Poa 2
JF-Expert Member
- Jul 7, 2019
- 1,317
- 1,320
Wakuu habari,
Miongoni mwa propaganda iliyopitwa na wakati lakini bado inatumiwa sana na wana CCM ni hii, kwamba upinzani ukichukua nchi utaleta machafuko.
Huwa najiuliza upinzani una nguvu sana na CCM wanalijua hilo ndio maana hutumia mbinu chafu dhidi ya upinzani Ili kujibakisha madarakani.
Wanachama wengi wa upinzani huwa wako tayari kwa lolote kulinda haki zao hata kwa kutumia mbinu chafu kama CCM lakini viongozi wa juu huwatuliza.
Vyama vya upinzani viko toka miaka ya 1990's havijawahi kuvunja amani au kuleta vurugu hapa nchini, bali wao hufanyiwa vurugu na CCM kwa miaka yote.
Sasa itakuwaje siku wapewe mamlaka na wananchi ya kuongoza nchi ndio wavunje amani? Na walete vurugu? Na vurugu hizo watawaletea wakina nani au wananchi waliowapa ridhaa?
Hebu wana CCM jibuni hoja wafafanulieni Watanzania, upinzani utaleta vurugu au uvunjifu wa amani kwa namna ipi?
Nyie CCM ndio mtavunja amani ya nchi hii kwa ubinafsi wenu uliokithiri.