Hivi nina Madhaifu gani mimi?

Hivi nina Madhaifu gani mimi?

Joined
Aug 19, 2021
Posts
54
Reaction score
78
Wakuu, jambo likikuchanganya ni bora kushare ili upate mawazo mapya.

Mimi nimehitimu chuo miaka 8 imepita. Kipindi chote cha masomo tangu darasa la kwanza nina rekodi nzuri ya ufaulu na uwezo wa kufanya mambo mbali mbali hasa ya kiubunifu, n.k.

Mara baada ya kuhitimu nilifanikiwa kupata kazi mbali mbali za muda mfupi na za kujitolea pia.

Tatizo sasa baada ya miaka kama minne kazi hizi zote zilikoma, kila napogusa sifanikiwi kupata. Iwe kuajiriwa au kujitolea.
Mpaka imefika hatua najiuliza kimenitokea kitu gani au nina madhaifu gani mimi? Mbona interview siitwi tena?

Haya sasa nilipoona nimekaa mda mrefu bila mwelekeo nikaamua kujichanga kadili nilivyoweza nikaamua kufungua duka dogo la rejareja.
Hili nimekomaa nalo ni mwaka wa 3 sasa. Lakini cha kushangaza sioni matumaini ya kuwa na future iliyo nzuri au bora kutokana na biashara hii.

Kiukweli nikikaa nikatafakari na kuangalia dunia inavyoenda na watu wanavyopambana na kufanikiwa na umri unavyoenda mbio⁴ R3 binafsi najiona kama nina mapungufu.

Najiona kama nina madhaifu, tatizo sijajua haya madhaifu ni katika kufikiri? Ni katika uwezo wa kutafuta connection? Ni madhaifu katika kipi hasa??

Ndugu msomaji, kama umenielewa naomba unisadie kwa mtazamo wako hapo naweza kuwa na madhaifu gani? Kumbuka mchango wako unaweza kuchangia kubadilisha maisha yangu na wewe ukabarikiwa zaidi.
 
Wakati ukiwa chuo ulijiweka ktk mtazamo gani? au ulikuwa na malengo gani. Hiyo biashara umeifanya tuu but haikuwa plan yakofanya hilo duka la rejareja kama DARAJA la kukupeleka mbele zaidi. Jikite kuiboresha ukiwa chanya kuelekea ulikoamini ndio destination yako.....yes 3 yrs shughuli yeyote unayofanya kama haina dira achana nayo.....ila usiaiiche pambania mkuu..
 
UNAELIMU GANI NA UMESOMEA NINI NA UNAUJUZI GANI, nakushauri ujitoe ufahamu toka hapo ulipo nenda mbali na hapo kaanze maisha katika wilaya zingine,umweke Mungu mbele utafanikiwa
 
Ni maisha tu mkuu endelea kupambana nakubuni mambo tofauti .tatizo lako nahisi unajilinganisha na watu unasema unakiduka kuna wasomi kama ww wako humu hawana mtaji kama wako yotekwayote wakat wamungu unahusika ktk maisha yangu nayako
 
Umeoa?
Umesomea cozi gani?
Una sali / swali?
Mafanikio ya kitu chochote yanahitaji muda mkuu... Hivyo usikatetamaa
But Mungu ndo anae panga sio mwanadamu
Nimeoa mkuu.
Nimesoma Regional Development Planning.
Ninaswali, japo sio sana niwe mkweli.
Asante mkuu sitokata tamaa.
 
wakati ukiwa chuo ulijiweka ktk mtazamo gani? au ulikuwa na malengo gani, hiyo biashara umeifanya tuu but haikuwa plan yako.....fanya hilo duka la rejareja kama DARAJA la kukupeleka mbele zaidi. Jikite kuiboresha ukiwa chanya kuelekea ulikoamini ndio destination yako.....yes 3 yrs shughuli yeyote unayofanya kama haina dira achana nayo.....ila usiaiiche pambania mkuu.
Kiukweli malengo yalikuwa ni kuajiriwa.
Lakini ngoja nipambane mkuu.
Hivi hakuna madhaifu ambayo naonekana kuwa nayo mpaka hapo?
 
Hujaeleweka bado jaribu kuainisha ni kivipi unahisi una tatizo?
 
Ukweli mchungu Ni kua ili upate changes kubwa kwenye maisha yako inabidi Kuna dili moja kubwa ujipindue...lakini ukifanya vitu average...na maisha yako yatakua average
 
Hujaeleweka bado jaribu kuainisha ni kivipi unahisi una tatizo?
Ok.
Yaani nikilinganisha muda wa miaka yote 8 nipo mtaani baada ya kuhitimu na hatua niliyopiga kimaendeleo hasa kutokuwa na ajira au shughuli binafsi yenye kipato cha kuridhisha au matumaini ya kuwa nayo.

Haya hayawezi kuwa yanatokana na madhaifu yaliyo ndani yangu? Je yanaweza kuwa madhaifu gani hayo?
 
Tatizo limeanzia kwa kusoma ukiwa na malengo ya kuajiriwa,Je kichwani bado una matumaini ya kuajiriwa?
 
Back
Top Bottom