KERO Hivi ni sahihi Wanafunzi wa shule ya msingi kwenda shule saa 12 asubuhi mpaka 12 jioni?

KERO Hivi ni sahihi Wanafunzi wa shule ya msingi kwenda shule saa 12 asubuhi mpaka 12 jioni?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Noma sana mkuu nimesoma watu wana ndevu zimekomaa balaa😅
Hao waliokuwa na ndevu mkiwa mnasoma nao, huenda walipitia hiyo njia ya kushika sikio 😅

Kwa huu mtaala mpya, watoto wanaishia darasa la VI, watajikuta mtoto anamaliza darasa la VI akiwa na miaka 10 tu

Hata kusema apewe masomo ya kujiajiri inakuwa ni kumuonea
 
Ilaumiwe formula iliyokuwa inatumika ya sifa ya kujiunga darasa la kwanza, ni lazima uwe na uwezo wa kushika sikio 😅🙌

Mwanafunzi anafika darasa la VII, ameota ndevu kabisa na anajua kutumia Viwembe vyote 🙌

Nina rafiki yangu, wakati tunaanza kidato cha kwanza alikuwa ameacha mke nyumbani kwao mwenye mtoto wa miezi kadhaa 🙌

Miaka hii, mtoto anafika darasa la VII ana miaka 11, anamaliza kidato cha IV ana miaka 15 🙌

Hata kutongoza hajajua
Uko sahihi babu, hata mie ilibaki kidogo tu wanibakishe home, nilifeli zoezi la kushika sikio, kilichoniokoa nilikua najua kusoma na kuandika tayari na connection iliyokuwepo kati ya baba na mkuu wa shule,

Lakini tulisoma na mibaba ina ndevu mkitoka mchaka mchaka darasa zima linanuka vikwapa🤢 wengine wamama namkumbuka rafiki yangu Teresia alikua mmama maziwa hayooo wanafunzi wengi walimcheka na kumtenga lakini mimi, Winifrida, Magdalena na Consolata tukawa marafiki zake,

Sekondari tulisoma na Zahra alikua mke wa mtu mwenye mtoto wa miezi 6, break time alikimbia kunyonyesha, hakua anaishi mbali na shule.
 
Walimu lazima wapate chochote kitu
 
Nimemaliza la saba mwaka 2005.

Madarasa ya mitihani kama la 4 na 7 walikuwa wanaanza kusoma saa 12 asbh, siyo kufika! Hapana! Yani saa 12 kamili mwalimu yuko darasani.

Na kwa wale vichwa walimu wakatufanyia mpango tukawa tunajisomea mpaka usiku.

Sasa mkuu wewe kinachokushangaza ni nini? Tuwaache walimu wafanye kazi zao kwa uhuru!

Wewe kama hautaki, basi nenda shule kajicommit kimaandishi ili mwanao awe anaenda shule muda unaotaka wewe.
Tatizo kuwepo kizazi kilichopita sio uhalali wa tatizo hilo kudumu milele. 12 asubuhi mpaka 12 jioni hao watoto wanasoma nini.! Ungefanya cha maana kama ungesdma faida maalumu za watoto kuwepo shuleni muda wote huo, sio kuhalalisha tu kwa sababu na wewe umeishi maisha hayo.
 
Yani hili bandiko limenigusa sana,nimekuwa najiuliza hivyo hivyo je elimu ya msingi imekuwa ngumu kiasi hicho

Huwa nakutana na vitoto vidogo saa 11 na nusu asubuh eti wanaenda shule,yani giza mpaka unajiulia vikibakwa je? Juzi nilikutana na kimoja nikakiuliza hivi mida hii ya giza shuleni kwenu kuna taa?

Jamani viongozi na wahusika,hii kweli ni sawa? Yani watoto sasa hivi wanapambania elimu ya msingi katika mazingira magumu kiasi hiki? Wanatoka jioni sana wanafika nyumbani usiku kweli ni sawa kwa umri wao?

Kuna wengine wa secondary nimewaona maeneo ya kariakoo nadhani itawakuwa pale Benjamini mkapa wanatoka shule saa 2 usiku, halafu hapo bado hawajapanda daladala kwa tabu,je wanafika nyumbani saa ngapi?

