Hivi R, L na H, ni Ugonjwa wa Taifa?

Wewe hujui kama watu wanaadapt kutumia hizo R na L kutokana na interaction na wanaotumia hizo R na L kimakosa
Kushindwa kutamka sauti fulani kunatokana na athari ya lugha ya kwanza ya mtu au mazingira na si suala la kuiga kama unavyotaka kutuaminisha. Fonetiki na fonolojia hazisemi hivyo.
 
Kutamka sio shida....bomoa unavyotaka. Shida ni kupeleka huo upuuzi kwenye kuandika.
 
... hii inaonesha tatizo lipo kuanzia elementary education "vidudu". Enzi zetu elementary education ilikuwa inafundishwa na wazee wenye uzoefu na waliokaribia kustaafu mnajihisi mnafundishwa na babu - kwenye maongezi penye nukta anaweka nukta; koma unaiona kabisa koma imetamkwa; n.k.

Penye R inatamkwa R na sio L na penye L vivyo hivyo all the way hadi herufi zote like V vs F, S vs Z ambapo ilikuwa inafundishwa namna ya kuchezesha ulimi na ku-control pumzi ili kila herufi isikike kwa ubora unaotakiwa.

Walimu macheck-bob na masister-du wa leo sina hakika kama wana huo muda au skills za kufundisha hivyo especially at the elementary level ambapo ndipo ubongo wa mtoto unatakiwa kufinyangwa kweli kweli. Garbage in, garbage out.
 
Tatizo lingine kubwa ni hili kama lako. Wengi hawajui wapi h au a inatumika. Mfano wewe ulitakiwa kuandika waandishi. Au mwingine hajui tofauti ya HANA na ANA.
Watu wamekariri hizi herufi 2 TU, lakini tatizo ni kubwa kuliko wanavyodhani.

Acha niendelee kukosea R na L
Hazibadiri maudhui Zaidi Zaidi unapoteza ladha kwa anae kusoma.

A na H: ukoseaji wa hizi unaweza kupoteza maana harisi.
Mfano
Unapokea ujumbe " Bana hatuna sukari na dada anahera.
hii "Dada anahera "imeondoa

Maana nzima ya ujumbe . Lengo ilikua kuonesha kua hakuna pesa.

Ujumbe unasomeka ana pesa.usipo.elewa mapema ,utaona kama dada amekaa na pesa hataki Kununua sukari.

Makosa nimengi ,Kuna ambao Hawana
Dha , wao hutumia (Tha) iwe kuongea hata kuandika. Kama tumeamua kunyosha ni vyema tupite Kila Kona tumlike Kila pembe.
 
Sawa mkuu, haya yote yanatazamwa. Binafsi ninaendelea kujidhatiti katika kuimarisha lugha hii. Na ninakubali kuwa bado najifunza.
 

Tatizo la uandishi, matamshi nadhani pia na uelewa ni kubwa sana. Ukiwa unasoma baadhi ya mada na michango hapa JF utashangaa kabisa uandishi.

Ukifungua online-tv ndio unaishia kupata aibu mwenyewe.
Hata kwenye magazeti ambako habari inaandikwa na mwandishi na kuhaririwa na mhariri huko nako hakuko salama.

Tatizo hili, hasa la kukosea matumizi ya "a" na "ha" limeongezeka sana miaka ya karibuni. Kiswahili ni lugha ya taifa, tumakitumia kila wakati, kila mahali. Nadhani iko haja ya kuangalia kiini cha tatizo
 
Hazibadiri[emoji777]
Hazibadili[emoji736]

Huwa nakereka sana ninapoona mtu anakosea akiwa anamsahihisha aliekosea awali
 
Hazibadiri[emoji777]
Hazibadili[emoji736]

Huwa nakereka sana ninapoona mtu anakosea akiwa anamsahihisha aliekosea awali
Wala usikereke sana mkuu .
Endelea kusahihisha hadi tuzielewe hizi herufi.

Hivi kwa asie sikia anatofautishaje hizi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…