Lububi
JF-Expert Member
- May 3, 2013
- 2,158
- 3,808
Ni kwa bahati mbaya sana wanaominya uwepo wa mgombea binafsi huwa hawajitokezi kujenga hoja huenda ipo.(kama ilivyo kwa hoja ya uraia pacha).Chadema hawawezi kutaka uwepo wa mgombea binafsi. Wao kama ilivyo tu CCM au vyama vingine vya siasa, wanapenda kutumia udhamini wa chama kama fimbo au kontroo ya kum-monitor mwanachama aliye na uongozi wa cheo cha kisiasa au anayegombea uongozi wa nafasi ya kisiasa serikalini.
Uwepo wa mgombea binafsi utafanya wanachama wao kutokuwa na hofu tena juu ya udhamini wao ikiwa wataamua kutokubaliana na matakwa ya chama, hata kama kutokukubaliana huko ni kwa maslahi ya Taifa au ya watu anaowaongoza
Tunajikuta mzani umelalia upande mmoja.
Ila ccm wanakuwa hatarin zaidi kwa ueeoo mgombea binafs kuliko cdm.
Sabab kubwa ni CDM wote ilionao ni wake kimwili na kiroho lakin ccm ina wanachama wake kabsa(wanufaika na mbumbumbu) pamoja na wanafiki.