Ebu muwaonee huruma hawa vijana wadogo, hawastahili hizo changamoto
 
Kuna tabia inakomaa ya wanafunzi hasa kwa Dar kwenda shule saa 12 asubuhi na kutoka 12 jioni, awali tabia hii ilikuwa kwa shule za kulipia za watu binafsi ikawa inapigiwa kelele ila sasa naona hata za Serikali zinafanya hivyo.

Wengi wanaweka sababu kuwa wanawaandaa watoto kwa mitihani ya Taifa, swali langi ni je, Wizara ya elimu imeruhusu muda huo au ni matakwa ya shule fulani fulani tu?

Katika mazingira hayo hayo kwa shule za Serikali wapo wazazi wasioweza kulipia chakula kila siku kwa ajili ya watoto kwenye huo mpango wa wazazi kuchangia watoto wale shule hivyo inamlazimu mtoto kushinda njaa siku nzima mpaka 12 jioni na kama anakaa mbali kidogo hadi afike nyumbani ni saa moja!

Ina maana elimu ya msingi imekuwa ngumu kiasi hicho mpaka watoto washinde shule kutwa nzima na hata siku ya Jumamosi wanalazimishwa kwenda kwa masaa hayo hayo.

Kwa upande wangu naona kuna tatizo ambalo inabidi Wizara iliangalie ili watoto waone kusoma siyo adhabu ukizingatia wanarudi usiku na mzigo mzigo wa begi la madaftari mengi sana mpaka wanafika wanaomba kunyooshwa mabega kwa maumivu ya kubeba kaunta zaidi ya 12 kila siku na kushindwa shule kutwa nzima mpaka usiku.
Haya mambo yalikataliwa na mbunge KISHIMBA..
 
Na unaona ni sawa? saa 4 usiku alooo nasubiri nifikie muda wa kusomesha nitakua mzazi mtata sana😂😂
Inaniudhi sana, tatizo wazazi wengi ni kufuata mkumbo, shule inalazimisha wasome mpaka saa 4 usiku, Ukikataa wengine wanawaacha watoto wao unabaki peke yako. Bora amalize tu niachane na huu ujinga.
 
Uko sahihi babu, hata mie ilibaki kidogo tu wanibakishe home, nilifeli zoezi la kushika sikio, kilichoniokoa nilikua najua kusoma na kuandika tayari na connection iliyokuwepo kati ya baba na mkuu wa shule,

Lakini tulisoma na mibaba ina ndevu mkitoka mchaka mchaka darasa zima linanuka vikwapa🤢 wengine wamama namkumbuka rafiki yangu Teresia alikua mmama maziwa hayooo wanafunzi wengi walimcheka na kumtenga lakini mimi, Winifrida, Magdalena na Consolata tukawa marafiki zake,

Sekondari tulisoma na Zahra alikua mke wa mtu mwenye mtoto wa miezi 6, break time alikimbia kunyonyesha, hakua anaishi mbali na shule.
Una bahati ulisoma ukiwa underaged

Changamoto za kusoma ukiwa Mkubwa, unakuta unaanza michezo mibaya ukiwa bado shuleni

Ndiyo unapata zile kesi, mwanafunzi wa darasa la V ampa mimba Mwalimu wake 🙌

Huyo rafiki yako Zahra aliwezaje kusoma huku ananyonyesha?

Sisi mwaka 47, ilikuwa tunahitimu shule ya msingi tukiwa na miaka 20 hadi 25 🤪
 
Tunaishi katika zama ambazo Afisa elim anafokewa,mratibu anafokewa,mwalimu mkuu anafokewa,mwalimu wa SoMo anafokewa!kwamba kusiwe na zero!

Kifupi ni kwamba ,hakuna elim siku hizi Bali ufaulu ndio umefanywa elimu,yaani watoto wanaandaliwa kufaulu mitihani na sio kufaulu maisha!!

Kwenye jamii Kuna aina zote za watu wenye vipaji tofauti huwezi lazimisha wote wapate A kwenye mitihani badala wapate A kwenye kujamiiana na nature Ili kupata kilicho Bora zaidi!

