Hivi Rais Magufuli alifanya maamuzi ya busara kwa kuwaita Wakuu wa Vyombo vya Usalama kuongelea COVID19, badala ya kuwaita Wataalamu wa Afya?

Hivi Rais Magufuli alifanya maamuzi ya busara kwa kuwaita Wakuu wa Vyombo vya Usalama kuongelea COVID19, badala ya kuwaita Wataalamu wa Afya?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Tuliona wenyewe Rais Magufuli akiwaita wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini, wengi wakitoka jijini Dar na wengine wakitokea Dodoma, umbali mrefu wa kilometa maelfu, kuongelea ugonjwa wa corona, ambao unatikisa dunia nzima hivi sasa, ikiwemo Tanzania.

Nimekuwa nikijiuliza hivi si yeye mwenyewe ndiye aliyeunda hii Tume ya kitaifa, inayoshughulikia na kuratibu masuala yote ya ugonjwa wa corona nchini, akiwemo waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, mbona sijawaona wakiwa ni miongoni ya waalikwa kwenye kikao hicho?

Hivi Mheshimiwa Rais, anadhani kuwa ugonjwa wa corona utaondoka nchini kwa vifaru vya kijeshi, au mabomu ya machozi, au bunduki "zilizokokiwa" risasi za moto, au magari ya washawasha ya IGP Sirro?

La hasha, asijidanganye, hivyo virusi haviwezi kamwe kuondoka nchini kwa nguvu za kijeshi nchini, kwa kuwa hivyo virusi vya corona ni "invicible enemy"

Kwa kuwa kama nguvu za kijeshi zingekuwa na uwezo wa kuondoa virusi hivyo, basi Taifa kama Marekani linaloongoza duniani kwa nguvu za kijeshi, lisingekuwa linapelekwa "mchakamchaka" hadi sasa hivi likiwa ndilo linaloongoza duniani kwa maambukizi mengi na vifo pia

Mimi sikuona mantiki ya kuwaita wakuu wa vyombo vya usalama wa nchini kuongelea ugonjwa wa Corona nchini, wakati akiwaacha wataalamu wa Afya,ambao hivi sasa ndiyo wako mstari wa mbele kabisa katika vita hii ya kuutokomeza ugonjwa wa Corina nchini.

Kwa kuwa tunadadavua kujua mantiki ya Mheshimiwa Rais, kuwaita wakuu hao wa vyombo vya usalama nchini kwenda kijijini kwake Chato na kwenda kuwahutubia kuhusu suala la kiafya, nawakaribisha sana wadau nanyi mtoe maoni yenu
 
Tujiulize swali lingine, ikiwa Ikulu tunaijua kuwa ipo jijini Dar na Chamwino, Dodoma, iweje Rais wetu afanye kazi na aitishe kikao kikubwa kabisa cha kuitisha wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama, akiwa kijijini kwake Chato?
 
Tujiulize swali lingine, ikiwa Ikulu tunaijua kuwa ipo jijini Dar na Chamwino, Dodoma, iweje Rais wetu afanye kazi na aitishe kikao kikubwa kabisa cha kuitisha wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama, akiwa kijijini kwake Chato?
Gharama iliyotumika kuandaa maigizo ya chato ingeweza nunua saniterzer na barakoa za kutosha mkoa wa geita
 
Hao mnaowaita wataala ni tools zao watawala.
Watawala huwatumia wanataaluma/professionals kama sehemu ya vitendea kazi vyao.

Ukimuona mkulima kabeba jembe, nawe mwanataaluma jifananishe na jembe.
 
Kinachonishangaza hatujui nia ya huyu jamaa ktk nchi yetu anaonekana kbsa hayuko fit kua president alaf watu kama TISS wanaangalia tu,kweli unaeza mpa uraisi hata kingwendu na Tiss wakaufyata tu.
 
Maadui wa taifa hutumia kila mbinu kupata upenyo kufanya wanayotaka. Usidhani kila anayehubiri corona anawaza hilo tu. Maadui wanatumia nafasi ya sisi kuwa busy na corona, wao wataingiza vyao au hata watu wao kwa malengo yao. Hata aliposema angalieni wasijeingiza vitu vya hatari atakuwa ameshanusa harufu ya jambo fulani.

Kwa maadui zetu hata sherehe zetu ni hatari kwetu. Misiba yetu ya kitaifa na ziara za viongozi na wafanyabiashara toka nje ni hatari kwetu. Kwao ni fursa.

Nakumbuka Mkapa akiwa rais kulikuwa na tukio la harusi katika familia yao. Kuna mdau alitaka kuchangia 30m. Mkapa alikataa. Ni mfano tu wa maadui zako wanavyoweza kutumia raha au shida zako kukuteka na kisha kukuangamiza.
 
Lihakanga,
Maadui zetu ni kina nani hao?Aliotuachia mwalimu ni
-Umaskini
-Ujinga
-Maradhi

Kuna maadui wengine wapya?Tutajie hapa!
 
Back
Top Bottom