Aliyeleta huo ufala alikuwa ni Mkenya mmoja akiitwa Mungai kama sikosei. Aliunganisha masomo kibao na kufuta mengine. Yaani wizara muhimu pengine kuliko zote imegeuzwa kuwa shamba la bibi. Kila waziri anayekuja anakuja na lake. Akaja Kawambwa na naibu wake bomu aliyetoa kali kwenye kongamano huko Afrika Kusini kwa kudai eti Tanzania is a union of Tanganyika and Zimbabwe. Alikuwa akiitwa Mgulu nadhani.
Mfumo mzima wa hii elimu uchwara unatakiwa kufumuliwa na hili linapaswa kushirikisha wadau wote muhimu - wazazi, walimu, wanafunzi, wataalamu wa mitaala, wachumi na hata sisi watu wa mitaani tuliokomea la saba. Hii kukurupuka tu kwa maagizo ya wanasiasa hatutafika po pote.