Hivi Pesa za kurithi na mali zake zina laana gani??

Hii ni point. Washua wengi wana uhalifu nyuma ya mali zao.
Mali nyingi zimepatikana kidhulma dhulma hakuna mzazi anapenda mwanae afuate mkondo wake.. ni watu kam wachaga ndio wanaweza kuwaambia watoto wao kuwa tunapita hivi tunadhulumu vile..ila ni wachache bado wengi hawataki kabisa watoto au familia zao zijue chochote..
 
Hii mada yako umeitoa wapi? Mimi nimejibu mada, ya mirathi ya wazaz. Nimetoa mfano. Hayo maswali mengine hayahusu, alafu nikueleze mimi nimesoma, laiti mzee angetuacha hovyo, wote tungedondoka, na tusingefika hapa tulipo. Kuna shares, kuna vitu hata hatujavigusa hadi leo na vyte pesa. Yaani vinaendelea na ni vya mshua, kabla sijawa vizuri tayari nyumba mzee aliacha inameremeta
Sasa mkuu wewe ni tajiri? Au custodian ya mirathi
 
We graduate, jibu suali langu plz wewe ni tycoon or custodian wa mirathi kwa niaba ya wenzako?
 
Ndio umesema kweli mkuu,tatizo tunawapa samaki watoto wetu badala yakuwafundisha kuvua,ili wavue wenyewe,,hivyo hivyo kwa wake zetu,hilo ni tofauti sana na wenzetu wahindi.
.
 
Nakuombea kila la kheri kwa hilo
Kukaa shamba karibu na mjini ni wazo zuri sana ila usalama utakuwa mzuri?
Utahitaji vijana kama watono au zaidi wa kufanya shughuli zote na wewe ukiwa muangalizi wa juu
Kumbuka ukiweka mifugo utataka na kuwatafutia lishe ambapo itabidi ulime kwa ajili ya kuwalisha hao mifugo
Nawe utataka bustani pia ya mbogamboga
Kadri unavyoishi utaweka na kuku mara utamani bwawa la samaki ili uwe unatafuna mara moja moja
Nimewaza sana kuhusu maisha hayo ila nikawaza pia Ulaya lakini sio hapa nilipo maana hata waingereza wenyewe wakistaafu hawakai hapa

Spain au Italy na hata France hali ya hewa ni nzuri na unapata nyumba na shamba kwa thamani chini ya 3 bed ya UK
Hata Spain unapata shamba na nyumba mkuu na amani tele
 
Mwezi wa 4 nitakua hapo uingereza nakuja kucheki game Emirates
 
Nikionaga mtu katema yai la mbele kiasi hiki ,hasa nikiwa ofisini uwa naweka computer mbele ya uso wangu alafu nasoma kwa sauti ili workmate wasikie 😀😀
Alafu nazuga Kama Niko bize narudia hata Mara tano ,baadaye utasikia wanasema tumekusikia unapanga ndoto zako unaandika kwenye computer ,nacheka mwenyewe alafu nasema Mambo madogo .

Anyway Kuna raha kufanya kazi na vitoto vya kizazi hiki Ila mkuu Covax nakushimu sana
 
Hiyo ndo mipango yenyewe kua na vijana zaid ya wa tano siku zote natamani kufanya biashara isio kua na usumbufu wa TRA, na inanifanya niwe busy akili isilali kabisa......
 
Hiyo ndo mipango yenyewe kua na vijana zaid ya wa tano siku zote natamani kufanya biashara isio kua na usumbufu wa TRA, na inanifanya niwe busy akili isilali kabisa......
Haswaa peace of mind
Unakula hewa safi kila siku mjini unaenda ukiwa na shughuli zako tu
Unaweza kualika hata watu na baadae unatengeneza sehemu kama hotel na mapumziko ya uhakika watu wanakuja picnic unaweka hata wanyama pori walao majani tu
Kuna jamaa nimeona ana maisha hayo Kenya
Alianza kuishi na familia ila sasa watu wanamiminika kwenda kupumzika weekend na kulipia
Anachinja mpaka mbuzi wanne kwa familia zinazokuja kwake na kuku
Ila wanalipia kila kitu
Juice fresh anachuma tu kama passion na mengine
Aisee jamaa anaishi maisha ya kipekee
Kwa kuwa shamba ni kubwa anakaa mbali kidogo na vurugu hizo za weekend
Ameweka sasa mpaka michezo ya watoto
Ila sidhani kama wewe utapenda karaha hizo
 
Hakukua na hata ya kutoa taarifa sahihi na location ya unaowaongelea,hizi ni element za umbea
 
Hela za URITHI hazina laana .

Isipokuwa ELIMU ya fedha na kujitambua hii huwa ni changamoto.

Then kitu ambacho Mimi huwa nakijua sio kila mtu anahitaji Mali na pesa.

Hayo MAISHA ya kubahatisha labda ndo wapo comfortable nayo zaidi.

Mimi ninapomuona MTU anatumia Sana pesa bila mpangalio huwa simchukii wala kumfatilia maana sio kila anapenda maisha makubwa na yenye consistence.
 
Ukiichunguza sana pesa utatambua kuwa Haina tabia ya kukaa kwa mtu mjinga hata iwe bilioni moja inaisha yote na sio kuisha tu inaisha ikiwa umekuachia madeni makubwa.
 
Katika maisha yako usije akawa na matumaini mengi kwa watoto wako na mkeo, usijiumize sanaa eti unatengenezea watoto wako future watakuangusha tu......wafundishe maisha yao sio kuwatengenezea maisha hao hawakujua jinsi mali inavo tafutwa.
Mkuu umeongea la maana sanaaa
Imagine mtu unatafuta pesa unajibana et unawatengenezea watoto maisha mazuri matokeo yake ndo hayo Kiukweli mimi naona ni upumbavu bora uwafundishe njia ya kujipambania wenyewe ili wawe na uchungu nazo
Pesa zangu ni zangu na ntakula mwenyewe watoto watapata mahitaji yao sio mali za urithi
 
Huna pesa Wala mali wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…