Hivi nini kinawamaliza WASANII wetu wa BONGO MOVIE??

Hivi nini kinawamaliza WASANII wetu wa BONGO MOVIE??

Mm jibu ninalo
BONGO MOVIE wanakufa kwa sababu wanadamu hatujaumbwa kuishi milele.
Umeelewa mdau makini?
 
Wasife wao ni akina nani, binadamu wote ni sawa, kila nafsi itaonja mauti,wewe umawasikia coz ni watu maarufu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
hata marais walikufa mwaka jana, nini....
 
mkuu kwani wanakufa peke yao?

tukiangalia kwa undani kwani ni percent ya waalimu wangapi, wanasiasa wangapi, na wakulima wangapi wamefariki kwenye miaka mitatu iliyopita

Nadhani kifo ni kifo tu na wote tunaelekea huko nadhani hapa tunauliza swali pasipo na swali (its normal watu wanazaliwa, na wanakufa) labda ni kuepuka tu vile vifo vinavyozuilika vya ajali na kuangalia afya zetu.

br umetumia busara nyingi sana kujibu swali lisiloulizika, nadhan angeuliza watu wanaojulikana sana kwa jamii maana ukimpa orodha yako nami yangu anaweza akaona kua ameuliza kimakosa
 
Haina mashiko! Umefanya research ni walimu, askari, madokta n.k wangapi wamekufa then ulinganishe na hyo idadi ya wasanii uchwara wako?
 
Tunaona wasanii wanakufa kwa wingi kwa sababu ni watu wanaofahamika kiurahisi, hivi unajua walimu, askari, wanafunzi wangapi wamefariki mwaka huu? Ungejua idadi yao ungeweza kulinganisha mkuu

kweli mwaya weengi wametutokaaa sema wasanii kwakua wanatangazwa bt vifo vingekua underkapet kama wasiojulikana wala tusingeona shidaaaa
 
Tunaona wasanii wanakufa kwa wingi kwa sababu ni watu wanaofahamika kiurahisi, hivi unajua walimu, askari, wanafunzi wangapi wamefariki mwaka huu? Ungejua idadi yao ungeweza kulinganisha mkuu

asante sana.. nilikuwa nakuja hapohapo maelezo mazuri sana
 
Kwani alitaka afe nani??? Wakwao au wa kina nani wangekufa ndo asinge jiuliza????

Anyway mie ninajiuliza ni kwa maslahi yapi msanii wa bongo anae lalamika kuibiwa kazi zake, muvi zao zinakodisha na kukuta watu wa laki 5 wa gongolamboto kihalali wamenunua DVD 5 coz ndizo zinazo nunuliwa na kucopy then kukodishwa, na hapo bado hajaibiwa na muhindi (distributor) ANAKUWA NA UWEZO WA KUMILIKI MILLION 200 na Zaidi na hapo kaingia kwenye usanii miaka miwili ilopita na watu kama kinabishanga bashaija, keni, rich bado wanasota. Wanazipata wapi hizi amount kubwa kiasi hiki???
 
Kweli hainiingii akilin jinsi wasaanii wetu wanavyo kufa kwa kasi.Yaani kwa mwaka wa jana(2012) tumepoteza wasaan maarufu wawili(R.I.P Kanumba & Sharo Millionea) Na leo hii tunaupokea mwaka (02/01/2013 siku ya pili kwenye mwaka) tumempoteza msaanii wetu maarufu(R.I.P SAJUKI).Sipati picha hii kasi itatufikisha wapi, anyway Mungu uwalaze mahali pema peponi wapendwa wetu walio tangulia mbele ya mkono wa haki, Mungu ibariki Bongo Movie, Mungu ibariki TANZANIA!! Ameni.

Kuwa msanii wa bongo movie hakumaanishi kwamba wewe ni tofauti na binadam wengine. Kifo ni sehemu ya maisha ya binadam hapa duniani. It doesnt matter upo katika kundi lipi. Siku yako ikifika ni lazima uondoke, whether unacheza filamu, unaimba kwaya au unaendesha daladala.
 
asante sana.. nilikuwa nakuja hapohapo maelezo mazuri sana

Ningelikuwa mimi ni mwalimu ningekupa 1000%. Aende Lugalo hospital aone jinsi wanajeshi wanavyopukutika kama majani kila dakika.
 
