Hivi nini kinawamaliza WASANII wetu wa BONGO MOVIE??

Hivi nini kinawamaliza WASANII wetu wa BONGO MOVIE??

Mdau Makini

Member
Joined
Sep 18, 2012
Posts
70
Reaction score
10
Kweli hainiingii akilin jinsi wasaanii wetu wanavyo kufa kwa kasi.Yaani kwa mwaka wa jana(2012) tumepoteza wasaan maarufu wawili(R.I.P Kanumba & Sharo Millionea) Na leo hii tunaupokea mwaka (02/01/2013 siku ya pili kwenye mwaka) tumempoteza msaanii wetu maarufu(R.I.P SAJUKI).Sipati picha hii kasi itatufikisha wapi, anyway Mungu uwalaze mahali pema peponi wapendwa wetu walio tangulia mbele ya mkono wa haki, Mungu ibariki Bongo Movie, Mungu ibariki TANZANIA!! Ameni.
 
mkuu kwani wanakufa peke yao?

tukiangalia kwa undani kwani ni percent ya waalimu wangapi, wanasiasa wangapi, na wakulima wangapi wamefariki kwenye miaka mitatu iliyopita

Nadhani kifo ni kifo tu na wote tunaelekea huko nadhani hapa tunauliza swali pasipo na swali (its normal watu wanazaliwa, na wanakufa) labda ni kuepuka tu vile vifo vinavyozuilika vya ajali na kuangalia afya zetu.
 
Mkuu! mwaka jana ni zaidi ya wawili nadhani kuna dada mmoja na yule dogo Maganga, hao wote pia ni wa Bongo movies!. Na ni upepo tu huu, utapita mkuu! (sorry guys, i am actually serious about the topic, whilst taking the mickey of this very stupid and silly quote though)
 
Wewe unaonekana ni mchochezi, mnafiki na mpenda ushirikina. Kifo kimeumbiwa kila mwanadam na sio kipaji au wadhifa alokuwa nao. Kama kweli unamwamin Mungu basi hautapata shaka na kufadhaika sana na kama utabeza basi we ni mpagani. Kwani umehoji ni watu wangapi wamekufa siku ya leo? Na wangapi ktk familia ya damu moja hupotea kwa pamoja? Acheni uchochezi wa namna hiyo na kama vp watafute wasanii mtafute mbaya au kinachosababisha. R.I.P Sajuki.
 
Kwa hiyo unataka kutuletea mambo ya freemasons au?
 
Ni binaadamu kufa ni wajibu. Unafahamu vifo vyao kwa sababu vinatangazwa magazetini, lakini ukweli ni kuwa binaadamu huwa wanakufa.
 
Kweli hainiingii akilin jinsi wasaanii wetu wanavyo kufa kwa kasi.Yaani kwa mwaka wa jana(2012) tumepoteza wasaan maarufu wawili(R.I.P Kanumba & Sharo Millionea) Na leo hii tunaupokea mwaka (02/01/2013 siku ya pili kwenye mwaka) tumempoteza msaanii wetu maarufu(R.I.P SAJUKI).Sipati picha hii kasi itatufikisha wapi, anyway Mungu uwalaze mahali pema peponi wapendwa wetu walio tangulia mbele ya mkono wa haki, Mungu ibariki Bongo Movie, Mungu ibariki TANZANIA!! Ameni.

acha kumkufuru mungu wewe,,,,,,hao wanaokufa ahadi zao zimetimia,sajuki kaumwa kama wanavoumwa binadam wengine,kanumba mapenz yalimuua na wengineo sasa ww wasiwasi wako nini?haya tuambie kinachowamaliza ni nini?hawa ni binadam wameumbwa na WATAKUFA TU,,,,
 
Tunaona wasanii wanakufa kwa wingi kwa sababu ni watu wanaofahamika kiurahisi, hivi unajua walimu, askari, wanafunzi wangapi wamefariki mwaka huu? Ungejua idadi yao ungeweza kulinganisha mkuu
 
Tunaona wasanii wanakufa kwa wingi kwa sababu ni watu wanaofahamika kiurahisi, hivi unajua walimu, askari, wanafunzi wangapi wamefariki mwaka huu? Ungejua idadi yao ungeweza kulinganisha mkuu
Ni kwa sababu ya umaarufu tu mbona watu wengi wanakufa.
 
tusimkalipie mtoa mada ni mtazamo wake, lakini jambo la msingi fahamu kuwa haki pekee ya msingi ambayo hainyang'wanwi na mtu ni kifo, unavoshangaa wao kufa mwaka jana na mwaka huu, hebu tuambie ilibidi wafe lini?
 
mkuu kwani wanakufa peke yao?

tukiangalia kwa undani kwani ni percent ya waalimu wangapi, wanasiasa wangapi, na wakulima wangapi wamefariki kwenye miaka mitatu iliyopita

Nadhani kifo ni kifo tu na wote tunaelekea huko nadhani hapa tunauliza swali pasipo na swali (its normal watu wanazaliwa, na wanakufa) labda ni kuepuka tu vile vifo vinavyozuilika vya ajali na kuangalia afya zetu.

ufafanuzi mzuri ndugu, kila nafsi itaonja umauti..!!
 
Kazi ya Mola haina Makosa,hatuombei mtu kifo,bt sasa unataka afe nani??Eti?Jst ask in ur own mkuu.Ni cfa za Lvg org.Tusikoplikeiti bwana.Mtu anazaliwa,Then anakufa.
 
Kwani hawa wasanii wameamriwa kufa kwa mfumo gani nakusii usije ukamkosea Mungu
 
Wasanii wengi wanafast track maisha yao kwa kutumia madawa ya kulevya, pombe, sigara, ngono zembe, kuparty kwa muda mrefu na mmbo mengine mengi. Ukitizama world wide utaona kuwa wasanii wengi life span yao ni fupi ukilinganisha na watu wa kawaida.
 
Ni kifo tu mkuu! Tatizo hapa ni wauza sura ndo maana unaona ni wengi! Leo mtaani kwetu kuna misiba mitatu kwa sababu marehem siyo wauza sura ndiyo maana taarifa hazijakufikia!
 
Baada ya kufikiria ni vifo vingapi vinatokea hospitali kila siku,nikataka kumuuliza mtoa mada ni wasanii wangapi wamekufa.Lakini nilipojaribu kutumia sehemu ndogo tu ya akili yangu,nikagundua kuwa jamaa amefikiria kwa upeo wa umbali wa pua yake.Kwa hiyo sio tatizo lake,hapo ndipo uwezo wake wa kufikiri umeishia.
 
Back
Top Bottom