HOJA Hivi nini kinaendelea? Mbona Masaki imekuwa kama "Construction Site"? Kulikoni kila sehemu inajengwa?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Ngorongoro! Bandari!
Kauza nini?
Kamgawia hawara wake Kabula nyumba ya serikali.

JPM ndiye kamfundisha Samia habari za "kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake" na kuwezesha Samia kuona habari za uzalendo ni ujinga tu na yeye anapiga tu.

Wote hawa ni ma CCM mafisadi tu kwa nini mnaona huyo JPM wenu msafi hivyo wakati yeye ndiye kauza nyumba za serikali Masaki?

Magufuli kawapiga pesa ndefu kwa ku hijack manunuzi kwenye miradi mikubwa, ka fast track miradi mikubwa manunuzi yatoke Ikulu na yasipitiwe na CAG, mpaka kamuondoa CAG Assad kinyume na sheria sasa tumeambiwa na hukumu ya mahakama ya majuzi hapa. Halafu kapiga ban mazungumzo bungeni kuoneshwa live msione majadiliano, halafu kapiga ban mikutano ya kisiasa msiongelee, halafu kanunua wanasiasa wapinzani wasimpinge.

Huyu hakuiba pesa tu, huyu kaiba mpaka uhuru wa watu.

Huelewi wapi?
 
sisi masikin bana tuna shida sana
 
Nilirudi likizo 2012 mdogo wangu akanipeleka kule Doubletree Hotel kuangalia walivyojenga.

Baadaye kidogo nikasikia mgogoro wanamwaga maji machafu baharini.

Sijakanyaga Bongo tena.

Ukija mara hii utapotea. Hayo maeneo Doble Tree zamani ni sawa na pale PPF Tower posta
 
Mlaumu mkapa na mama Anna mkapa
Logical non sequitur fallacy.

Wanajeshi na wanasiasa wa Nazi Germany walioshitakiwa katika Mahakama ya Nuremberg, kwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Wayahudi, walijitetea kwamba wao walikuwa wanafuata amri kutoka juu tu, hivyo waachiwe, kwa sababu hawakufanya maamuzi, walitekeleza amri tu.

Mahakama ya Nuremberg ilikaa na kuwapata na hatia, ikisema, ukitekeleza amri haramu, inayovunja misingi ya haki za binadamu, iliyo kinyume na sheria, na wewe una wajibika kwa kutekeleza amri hiyo.

Huna utetezi wa kusema "mimi nilitekeleza amri kutoka juu tu". Huu si utetezi, hapo ulichofanya ni kukubali kosa.

Kwa msingi huu wa kanuni ya Nuremberg, kwanza hakuna niliposema Mkapa hana lawama. Mkapa ana lawama kubwa sana.

Lakini, Mkapa kuwa na lawama hakuondoi lawama kwa Magufuli.

Nasema Magufuli naye ana lawama, alishiriki. Hawezi kuepuka lawama kwa hoja ya kwamba Mkapa ndiye aliamua.

Katika kanuni ya Nuremberg anakutwa na hatia.

Katika kanuni ya "collective responsibility" Magufuli kama hakukubaliana na uuzwaji wa nyumba, alitakiwa kufanya jambo moja kati ya matatu haya.

1. Kujenga ushawishi na kubadili msimamo wa serikali. Mkapa alimpenda sana Magufuli, pengine angemsikiliza. Hakufanya hivi. Hakubadili uamuzi wa serikali.

2. Kama alipinga na hakusikilizwa, na aliona jambo hili ni la muhimu sana, angeweza kujiuzulu uwaziri na kulipinga jambo hili akiwa nje ya serikali. Hakufanya hivi.

3. Kama hakuweza kubadili msimamo wa serikali, na hakuweza kujiuzulu uwaziri, anatakiwa kukubali maamuzi ambayo hayataki, na kukubali lawama na hatia zozote zitakazoendana na maamuzi hayo. Hawezi kujitenganisha na maamuzi hayo. Hili ndilo Magufuli alilolifanya.

Sasa kwa uamuzi wake huo wa namba 3, utamtenganishaje Magufuli na lawama za kuuza nyumba za serikali?
 
Kwa hiyo sasa hivi iko vizuri kisiasa eti
 
Wale wanaomuonaga Magufuli kama mtakatifu waje wasome hapa.

Viongozi waadilifu wasipokubaliana na jambo huwa wanajiuzuru, wote tunakumbuka issue ya rada kuinunuwa kutoka Uingereza kuna waziri tena mwanamke alipinga na kujiuzuru.

Imagine nchi mnufaika wa biashara lakini wanatuonea uchungu maskini tunafanya manunuzi yasiyokuwa na tija.
 
Wee endelea Tu na hekaya za "no reforms no elections" Hadi leo, zikiisha utajikuta kwenye ZOO
 
Pesa za Wicknell😂
 
Yule Mama anaitwa Clare Short. Alikuwa Minister for International Development, UK.

Alijiuzulu kwa kufuata principle kwamba serikali imefanya mambo ambayo hakubaliani nayo.

Alisababisha mpaka kampuni ya BAE ikarudisha pesa Tanzania.
 
Site zote hizo ni za familia moja... maeneo ya wazi pia yameshachukuliwa. Akili na wizi
 
Upo sahihi niliwahi kuishi mitaa ya chole road miaka 20 iliyopita nilipojaribu kwenda miaka ya hivi karibuni nikapotea.
 
Shetani mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…