Baada ya kufikiria ni vifo vingapi vinatokea hospitali kila siku,nikataka kumuuliza mtoa mada ni wasanii wangapi wamekufa.Lakini nilipojaribu kutumia sehemu ndogo tu ya akili yangu,nikagundua kuwa jamaa amefikiria kwa upeo wa umbali wa pua yake.Kwa hiyo sio tatizo lake,hapo ndipo uwezo wake wa kufikiri umeishia.

Teh teh teh, mi napita tu.
 
Kinachowamaliza ni kifo
Ukitaka kujua chanzo ni hivi:
Kanumba alikufa kwa ajali iliyoambatana na kutumia kilevi na wivu wa mapenzi.
Kijoti na wenzie ajali pia nk.
Shalo milioni kwa ajali ya gari
Mzee Kipara, Sajuki, Mlopelo na Maganga kwa kuugua (iwe muda mrefu au mfupi ila waliugua).
Paka Mapepe ni matatizo ya uzazi

Hayo unayofikiri wewe nadhani ukienda kwenye jamii ya askari, walimu, nk utauliza hayo.
Mwaka jana kwa mfano kwenye tasnia ya sheria wamekufa si pungufu ya mawakili watatu, askari wa JWTZ si pungufu ya kumi wakiwemo waliowahi kuiletea sifa nchi hii. Wanasoka hawapungui wanne!

Fikra za ushirikina uanza hivi hivi kuhoji eti kwa nini fulani kafa.
 
Fikra za ushirikina uanza hivi hivi kuhoji eti kwa nini fulani kafa
.

Asante sana. Umefunga mjadala. Walate mada zenye akili.
 
Kinachowamaliza ni kifo
Ukitaka kujua chanzo ni hivi:
Kanumba alikufa kwa ajali iliyoambatana na kutumia kilevi na wivu wa mapenzi.
Kijoti na wenzie ajali pia nk.
Shalo milioni kwa ajali ya gari
Mzee Kipara, Sajuki, Mlopelo na Maganga kwa kuugua (iwe muda mrefu au mfupi ila waliugua).
Paka Mapepe ni matatizo ya uzazi

Hayo unayofikiri wewe nadhani ukienda kwenye jamii ya askari, walimu, nk utauliza hayo.
Mwaka jana kwa mfano kwenye tasnia ya sheria wamekufa si pungufu ya mawakili watatu, askari wa JWTZ si pungufu ya kumi wakiwemo waliowahi kuiletea sifa nchi hii. Wanasoka hawapungui wanne!

Fikra za ushirikina uanza hivi hivi kuhoji eti kwa nini fulani kafa.

Wabeja sana yani umemaliza kila kitu thread haina mashiko. Chukua tripple like
 
Kweli hainiingii akilin jinsi wasaanii wetu wanavyo kufa kwa kasi.Yaani kwa mwaka wa jana(2012) tumepoteza wasaan maarufu wawili(R.I.P Kanumba & Sharo Millionea) Na leo hii tunaupokea mwaka (02/01/2013 siku ya pili kwenye mwaka) tumempoteza msaanii wetu maarufu(R.I.P SAJUKI).Sipati picha hii kasi itatufikisha wapi, anyway Mungu uwalaze mahali pema peponi wapendwa wetu walio tangulia mbele ya mkono wa haki, Mungu ibariki Bongo Movie, Mungu ibariki TANZANIA!! Ameni.
Unaona hivyo kwa kuwa wanawatangaza. Kwa ujumla Tanzania watu wengi wanakufa kwa kukosa matibabu halisi, au ajali zinazoweza kuzuilika, ujambazi na vifo vingine vya kawaida. Ingawa ahadi nayo ikifika utaondoka tu. Hawa wengine hawatangazwi ndio maana. Wangekua wanakufa wao peke yao ndio ungeuliza hilo swali.
 
Mnashangaa kifo..angepona na hili akufa na jengine. Mwacheni alale in peace as long as hakuuliwa.
 
Back
Top Bottom