Hivi ni uzembe wa mdomo au maksudi?

Hivi ni uzembe wa mdomo au maksudi?

Lisaa....masaa....hii umeingia ndani mno....
Saa moja....saa tano

Mtihani kwa mfano, tunafanya kwa masaa mawili au saa mbili?

Haya tuendelee, Hivi ipi ni sahihi, Ovyo au hovyo.
 
hata wewe ni mchafuzi wa lugha, umeandika KAARIBU badala ya KAHARIBU
 
Sio makusudi ni mother tongue yao imawaharibu so wanakuwa wamezoea maneno ya aina fulani zaidi kuliko mengine ndo maana utaona wa Arusha wana RRR wa MAra pia wana RRR wakati wa Iringa ni LLLLL
 
mnapokuwa mnakosoa mujue kuwa katika matamshi ni ruhusa mtu kuvunja taratibu za lugha kimatamsh ili aweze kuendana na mazungumzo
mfano wazaramo wataalam wa kuongea kiswahili kwa haraka husema mwanke au (enyee) badala ya mwenyewe kwa mtazamo wa juu juu amekosea ila c kweli kwani amefikia lengo la lugha kitafsiri (kueleweka) ikiwa mtu anaonge c kweli atazungumza sawa na anayeandika. ni lazima azungumze kulingana na mazingira hata ikibidi kuvunja taratibu ila lengo aeleweke
 
Huwa nachukia sana ninaposoma na kukutana na maneno haya
Lula badala ya Rula
Mologolo-morogoro
Foreni-Foleni
Ugari-Ugali
Kula-Kura
Nimekuwa nikijiuliza tatizo ni nini kwa watu kama hawa
Nashauri tuanze kuwapiga vita kuboresha lugha yetu ya kiswahili
Tulipiga vita X kuwa S na tumefanikiwa
Kuna mkuu anaitwa LEGE kaanzisha topic anaandika ABILIA wa makongo,Kaaribu utamu wa UZI jirekebishe MKUU
Usichukie mkuu LEGE hapa ni sehemu ya kurekebishana jombaa!
Inawezekana ni watu wavivu wa kubadilika huwezi kuwa kiongozi mkubwa wa nchi then unatumia kuongea au kuandika kwa mfano niliotoa hapo juu.

Mkuu hapo kwenye colour mbona sasa umekuwa mzembe pia. Sema Kaharibu na sio kaaribu, mimi sipendi huu uchafuzi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hapo kwenye colour mbona sasa umekuwa mzembe pia. Sema Kaharibu na sio kaaribu, mimi sipendi huu uchafuzi

Ok!nimesha papiga spana mkuu!
 
Kichuguu,
wakati tunapata uhuru mengi yalisemwa na kweli tulikuwa hatupo tayari kwa sababu waafrika wengi tulikuwa hatufahamu nini maana ya Uhuru.. leo hii inaonyesha wazi. Nyerere aliyajua yote haya na ndio maana ilipovumbuliwa gas na mafuta miaka ya 70's na mwanzo 80's Nyerere alidai ziachwe huko chini ardhini kwa sababu watu wangu hawana elimu wala uwezo wa ku-deal na mali kama hiyo. Wote wataacha kufanya kazi kwa sababu utajiri umepatikana!...Kwa mwafrika utajiri ndio maendeleo yenyewe.
TZ tunayo mafuta na wala msije danganywa!
Nyerere hakufahamu tu kuwa mbali na elimu tulikuwa bado na akili za kitumwa na hadi leo bado hatujaelemika zaidi ya elimu ya kitumwa!...Sasa Tazara nayo itauzwa kwa mpango gani hali ni mali ya jumuiya?... Zambia wapo radhi?... jamani mweee!...mimi nipeni hiyo Tazara club tosha kabisa nitafunga domo langu.kwi..kwi...kwi...
Kichuguu sii Mlima, nenda kwenye mada ya Idriss Rashid, leo nimeweka orodha ya viongozi walioshiriki kuipitisha IPTL kisha nambie kabaki nani?... na list itaendelea kesho. Kila unayemfikiria kuwa msomi mzuri utamshangaa ktk maamuzi.. JK, Mwinyi na Mkapa ndani mshikaji sasa hapa kweli tutafika?

hivyo vitu vipo na husababishwa na athari za vijieneo au lugha mama. na inakuwa tayari imeathiri mfumo wa lugha katika karakana ya ubongo wake kwenye pango la lugha hata ukimrekebisha ni muda mfupi tu anaboronga.
ni sawa na kwamba umwambie muhaya atamke ng'ombe hawezi atatamka ngombe.
 
Back
Top Bottom