Habari Wanandugu,
Katika kitu ambacho huwa kinanishangaza katika nyakati hizi ni maandishi na matamshi ya baadhi ya herufi na silabi. Huwa najiuliza kuwa Watanzania tunakwama wapi kwenye herufi "R" na "L" kuanzia kuyaandika mpaka kutamka?
Miaka ya nyuma kulikuwa na kichaka cha kujificha kuwa kuna Makabila ambayo hayana herufi "R" kwenye lugha zao za nyumbani, hasa mikoa ya kusini (Lindi & Mtwara).
Lakini siku hizi siyo kushindwa kutamka bali yanabadilishwa kabisa. Utakuta mtu na elimu yake anakuandikia "RAKINI" badala ya "LAKINI", Eti " KALILI" badala "KARIRI", kuna muda unamsikiliza mtu mpaka unashindwa kumwelewa kama anaongea kiswahili au anatumia lugha nyingine.
Tena kuna hawa Wachungaji na Manabii ukiwaskia wakiongea ndiyo wanazikazia " L" badala ya "R". Halafu hapo bado haujahamia kwenye vyombo vya habari.
Sasa cha ajabu siwani wakiwa wanabadili matumizi ya R na L wakiwa wanazungumza Kiingereza. Kwa hiyo huu ugonjwa ni ulimbukeni uliotujaa au ni wa makusudi?
MAONI KUTOKA KWA WADAU
------------