Hivi R, L na H, ni Ugonjwa wa Taifa?


Nilichokusudia mimi kukuambia, kupasi mtihani wa darasani sio hoja kabisa ya kuwa wewe ndio mwenye lugha, Hata mtoto wa kizungu akiingia tuition miaka miwili anaweza faulu pia.
 
Nilichokusudia mimi kukuambia, kupasi mtihani wa darasani sio hoja kabisa ya kuwa wewe ndio mwenye lugha, Hata mtoto wa kizungu akiingia tuition miaka miwili anaweza faulu pia.
Nimekuelewa sana tu mkuu. Sasa ni nini maana ya kuwa na mtihani? Nijuavyo mtihani ufanyika ili kutenganisha anayejua na asiyejua kitu fulani mfano lugha. Hivyo ikiwa mwenye lugha akafundishwa lugha yake hiyohiyo na kisha akapewa mtihani na akashindwa na mtu asiye mwenye lugha bali amefundishwa kwa muda tu ujue kuna tatizo kwa mwenye lugha.

Kwa maana nyingine ni kuwa aliyejifunza ame-jua/elewa hiyo lugha zaidi na mwenye lugha ajui lugha yake!! Ni sawa na wanaomiliki mfano magari wakati wanaogopa kuyaendesha hata baada ya kufundishwa udereva kisha wanatafuta dereva awaendeshe. Unamiliki lugha lakini ujui kuitumia kifasaha na mwisho una-fail mtihani wa lugha yako!!!, unapata wapi jeuri ya kutamba eti wewe ndiyo mwenye lugha?
 
Mjerumani kushindwa kutamka vizuri maneno ya kiswahili ni jambo linaloeleweka lakini Mswahili kushindwa kutamka vizuri maneno ya lugha yake ya kiswahili ni kihoja.
Sio "kihoja" ni "kioja"
 
profftobe,

Hata wewe waweza faulu mtihani wa kiengereza kuliko waengereza wenyewe, Bado Haitojaalisha kuwa wewe ndie mwenye kiengereza.
 
Kwenye vibao vya anwani za makazi imekuwa ni vihoja vitupu
 
Naenda kura nikishiba ndio nitaenda kupiga kula 🤣🤣
 
Ngoja tuache wabara wagombane hamna wanachojua hapo kweny lugha kazi kuweka ukabila mbele

Kuna moja ana masters ila meseji kama mtoto anavyoandika
 
Haiwezekani matamshi ya maneno jamii zote zikafanana

Mjerumani hata umshikie bunduki hawezi kutamka ROHO badala yake atatamka HOHO

Mhindi hata umlipue kwa bomu hawezi kusema WEWE atasema VEVE
 
Watu wanajifunza na kunyoosha lugha. Hajataka tu.

Mbona kuna wazee wengi tu wamezaliwa huko na wanaongea vizuri tu.
True story
Lugha mama sio issue

Wazee wengi wa zamani waliosoma are very eloquent actually

Mi naona ni watu hawajui tu kusoma na kuandika
Hawakuzingatia shuleni
Na hawasomi vitabu ili kutajirisha/enrich ufahamu wa maneno na misamiati

Mtu akikosea tu l na r sijui aniambie nini nimuone kama ni mtu serious

Cause how cant you comprehend something so basic; Grade 7 comprehension

Wengi ukifatilia hawana 'attention to details' na ufahamu wao una walakini fulani

Angalia taarifa na makala wanazoandika..utakutana na makosa mengine ambayo mtu makini unatakiwa uyaone
 
Watu wanajifunza na kunyoosha lugha. Hajataka tu.

Mbona kuna wazee wengi tu wamezaliwa huko na wanaongea vizuri tu.
Siku hizi ni tatizo la kuiga/ulimbukeni, zamani waandishi na watangazaji wa vyombo vya habari kutoka sehemu mbalimbali za nchi hii walikuwa hawafanyi makosa hayo, siku hizi wanaiga kama anayeharibu ni maarufu au msomi.
 
Ni ushamba fulani hivi ambao unawasumbua wengi
 
Kushindwa kutamka baadhi ya herufi za lugha ya Kiswahili kwa usahihi kunasababishwa na athari ya lugha ya kwanza ya mtu. Hilo ni tatizo linaloweza kurekebishwa iwapo mtu husika atapelekwa kwenye maabara ya sauti na kusaidiwa kurekebisha kasoro hiyo chini ya tawi la fonetiki liitwalo fonetiki matamshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…