KERO Hivi ni sahihi Wanafunzi wa shule ya msingi kwenda shule saa 12 asubuhi mpaka 12 jioni?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Noma sana mkuu nimesoma watu wana ndevu zimekomaa balaa😅
Hao waliokuwa na ndevu mkiwa mnasoma nao, huenda walipitia hiyo njia ya kushika sikio 😅

Kwa huu mtaala mpya, watoto wanaishia darasa la VI, watajikuta mtoto anamaliza darasa la VI akiwa na miaka 10 tu

Hata kusema apewe masomo ya kujiajiri inakuwa ni kumuonea
 
Uko sahihi babu, hata mie ilibaki kidogo tu wanibakishe home, nilifeli zoezi la kushika sikio, kilichoniokoa nilikua najua kusoma na kuandika tayari na connection iliyokuwepo kati ya baba na mkuu wa shule,

Lakini tulisoma na mibaba ina ndevu mkitoka mchaka mchaka darasa zima linanuka vikwapa🤢 wengine wamama namkumbuka rafiki yangu Teresia alikua mmama maziwa hayooo wanafunzi wengi walimcheka na kumtenga lakini mimi, Winifrida, Magdalena na Consolata tukawa marafiki zake,

Sekondari tulisoma na Zahra alikua mke wa mtu mwenye mtoto wa miezi 6, break time alikimbia kunyonyesha, hakua anaishi mbali na shule.
 
Walimu lazima wapate chochote kitu
 
Tatizo kuwepo kizazi kilichopita sio uhalali wa tatizo hilo kudumu milele. 12 asubuhi mpaka 12 jioni hao watoto wanasoma nini.! Ungefanya cha maana kama ungesdma faida maalumu za watoto kuwepo shuleni muda wote huo, sio kuhalalisha tu kwa sababu na wewe umeishi maisha hayo.
 
Yani hili bandiko limenigusa sana,nimekuwa najiuliza hivyo hivyo je elimu ya msingi imekuwa ngumu kiasi hicho

Huwa nakutana na vitoto vidogo saa 11 na nusu asubuh eti wanaenda shule,yani giza mpaka unajiulia vikibakwa je? Juzi nilikutana na kimoja nikakiuliza hivi mida hii ya giza shuleni kwenu kuna taa?

Jamani viongozi na wahusika,hii kweli ni sawa? Yani watoto sasa hivi wanapambania elimu ya msingi katika mazingira magumu kiasi hiki? Wanatoka jioni sana wanafika nyumbani usiku kweli ni sawa kwa umri wao?

Kuna wengine wa secondary nimewaona maeneo ya kariakoo nadhani itawakuwa pale Benjamini mkapa wanatoka shule saa 2 usiku, halafu hapo bado hawajapanda daladala kwa tabu,je wanafika nyumbani saa ngapi?

Ebu muwaonee huruma hawa vijana wadogo, hawastahili hizo changamoto
 
Haya mambo yalikataliwa na mbunge KISHIMBA..
 
Na unaona ni sawa? saa 4 usiku alooo nasubiri nifikie muda wa kusomesha nitakua mzazi mtata sana😂😂
Inaniudhi sana, tatizo wazazi wengi ni kufuata mkumbo, shule inalazimisha wasome mpaka saa 4 usiku, Ukikataa wengine wanawaacha watoto wao unabaki peke yako. Bora amalize tu niachane na huu ujinga.
 
Una bahati ulisoma ukiwa underaged

Changamoto za kusoma ukiwa Mkubwa, unakuta unaanza michezo mibaya ukiwa bado shuleni

Ndiyo unapata zile kesi, mwanafunzi wa darasa la V ampa mimba Mwalimu wake 🙌

Huyo rafiki yako Zahra aliwezaje kusoma huku ananyonyesha?

Sisi mwaka 47, ilikuwa tunahitimu shule ya msingi tukiwa na miaka 20 hadi 25 🤪
 
Tunaishi katika zama ambazo Afisa elim anafokewa,mratibu anafokewa,mwalimu mkuu anafokewa,mwalimu wa SoMo anafokewa!kwamba kusiwe na zero!

Kifupi ni kwamba ,hakuna elim siku hizi Bali ufaulu ndio umefanywa elimu,yaani watoto wanaandaliwa kufaulu mitihani na sio kufaulu maisha!!

Kwenye jamii Kuna aina zote za watu wenye vipaji tofauti huwezi lazimisha wote wapate A kwenye mitihani badala wapate A kwenye kujamiiana na nature Ili kupata kilicho Bora zaidi!

Plato Ali group watu katika makundi matatu,na mtihani halisi lazima wawepo watakaopata zero ,hiyo no lazima kwa Maana halisi ya mtihani!mashindano ya kufaulisha sio muktadha halisi was elim Bali data za majukwaani!!

Watoto wanaandaliwa kufaulu makaratasi kuliko kujamiiana na asili nature!matokeo yake tunaandaa maroboti yatakayokufa Kwa msongo wa mawazo coz hayana uwezo wa kupambana na mitihani ya asili katika mazingira halisi!!

Cases za kujiua zitaongezeka zaidi Kwa wasomi coz elim wanayoipata Haina tija kwenye kujamiiana na asili,hawatakua na uwezo wa ku handle nature!!

TULIOSOMA ZAMANI ENZI ZA VIBUYU VYA MAJI,TUKIBEBA MABOGA,MAHINDI,KARANGA ZA KUCHEMSHWA NA N.K TULIINJOY SANA NA SASA TUMESHIKA DOLA TUKIWA NA SULUHISHO LA HARAKA LA KILA HALI INAYOTUPATA KWENYE MAISHA,TUNAHESHIMU
 
Siyo sahihi hata kidogo tatizo ni Serikali kupmbavu ya ccm ....hata jumamosi na jumapili ni kosa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwenda shule ....shule aitakiwi kuwa mateso kwa watoto.
 
Sio sahihi bali uchaguzi wa wazazi kuchagua shule za mbali ni sababu mojawapo. Pia ratiba za shule zinawabana watoto haswa wenye ufaulu mdogo kuunganisha na tuition baada ya masaa ya kawaida ya masomo.
 
Na unaona ni sawa? saa 4 usiku alooo nasubiri nifikie muda wa kusomesha nitakua mzazi mtata sana😂😂
From an experienced to a future mzazi mtata, muda ukifika kazia hapo hapo maana kumlazimishia mtoto kitabu asubuhi mpaka usiku ni kumtesa tu, wala haiwasadii zaidi ya kukariri vitu.

Wangu alivyoingia Class 4 nilikataa boarding (never been a fan), nikaambiwa basi lazima umlete asubuhi mapema na achukuliwe saa mbili usiku ili ratiba yake ya masomo isivurugike. Nikamwambia mwalimu, dogo atakuja kwa school bus, na atarudi nalo nyumbani kama ilivyokua mwanzo. Swala la kufeli niachie mimi kama mzazi.

Nyumbani akawa anapimzika zake na mwisho wa siku bado akaondoka zake na A 😏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…