muda ambao, kwa mtoto wa Kijijini anakuwa ameshalala usingizi
 
Kuna tabia inakomaa ya wanafunzi hasa kwa Dar kwenda shule saa 12 asubuhi na kutoka 12 jioni, awali tabia hii ilikuwa kwa shule za kulipia za watu binafsi ikawa inapigiwa kelele ila sasa naona hata za Serikali zinafanya hivyo.

Wengi wanaweka sababu kuwa wanawaandaa watoto kwa mitihani ya Taifa, swali langi ni je, Wizara ya elimu imeruhusu muda huo au ni matakwa ya shule fulani fulani tu?

Katika mazingira hayo hayo kwa shule za Serikali wapo wazazi wasioweza kulipia chakula kila siku kwa ajili ya watoto kwenye huo mpango wa wazazi kuchangia watoto wale shule hivyo inamlazimu mtoto kushinda njaa siku nzima mpaka 12 jioni na kama anakaa mbali kidogo hadi afike nyumbani ni saa moja!

Ina maana elimu ya msingi imekuwa ngumu kiasi hicho mpaka watoto washinde shule kutwa nzima na hata siku ya Jumamosi wanalazimishwa kwenda kwa masaa hayo hayo.

Kwa upande wangu naona kuna tatizo ambalo inabidi Wizara iliangalie ili watoto waone kusoma siyo adhabu ukizingatia wanarudi usiku na mzigo mzigo wa begi la madaftari mengi sana mpaka wanafika wanaomba kunyooshwa mabega kwa maumivu ya kubeba kaunta zaidi ya 12 kila siku na kushindwa shule kutwa nzima mpaka usiku.
Wa kwangu anaenda saa 12 mpaka saa 4 usiku, darasa la saba.
 
Nilivyosoma jina lako haraka haraka nikajua mafwele. Vipi wakati wewe unasoma shule ya msingi hali ilikuwaje?
 
Nimemaliza la saba mwaka 2005.

Madarasa ya mitihani kama la 4 na 7 walikuwa wanaanza kusoma saa 12 asbh, siyo kufika! Hapana! Yani saa 12 kamili mwalimu yuko darasani.

Na kwa wale vichwa walimu wakatufanyia mpango tukawa tunajisomea mpaka usiku.

Sasa mkuu wewe kinachokushangaza ni nini? Tuwaache walimu wafanye kazi zao kwa uhuru!

Wewe kama hautaki, basi nenda shule kajicommit kimaandishi ili mwanao awe anaenda shule muda unaotaka wewe.
Miaka hiyo mlikua mnaanza shule mijitu mizima, mshabalehe,
Watoto wa siku hizi wanaanza shule wadogo sana kuwashindisha masaa yote hayo ni uonevu na kufanya mtoto asiipende shule.
 
Kuna tabia inakomaa ya wanafunzi hasa kwa Dar kwenda shule saa 12 asubuhi na kutoka 12 jioni, awali tabia hii ilikuwa kwa shule za kulipia za watu binafsi ikawa inapigiwa kelele ila sasa naona hata za Serikali zinafanya hivyo.

Wengi wanaweka sababu kuwa wanawaandaa watoto kwa mitihani ya Taifa, swali langi ni je, Wizara ya elimu imeruhusu muda huo au ni matakwa ya shule fulani fulani tu?

Katika mazingira hayo hayo kwa shule za Serikali wapo wazazi wasioweza kulipia chakula kila siku kwa ajili ya watoto kwenye huo mpango wa wazazi kuchangia watoto wale shule hivyo inamlazimu mtoto kushinda njaa siku nzima mpaka 12 jioni na kama anakaa mbali kidogo hadi afike nyumbani ni saa moja!

Ina maana elimu ya msingi imekuwa ngumu kiasi hicho mpaka watoto washinde shule kutwa nzima na hata siku ya Jumamosi wanalazimishwa kwenda kwa masaa hayo hayo.

Kwa upande wangu naona kuna tatizo ambalo inabidi Wizara iliangalie ili watoto waone kusoma siyo adhabu ukizingatia wanarudi usiku na mzigo mzigo wa begi la madaftari mengi sana mpaka wanafika wanaomba kunyooshwa mabega kwa maumivu ya kubeba kaunta zaidi ya 12 kila siku na kushindwa shule kutwa nzima mpaka usiku.
na jumamosi ni amri waende,Tena na buku buku za walimu
 
Miaka hiyo mlikua mnaanza shule mijitu mizima, mshabalehe,
Watoto wa siku hizi wanaanza shule wadogo sana kuwashindisha masaa yote hayo ni uonevu na kufanya mtoto asiipende shule.
Ilaumiwe formula iliyokuwa inatumika ya sifa ya kujiunga darasa la kwanza, ni lazima uwe na uwezo wa kushika sikio 😅🙌

Mwanafunzi anafika darasa la VII, ameota ndevu kabisa na anajua kutumia Viwembe vyote 🙌

Nina rafiki yangu, wakati tunaanza kidato cha kwanza alikuwa ameacha mke nyumbani kwao mwenye mtoto wa miezi kadhaa 🙌

Miaka hii, mtoto anafika darasa la VII ana miaka 11, anamaliza kidato cha IV ana miaka 15 🙌

Hata kutongoza hajajua
 
Ilaumiwe formula iliyokuwa inatumika ya sifa ya kujiunga darasa la kwanza, ni lazima uwe na uwezo wa kushika sikio 😅🙌

Mwanafunzi anafika darasa la VII, ameota ndevu kabisa na anajua kutumia Viwembe vyote 🙌

Nina rafiki yangu, wakati tunaanza kidato cha kwanza alikuwa ameacha mke nyumbani kwao mwenye mtoto wa miezi kadhaa 🙌

Miaka hii, mtoto anafika darasa la VII ama miaka 11, anamaliza kidato cha IV ana miaka 15 🙌

Hata kutongoza hajajua
Noma sana mkuu nimesoma watu wana ndevu zimekomaa balaa😅
 
Back
Top Bottom