Hivi Padri mtuhumiwa wa ubakaji na yeye ana Wakili?

Hivi Padri mtuhumiwa wa ubakaji na yeye ana Wakili?

Kalpana

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2017
Posts
32,603
Reaction score
62,269
Uwakili ni kazi ya ajabu sana kwakweli, yaani unaanzaje kumtetea mtu katili kama huyo Padri, anaeweza kubaka watoto wadogo?

Mimi ni Mkatoliki kabisa ila naomba sana sheria isipindishwe kwa huyu mtu, apewe adhabu stahiki iwe fundisho kwa wote wanaonyanyasa watoto kihisia kwa sababu ya mwamvuli wa dini.

Leo mahakamani amejificha mpaka pua huiioni kama angekua hajatenda hivyo kwanini ajifiche? Wapo wengi aina yake huko makanisani wenye mapepo kama yake, wanaowaka tamaa kwa watoto ipo siku yao.

Yaani natamani hata mahakama wamtoe kwa wazazi na wananchi wa huko Moshi huyo mtu wamponde mawe. Kuna mtu amesoma naye Seminary anashangaa kwanini hata alifikia level ya upadri wakati tabia yake ya uchafu alianza zamani.

Wakili acha kutetea upumbavu wakati ushahidi upo, maana mtoto au watoto hawawezi kudanganya na tena kwa mtu waliyeaminishwa ni mtu wa Mungu mjue mpaka wamesema wamenyanyaswa haswa.
 
Kwa mtu ambaye inaonekana umeelimika unashangaza ukicomnent hivi?

Na akipimwa akagundulika ni khanisi utasemaje?

Mahakama ndio chombo cha kutenda haki na kuthibitisha pasipo shaka yoyote kwamba mtuhumiwa ni guilty.
Ni mara ngapi sheria inapindishwa hata kama ushahidi ni wa ukweli? Mimi nasema kama ushahidi upo basi sheria ichukue mkondo wake yani pasiwe na kuchelewesha hukumu.
 
Kuna mtu anaitwa Saul Goodman😅
Yeye anatetea wahalifu tu hata ukiua unaweza usifungwe. Kiwa hana pesa anatengeneza mchongo ili watu watende uhalifu wakamatwe awatetee.

Najua niko nje ya mada lakini...
 
Back
Top Bottom