Mdau Makini
Member
- Sep 18, 2012
- 70
- 10
Kweli hainiingii akilin jinsi wasaanii wetu wanavyo kufa kwa kasi.Yaani kwa mwaka wa jana(2012) tumepoteza wasaan maarufu wawili(R.I.P Kanumba & Sharo Millionea) Na leo hii tunaupokea mwaka (02/01/2013 siku ya pili kwenye mwaka) tumempoteza msaanii wetu maarufu(R.I.P SAJUKI).Sipati picha hii kasi itatufikisha wapi, anyway Mungu uwalaze mahali pema peponi wapendwa wetu walio tangulia mbele ya mkono wa haki, Mungu ibariki Bongo Movie, Mungu ibariki TANZANIA!! Ameni.
Ni kwa sababu ya umaarufu tu mbona watu wengi wanakufa.Tunaona wasanii wanakufa kwa wingi kwa sababu ni watu wanaofahamika kiurahisi, hivi unajua walimu, askari, wanafunzi wangapi wamefariki mwaka huu? Ungejua idadi yao ungeweza kulinganisha mkuu
mkuu kwani wanakufa peke yao?
tukiangalia kwa undani kwani ni percent ya waalimu wangapi, wanasiasa wangapi, na wakulima wangapi wamefariki kwenye miaka mitatu iliyopita
Nadhani kifo ni kifo tu na wote tunaelekea huko nadhani hapa tunauliza swali pasipo na swali (its normal watu wanazaliwa, na wanakufa) labda ni kuepuka tu vile vifo vinavyozuilika vya ajali na kuangalia afya zetu.