Hivi 'No Reform no Election' inapigania na mgombea binafsi?

Hivi 'No Reform no Election' inapigania na mgombea binafsi?

No reform ili maanisha, bila reform ndani ya chama chetu CHADEMA hatuezi enda mbele. No surrender ina maana no surrender kwa team FAM.
 
siku hizi Extrovert umekuwa ukigawa sana thanks, umezishusha hadhi sana likes zako
 
Kwa kweli binafsi nimechoka na wagombea wa vyama. Hii 'No reforms no surrender' ya TL inapigania na mgombea binafsi?

Ngoma hiyooooo
 
Ni No reforms, no election. Bila shaka mgombea binafsi ni sehemu za reforms zinazotakiwa.
 
Inawezekana kabsa CDM na wadau tunahitaji mabadiriko haya ya kikatiba, kisheria/kanuni, kimfumo na kimtazamo.
Ila tukubaliane tu njia ya maandamano imethibitika kutoweza kuleta matokeo tarajiwa.
Tunahitaji kusikia mbinu mpya.
Na kwa vyovyote vile mbinu hiyo si ya kuchekeana.
"Negotiation with a terrorist flourishes terrorism'
 
Kama nakumbuka vizuri mahakama kuu iliamuwa kwamba kuzuia mgombea binafsi ilikuwa kinyume na katiba.

Watawala wakafanya mabadiliko ya katiba haraka haraka kulazimisha wagombea wawe wanachama wa vyama vya siasa.
 
Kama nakumbuka vizuri mahakama kuu iliamuwa kwamba kuzuia mgombea binafsi ilikuwa kinyume na katiba.
Ni kweli, Ila Mahakama ya Rufani ya Tanzania ndiyo ilitengua Hukumu hiyo.
Watawala wakafanya mabadiliko ya katiba haraka haraka kulazimisha wagombea wawe wanachama wa vyama vya siasa.
Mahakama ya Rufani ya Tanzania chini ya Jaji Mkuu wa wakati huo Augustino Ramadhan ilijipotosha na kutoa Uamuzi potofu ambao ulirejesha suala hili Bungeni ili likafanyiwe Uamuzi wa kurekebishwa kwa Sheria juu ya jambo hili. Uamuzi huo unakwenda kinyume na matakwa ya Katiba.
 
Ni kweli, hili nimelielimisha sana Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama? Na Haki, Haki, Haki! Serikali, Bunge na Mahakama hazina uwezo wala mamlaka ya kupora haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Je, jicho ona litaliona hili?
P
 
Inawezekana kabsa CDM na wadau tunahitaji mabadiriko haya ya kikatiba, kisheria/kanuni, kimfumo na kimtazamo.
Ila tukubaliane tu njia ya maandamano imethibitika kutoweza kuleta matokeo tarajiwa.
Tunahitaji kusikia mbinu mpya.
Na kwa vyovyote vile mbinu hiyo si ya kuchekeana.
"Negotiation with a terrorist flourishes terrorism'
Chadema hawawezi kutaka uwepo wa mgombea binafsi. Wao kama ilivyo tu CCM au vyama vingine vya siasa, wanapenda kutumia udhamini wa chama kama fimbo au kontroo ya kum-monitor mwanachama aliye na uongozi wa cheo cha kisiasa au anayegombea uongozi wa nafasi ya kisiasa serikalini.

Uwepo wa mgombea binafsi utafanya wanachama wao kutokuwa na hofu tena juu ya udhamini wao ikiwa wataamua kutokubaliana na matakwa ya chama, hata kama kutokukubaliana huko ni kwa maslahi ya Taifa au ya watu anaowaongoza
 
Back
Top Bottom