Plato Ali group watu katika makundi matatu,na mtihani halisi lazima wawepo watakaopata zero ,hiyo no lazima kwa Maana halisi ya mtihani!mashindano ya kufaulisha sio muktadha halisi was elim Bali data za majukwaani!!

Watoto wanaandaliwa kufaulu makaratasi kuliko kujamiiana na asili nature!matokeo yake tunaandaa maroboti yatakayokufa Kwa msongo wa mawazo coz hayana uwezo wa kupambana na mitihani ya asili katika mazingira halisi!!

Cases za kujiua zitaongezeka zaidi Kwa wasomi coz elim wanayoipata Haina tija kwenye kujamiiana na asili,hawatakua na uwezo wa ku handle nature!!

TULIOSOMA ZAMANI ENZI ZA VIBUYU VYA MAJI,TUKIBEBA MABOGA,MAHINDI,KARANGA ZA KUCHEMSHWA NA N.K TULIINJOY SANA NA SASA TUMESHIKA DOLA TUKIWA NA SULUHISHO LA HARAKA LA KILA HALI INAYOTUPATA KWENYE MAISHA,TUNAHESHIMU
 
Kuna tabia inakomaa ya wanafunzi hasa kwa Dar kwenda shule saa 12 asubuhi na kutoka 12 jioni, awali tabia hii ilikuwa kwa shule za kulipia za watu binafsi ikawa inapigiwa kelele ila sasa naona hata za Serikali zinafanya hivyo.

Wengi wanaweka sababu kuwa wanawaandaa watoto kwa mitihani ya Taifa, swali langi ni je, Wizara ya elimu imeruhusu muda huo au ni matakwa ya shule fulani fulani tu?

Katika mazingira hayo hayo kwa shule za Serikali wapo wazazi wasioweza kulipia chakula kila siku kwa ajili ya watoto kwenye huo mpango wa wazazi kuchangia watoto wale shule hivyo inamlazimu mtoto kushinda njaa siku nzima mpaka 12 jioni na kama anakaa mbali kidogo hadi afike nyumbani ni saa moja!

Ina maana elimu ya msingi imekuwa ngumu kiasi hicho mpaka watoto washinde shule kutwa nzima na hata siku ya Jumamosi wanalazimishwa kwenda kwa masaa hayo hayo.

Kwa upande wangu naona kuna tatizo ambalo inabidi Wizara iliangalie ili watoto waone kusoma siyo adhabu ukizingatia wanarudi usiku na mzigo mzigo wa begi la madaftari mengi sana mpaka wanafika wanaomba kunyooshwa mabega kwa maumivu ya kubeba kaunta zaidi ya 12 kila siku na kushindwa shule kutwa nzima mpaka usiku.

Siyo sahihi hata kidogo tatizo ni Serikali kupmbavu ya ccm ....hata jumamosi na jumapili ni kosa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwenda shule ....shule aitakiwi kuwa mateso kwa watoto.
 
Sio sahihi bali uchaguzi wa wazazi kuchagua shule za mbali ni sababu mojawapo. Pia ratiba za shule zinawabana watoto haswa wenye ufaulu mdogo kuunganisha na tuition baada ya masaa ya kawaida ya masomo.
 
Na unaona ni sawa? saa 4 usiku alooo nasubiri nifikie muda wa kusomesha nitakua mzazi mtata sana😂😂
From an experienced to a future mzazi mtata, muda ukifika kazia hapo hapo maana kumlazimishia mtoto kitabu asubuhi mpaka usiku ni kumtesa tu, wala haiwasadii zaidi ya kukariri vitu.

Wangu alivyoingia Class 4 nilikataa boarding (never been a fan), nikaambiwa basi lazima umlete asubuhi mapema na achukuliwe saa mbili usiku ili ratiba yake ya masomo isivurugike. Nikamwambia mwalimu, dogo atakuja kwa school bus, na atarudi nalo nyumbani kama ilivyokua mwanzo. Swala la kufeli niachie mimi kama mzazi.

Nyumbani akawa anapimzika zake na mwisho wa siku bado akaondoka zake na A 😏
 
Back
Top Bottom